Sunday, April 21, 2013

WANAFUNZI WAPATA AJALI YA GARI MWANZA

Na. Afisa Habari Mkoa wa Mwanza 

Jumla ya wanafunzi wapatao ishini na saba wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyo lihusisha garia aina ya Roli lililokuwa likisafiri kutoka Kasororo kwenda Misasi kwenye shughuli za Umiseta.
 
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Afisa Michezo wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, nikuwa gari hilo lilikuwa likiwasafirisha wanafunzi kwenda kwenye Michezo ajali imetokea katika Tarafa ya Mbarika Wilaya ya Misungwi Mkoani hapa.
Majeruhi 12 wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Missungwi na kumi na watano(15), walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Bugando kwa Matibabu zaidi.
 
Taarifa hiyo imesema pia kuwa hali ya Majeruhi mmoja sio nzuri sana kwani sehemu kubwa ya kichwa ndio iliyojeruhiwa vibaya, huku mwalimu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja akiwa amechanwa na kitu kinacho zaniwa kuwa ni chuma sehemu ya kifua.
Hata hivyo Ninaendelea kufatilia juu ya tukio hili na habari kamili juu ya Majina ya Majeruhi hao nitawatumia kupitia mtandao wetu wa Mawasiliano.