Wednesday, August 28, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA YA SIKU YA FAMILIA NA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI MAHALA PA KAZI

                                          Wadau wakiwa wanafuatilia semina

                             Wadau wa semina wakifuatilia mafunzo

                                                    Wasanii nao hawakuwa nyuma

                                         Wafuatiliaji wakifuatilia wa Senina

                                                             Muda wa maakuli

                                                        Dkt. Paul Luvanda akitoa mada

                          Scolastica Mlawi akihamasisha watumishi kujimwaga katika muziki

                                                               Muda wa muziki


                                     Ndani ya ukumbi wa SIASA ni KILIMO




                 Washiriki wa siku ya Familia na Mapambano dhidi ya Ukimwi Mahala Pa kazi


                                                 Ndani ya ukumbi muda wa maakuli


                                 Mtoa mada akiwasilisha mada yake


        Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu- Nuhu Mwasumilwe akifunga Semina



RS IRINGA PIMENI AFYA




Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wametakiwa kupima afya zao ili kujitambua na kuchukua hatua dhidi ya maambukizi ya VVU na ukimwi kwa lengo la kuwa na afya njema na kuongeza ufanisi wa kazi.
                            Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala, Scolastica Mlawi

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu, Scolastica Mlawi wakati wa kufungua semina ya siku ya familia na mapambano dhidi ya ukimwi mahala pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Siasa ni Kilimo wilayani Iringa. 

Dkt. Christine amesema “ni vema kila mtumishi apime afya yake ili ajitambue na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwa huduma za kuzuia maambukizi mapya kwa watu ambao hawana maambukizi pia wale wenye maambukizi wasipate maambukizi mengine zinatolewa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali, taasisi na mashirika binafsi”. Amesema kuwa wateja wanaotembelea vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa wanaumwa magonjwa mengine aukusindikiza wagonjwa wanashauriwa kupima VVU. Amesema kuwa huduma hiyo imesaidia sana kuwafanya watu wengi kujua hali za afya zao kuhusiana na maambukizi ya VVU na kuchukua hatua.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawajali sana watumishi wake hasa wanaoishi na VVU. Amesema “serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwajali watumishi wake inatekeleza Waraka Na. 6 wa Mwaka 2006 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambao unamtaka kila mwajiri katika Wizara, Taasisi, Mashirika na Idara za Serikali  kuwasaidia watumishi wanaoishi na V.V.U. kwa kuwapa fedha kidogo kwa ajili chakula na nauli wakati wa kwenda kupata huduma za matibabu”.

Ameendelea kusema kuwa watumishi wamekuwa wakishauriwa kupima afya zao na kutoa elimu ya kuzuia maambukizi mapya. Katika kuonesha msisitizo, ametoa rai tena kwa watumishi kupima afya zao ili wanapogundulika kuwa na maambukizi ya V.V.U. waweze kupata huduma ya ushauri, vipimo, dawa, matibabu kwa magonjwa nyemelezi na mlo kamili.

Akiongelea malengo ya semina hiyo kwa watumishi, Afisa Tawala mwandamizi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Neema Mwaipopo amesema kuwa lengo ni kuelimishana na kukumbushana kujikinga na maambukizi mapya ya ukimwi kwa ambao bado hawajapata na kwa ambao wamepata kujikinga na maambukizi mapya. Amesema kuwa lengo jingine ni kuwahamasisha watumishi kwenda kupima na watakaokutwa wameathirika watoe taarifa kwa mwajiri ili waweze kunufaika na msaada wa huduma kwa mujibu wa Waraka Na. 6 wa Mwaka 2006 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambao unamtaka kila mwajiri kuwasaidia watumishi wanaoishi na V.V.U.

Neema amesema kuwa suala la unyanyapaa halipo kutokana na watumishi kupatiwa elimu ya mara kwa mara. Amesema kuwa utaratibu wa kutoa elimu kupitia semina, vikao na mikutano mbalimbali ni endelevu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Siku ya familia na mapambano dhidi ya ukumwi katika ofisi ya mkuu wa mkoa imeongozwa na kaulimbiu isemayo Iringa bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi inawezekana. 
=30=