Tuesday, February 27, 2018

WAKANDARASI UJENZI BARABARA WATAKIWA KUJIPANGA SAWASAWA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Serikali mkoani Iringa imewataka wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya barabara kujipanga sawasawa katika kutekeleza miradi ya ujenzi ili idumu kwa muda mrefu.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya halfa ya utiaji saini mikataba baina ya TARURA na wakandarasi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
Masenza aliwataka wakandarasi wote walioshinda zabuni za ujenzi wa barabara katika Mkoa wa Iringa kujipanga sawasawa. “Serikali imewekeza pesa nyingi katika ujenzi wa barabara kwa lengo la kujenga na kuimarisha barabara ili mwananchi aweze kunufaika na barabara hizo. Tumesikia katika taarifa ya mratibu wa TARURA Mkoa wa Iringa kuwa gharama za ujenzi wa barabara ni shilingi bilioni 3.56” alisema Masenza. 

Aidha, alitumia hafla hiyo kuwataka wakandarasi wote kufanya kazi kwa kuzingatia muda uliopangwa na viwango vya ubora wa kazi. Serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayefanya kazi chini ya muda uliopangwa kwenye mkataba wala kazi iliyofanywa chini ya kiwango, aliongeza Masenza.

Katika kuhakikisha ubora wa kazi za ujenzi, mkuu wa mkoa wa Iringa aliwataka mameneja wa TARURA wa halmashauri kuwasimamia wakandarasi ili watekeleze majukumu yao. “Serikali imeajiri mameneja wa TARURA katika halmashauri. Jukumu kubwa la mameneja hawa ni kuwasimamia wakandarasi ili watekeleze wajibu wao. Hivyo, mameneja wa halmashauri pia mjipange sawasawa kuhakikisha ubora na thamani ya fedha inapatikana” alisisitiza mkuu wa mkoa.

Mkuu wa mkoa alitoa wito wa kulipwa kwa wakati pindi wakandarasi watakapotimiza wajibu wao kwa kuzingatia vigezo vya ubora kwa mujibu wa mikataba iliyosainiwa. Alisema kuwa kuna wakati malipo ya wakandarasi yamekuwa yakicheleweshwa kutokana na uzembe na kutofuata taratibu. “Utekelezaji huo utawafanya kuongeza morari ya kazi na pia kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima kwa Serikali” alisema mkuu wa mkoa.

Awali mratibu wa TARURA Mkoa wa Iringa, mhandisi Juma Wambura katika taarifa yake alisema kuwa TARURA Mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara za halmashauri zote za Mkoa jumla ya zabuni 26 zenye thamani ya shilingi bilioni 6.5. “Leo utaishuhudia mikataba 18 ikisainiwa na wazabuni walioshinda baada ya mchakato mzima wa manunuzi kukamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 3.56. Mhe. mkuu wa mkoa, mikataba takribani 8 itasainiwa baadae baada ya taratibu za manunuzi kukamilika” alisema mhandisi Wambura.

Mratibu huyo alisema kuwa lengo la TARURA ni kufanikisha dhima kuu ya Serikali kuwa miundombinu ya barabara inaboreshwa na kusonga mbele kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi ili iweze kuboresha uchumi wa wananchi.

TARURA mkoa wa Iringa inahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya Kilomita 4,601.25 inayojumuisha halmashuri tano za Manispaa, halmashauri za wilaya za Iringa, Kilolo, Mufindi na Mji wa Mafinga.
=30=

MIKATABA 18 YA UJENZI WA BARABARA YASAINIWA IRINGA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Jumla ya mikataba 18 imesainiwa na wazabuni walioshinda zabuni yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 mkoani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa Wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa wa Iringa, Mhandisi Juma Wambura katika taarifa fupi ya TARURA iliyowasilikswa kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara na vivuko baina ya TARURA na wakandarasi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa jana.
 
Mhandisi Juma Wambura
Mhandisi Wambura alisema TARURA mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya halmashauri zote za mkoa. 

Mhe. mkuu wa mkoa, TARURA Mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya halmashauri zote za mkoa jumla ya zabuni 26 zenye thamani ya shilingi bilioni 6.5 ambayo leo utaishuhudia mikataba 18 ikisainiwa na wazabuni walioshinda baada ya mchakato mzima wa manunuzi kukamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 3.56” alisema mhandisi Wambura. Alisema kuwa mikataba minane itasainiwa baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.

Mratibu wa TARURA mkoa aliwaasa wazabuni hao kutekeleza miradi hiyo kwa weledi na ufanisi mkubwa pasipo kuchelewesha kama utaratibu wa miaka ya nyuma ulivyokuwa. 

Aidha, ninawakumbusha wazabuni kuacha mazoea ya kutekeleza kazi chini ya kiwango kwa visingizio mbalimbali. TARURA haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayezembea katika utekelezaji wa miradi hii” alisema mratibu wa TARURA. Aliwahakikishia wakandarasi kupata ushirikiano unaostahili katika kutekeleza majukumu yao.

Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya wakala za serikali sura 245 na kutangazwa katika Gazeti la serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017.
=30=

WAKANDARASI WATAKIWA KUJENGA BARABARA KWA VIWANGO

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
SERIKALI mkoani Iringa imewataka wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya barabara kujipanga sawasawa katika kutekeleza miradi ya ujenzi ili idumu kwa muda mrefu.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya halfa ya utiaji saini mikataba baina ya TARURA na wakandarasi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa jana.
 
Mkuu wa Mkoa, amina Masenza
Masenza aliwataka wakandarasi wote walioshinda zabuni za ujenzi wa barabara katika Mkoa wa Iringa kujipanga sawasawa. “Serikali imewekeza pesa nyingi katika ujenzi wa barabara kwa lengo la kujenga na kuimarisha barabara ili mwananchi aweze kunufaika na barabara hizo. Tumesikia katika taarifa ya mratibu wa TARURA Mkoa wa Iringa kuwa gharama za ujenzi wa barabara ni shilingi bilioni 3.56” alisema Masenza. 

Aidha, alitumia hafla hiyo kuwataka wakandarasi wote kufanya kazi kwa kuzingatia muda uliopangwa na viwango vya ubora wa kazi. Serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayefanya kazi chini ya muda uliopangwa kwenye mkataba wala kazi iliyofanywa chini ya kiwango, aliongeza Masenza.

Katika kuhakikisha ubora wa kazi za ujenzi, mkuu wa mkoa wa Iringa aliwataka mameneja wa TARURA wa halmashauri kuwasimamia wakandarasi ili watekeleze majukumu yao. “Serikali imeajiri mameneja wa TARURA katika halmashauri. Jukumu kubwa la mameneja hawa ni kuwasimamia wakandarasi ili watekeleze wajibu wao. Hivyo, mameneja wa halmashauri pia mjipange sawasawa kuhakikisha ubora na thamani ya fedha inapatikana” alisisitiza mkuu wa mkoa.

Mkuu wa mkoa alitoa wito wa kulipwa kwa wakati pindi wakandarasi watakapotimiza wajibu wao kwa kuzingatia vigezo vya ubora kwa mujibu wa mikataba iliyosainiwa. Alisema kuwa kuna wakati malipo ya wakandarasi yamekuwa yakicheleweshwa kutokana na uzembe na kutofuata taratibu. “Utekelezaji huo utawafanya kuongeza morari ya kazi na pia kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima kwa Serikali” alisema mkuu wa mkoa.

TARURA mkoa wa Iringa inahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya Kilomita 4,601.25 inayojumuisha halmashuri tano za Manispaa, halmashauri za wilaya za Iringa, Kilolo, Mufindi na Mji wa Mafinga.
=30=

Tuesday, February 20, 2018

PICHA ZA ZIARA YA NAIBU WAZIRI- MADINI KATIKA MACHIMBO YA NYAKAVANGALA, IRINGA

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA NAIBU WAZIRI BITEKO IRINGA

SERIKALI YATOA MASHARTI MATATU KUFUNGULIWA NGODI WA NYAKAVANGALA

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Serikali yatoa masharti matatu kufungua mgodi wa kuzalisha dhahabu Nyakavangala na kuelekeza yatekelezwe ndani ya wiki mbili.

Masharti hayo ambayo ni kupitisha kanuni za uchimbaji madini, wataalam kutoka wizara ya madini kukagua mashimo yote ya kuchimba dhahabu na mafunzo ya usalama katika machimbo yalitolewa na naibu waziri wa Madini, Dotto Biteko aliyefanya ziara ya siku moja katika mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali wilayani Iringa jana.
 
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (Mb)
Biteko alisema kabla ya kufunguliwa mgodi huo mambo hayo matatu lazima yafanyiwe kazi ili kufanya mazingira ya uchimbaji dhahabu kuwa salama. Katika kuhakikisha mazingira yanakuwa sawa, aliwataka wachimbaji hao kuwa wakweli na wazalengo kwa nchi yao katika kiasi cha dhahabu kinachozalishwa mgodini hapo. Akiongelea utoroshaji madini hayo, alisema “mchimbaji anayedhani serikali ya Dr. John Magufuli anaweza kutorosha dhahabu atafute kazi nyingine” alisema Biteko. 

Aliongeza kuwa serikali ipo makini kuhakikisha madini hayo yanawanufaisha watanzania na kuchangia katika uchumi wa Taifa.

Awali mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa katika kuhakikisha hali ya machimbo dhahabu ya Nyakavangala inakuwa salama, kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa iliagiza ufanyike ukaguzi katika mashimo yote yanayochimba dhahabu katika mgodi huo. Alisema lengo la ukaguzi huo ni kuwahakikishia usalama wachimbaji hao na kuepuka vifo vitokanavyo na mashimo hayo kuanguka.
=30=