Thursday, September 26, 2013

PICHA ZA KLABU YA RAS IRINGA

 MAANDAMANO YA TIMU MBALIMBALI ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA SHIMIWI

 BENDI IKITUMBUIZA 

 KATIBU WA KLABU YA RAS IRINGA NEEMA MWAIPOPO AKIMUELEZEA KAIMU KATIBU TWALA MKOA WA IRINGA  MAANDALIZI YA TIMU HIZO MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA SAFARI

 KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA IRINGA, WAMOJA AYUBU AKITOA NASAHA KWA TIMU

 VIONGOZI WA KLABU YA RAS IRINGA

 WACHEZAJI WA KLABU YA RAS IRINGA AKISIKILIZA NASAHA ZA KAIMU RAS

 TIMU YA RAS IRINGA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA AFISA UTUMISHI, GASTO ANDONGWISYE KASUMO MWAMBIGIJA

 VIONGOZI WA TIMU 

 KATIBU WA KLABU YA RAS IRINGA NEEMA MWAIPOPO (KUSHOTO) NA KOCHA WA TIMU HIYO


 WACHEZAJI WA KLABU YA RAS IRINGA

NAHODHA WA KLABU YA RAS IRINGA AGNES MLULA

KLAB YA RAS IRINGA YAANZA SAFARI YA DODOMA




Na Charles Amulike - Iringa
Timu ya kuvuta kamba (wanawake) ya clabu ya RAS Iringa imeanza safari yake kuelekea mkoani Dodoma kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Idara Serikali, Mikoa na Wizara (SHIMIWI) ikitarajia kurudi na kikombe.

 Katibu wa Clabu ya SHIMIWI ya RAS IRINGA Neema Mwaipopo (kulia) akimueleza Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa maandalizi ya timu


Hayo yamesemwa na Katibu wa SHIMIWI Katika Ofiis ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Neema Mwaipopo wakati wa kuiaga timu hiyo tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Mwaipopo amesema kuwa timu hiyo yenye juml;a ya wachezaji 15 inakwenda mjini Dodoma kushiriki mashindano hayo ya SHIMIWI kwa kucheza na timu za ofisi za wakuu wa mikoa, wizara na taasisi mbalimbali za serkali. Ameongeza kuwa timu hiyo imejiandaa vizuri na kutarajia kurudi na ushindi wa kishindo.

Akiongelea changamoto wakati wa maandalizi ya timu hiyo Nahodha wa timu hiyo, Agness Mlula amesema kuwa wachezaji wengi walishindwa kuhudhuria mazoezi kutokana na wengi wao kunyimwa ruhusa kazini. Amesema pamoja na changamoto hiyo, timu hiyo imejipanga vizuri na wanatarajia kurudi na ushindi katika mashindano hayo.

Timu hiyo inatarajia kurudi mkoani Iringa tarehe 6 Oktoba mwaka huu 2013 mara tu watakapomaliza mashindano hayo. 

Nahodha wa Klabu ya RAS IRINGA, Agness Mlula

=30=

Tuesday, September 17, 2013

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiongea na ujumbe wa wanazuoni kutoka Angola






Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma 





Mkuu wa Mkoa akiongea na Wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Iringa (hawapo pichani) kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu

Mkuu wa Mkoa akiongea na Wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Iringa



Mkuu wa Mkoa wa Iringa (katikati) muda mfupi kabla ya kufunga mafunzo juu ya mbinu za kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja mahala pa kazi kwa watumishi wa TANAPA kutoka hifadhi za kusini yaliyofanyika katika ukumbi wa Neema Craft Manispaa ya Iringa. Kushoto ni Mratibu wa SPANEST, Godwell Meing'ataki na Risala Kabongo (kulia) Afisa Utalii -TANAPA Kanda ya Kusini

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisoma hotuba ya kufunga mafunzo juu ya mbinu za kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja mahala pa kazi kwa watumishi wa TANAPA kutoka hifadhi za kusini yaliyofanyika katika ukumbi wa Neema Craft Manispaa ya Iringa



Mkuu wa Mkoa wa Irinag, Dk.Christine Ishengoma mwenye nguo nyekundu katika picha ya pamoja na wanasena wa TANAPA kanda ya kusini

Makamu wa Rais wa Commercial Seeds Production, Chadjen Ucharattana akimuonesha mahindi Mkuu wa Mkoa wa Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma akiangalia mahindi ya njano toka kwa Makamu wa Rais wa Commercial Seeds Production, Chadjen Ucharattana

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk.Christine Ishengoma (kulia) akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Ujenzi baada ya kukagua barabara ya Iringa-Dodoma (km 260)

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk.Christine Ishengoma (kulia) wakifuatilia hali ya mambo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Ujenzi baada ya kukagua barabara ya Iringa-Dodoma (km 260)

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga (kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa

Katibu wa Kamati ya Itifaki, Ratiba, mapokezi na Malazi, Neema Mwaipopo (kulia) akichangia mada katika kikao cha maandalizi ya Sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana Kitaifa

SIETCO YAONGEZEWA MIEZI 6 KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA YA IRINGA- MIGORI




Serikali imemuongezea muda wa miezi sita mkandarasi anayejenga barabara ya Iringa-Migori ili aweze kukamilisha ujenzi huo na kukabidhi barabara hiyo serikalini. 
 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma (kulia) 
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua mradi wa barabara ya Iringa-Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Dk. Magufuli amesema kuwa Mkandarasi China Sichuan International Cooperation Company Limited (SIETCO) anayejenga barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya kwanza Iringa- Migori (km. 95.2) yupo nyuma, hivyo serikali imemuongezea miezi sita. 

Amesema kuwa baada ya kuongeza miezi hiyo mkandarasi huyo atatakiwa kukabidhi barabara hiyo kwa serikali mwezi Septemba, 2014. Akiongelea sababu zilizomfanya mkandarasi huyo awe nyuma, Dk. Magufuli amesema kuwa eneo la Nyang’oro lilikuwa na milima mikali na kuhitajika nguvu zaidi katika kuikata kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Amesema baada ya kipindi hicho mkandarasi lazima akabidhi barabara na hakuna muda wa ziada utakaoongezwa.

Kutokana na umuhimu wa kimkakati wa barabara ya Iringa- Dodoma yenye urefu wa km 260 utakapokamilika, Waziri wa Ujenzi ameshauri uandaliwe mpango wa kutengeneza barabara za michepuo. Amesema kuwa umuhimu wa barabara hizo za michepuo ambazo zitakuwa haziingii katikati ya mji zitaondoa msongamano wa magari katikati ya mji. Aidha, ameshauri itengenezwe stendi kubwa ya magari nje ya mji ili kupunguza msongamano wa magari mjini.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma ameishukuru serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete kwa kuweka nguvu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini hasa mkoani Iringa. Amesema kuwa Mkoa wa Iringa utaendela kusimamia barabara zote ili ziweze kudumu kwa muda mrefu. Amesema kuwa serikali kupitia wizara ya Ujenzi inafanya kazi nzuri na wale wasiyoiona basi hawana macho alisisitiza Dk. Christine.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma (kulia) akitoa shukrani. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa alitumia majumuisho hayo kumuomba Waziri wa Ujenzi kuiangalia kwa jicho la pekee barabara kuu ya TANZAM sehemu ya mlima Kitonga ipanuliwe ili kuondoa ajali za mara kwa mara na hadha kwa watumiaji wa barabara hiyo. Waziri Dk. Magufuli alilipokea ombi hilo na kuahidi kulitafitia ufumbuzi.

Mkataba wa ujenzi wa mradi wa barabara ya Iringa-Migori (km. 95.2) ulisainiwa tarehe 13 Januari, 2011 kati ya Tanroads na Mkandarasi China Sichuan International Cooperation Company Limited (SIETCO) kwa gharama ya shilingi 84.216 bilioni kwa utekelezaji wa miezi 35.
=30=