Monday, February 3, 2014



HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 37 YA UHAI WA CCM KWENYE UWANJA WA SOKOINE, MBEYA, TAREHE 2 FEBRUARI, 2014
 
 Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, 
Ndugu Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, 
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM   Taifa,
Ndugu Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya   Taifa,
Ndugu Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya   Taifa Mliopo,
Watendaji Wakuu wa Serikali na viongozi wa CCM wa Ngazi Mbalimbali,
Wanachama Wenzangu wa CCM,
 Mabibi na Mabwana 
 
 
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana siku ya leo hapa Mbeya, kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Nawashukuru sana viongozi, wanaCCM na wakazi wote wa Mbeya kwa mapokezi mazuri na ukarimu wenu kwangu na wageni wenzangu tangu tulipowasili jijini hapa jana mpaka sasa.
 
Wakika tutaondoka Mbeya tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ukarimu na upendo wenu kwetu.!hukrani nyingine nazitoa kwa viongozi na wanachama wenzetu wa Mbeya kwa kukubali kuwa mwenyeji wa sherehe hizi. Nafahamu fika kwamba kuandaa sherehe kubwa kama hii si jambo jepesi. Lakini, inafurahisha na kuleta   faraja kwamba, kutokana na moyo wenu wa kujitolea, umahiri na umakini wenu, mambo yamefana sana.  
 
Mwenyekiti wa CCM (T) Rais Jakaya Kikweye akihutubia mamia ya wananchi njini Mbeya
 
 
 
Matembezi ya mshikamano yalifana sana na hapa kiwanjani mambo ni mazuri sana. ongereni sana. Niruhusuni, kupitia hadhara hii, niwapongeze kwa dhati viongozi, wanachama, makada, wapenzi na washabiki wote wa CCM kote nchini kwa kuadhimisha miaka 37 ya uhai wa Chama chetu. Tunafanya sherehe hizi leo kwa vile tarehe 5 Februari, 2014 ni siku ya kazi.
 
Si vyema kuwatoa watu kazini. Ndiyo maana tunafanya madhimisho haya leo. Tunayo kila sababu ya kusherehekea siku hii kwa vifijo na nderemo kama tufanyavyo siku zote. ii ni kutokana na ukweli kuwa CCM ina historia iliyotukuka, kuvutia na kusisimua. Chama chetu kimepata mafanikio makubwa tangu kuasisiwa kwake tarehe 2 Februari, 1977 mpaka sasa.  
 
Tumefanya mambo mengi mazuri kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake. Nchi imetulia, kuna amani na utulivu na maendeleo ya kichumi na kijamii yanazidi kupatikana kila kukicha. Mwenye macho haambiwi tazama.  Ni jambo linalourahisha na kutia moyo na, la kujipongeza kwa kipindi cha miaka 37 kati ya hiyo ikiwa ndani ya mfumo wa vyama vingi, CCM imeendelea kuwa Chama kikubwa na chenye nguvu kuliko vyama vyote hapa nchini. 
 
Aidha, CCM imebaki kuwa chama chenye mafanikio makubwa na kukubalika zaidi na Tatanzania kuliko vyote kwa kila hali na kwa vigezo vyote. Japo wanaojaribu kuiga lakini hawajaweza.
 
Kwa kweli, itawachukua miaka mingi kufikia hata theluthi moja ya hapa tulipofikia sisi. CCM inaongoza na wengine wanafuatia.  Ninyi na mini tunavifahamu vyama kadhaa vya siasa ambavyo vilianzishwa lakini havijapata mafanikio kama Chama chetu na baadhi havikudumu. Baadhi ya vyama na watu walijifanya bundi na kukitabiria kifo Chama cha Mapinduzi. Nilisema wakati ule kuwa CCM haifi na si ajabu vitakufa vyama vyao na CCM wataiacha hapa hapa. Haya kiko wapi CCM ipo haipo? CCM hai siyo hai? CCM ipo, CCM ni hai na wala haina dalili ya ugonjwa wo wote. Wahenga walisema dua la kuku halimpati mwewe na mchimba shimo hujichimbia mwenyewe. /aadhi yao sasa wanahangaika nchi nzima wakitapatapa kujinusuru. Tanakabiliwa na migogoro mikubwa inayotishia uhai wao. Lakini, sisi hatuwaombei mabaya.
 
Ndugu WanaCCM Wenzangu"
Pamoja na ukweli kwamba Chama cha Mapinduzi ni kikubwa, kina nguvu na kimepata ma"aniko makubwa tusije tukalewa mafanikio na kujisahau hata mara moja. Wenzetu wanaendelea kujijenga na wanapata mafanikio ya kiasi chao. Hivyo basi, lazima tuendelee kufanya kazi ya kuimarisha Chama ili kiendelee na hata kizidi kukua na kuwa na nguvu kubwa zaidi. Mtakumbuka kuwa, 4ktoba, '((5 tulianzsha Mradi wa uimarisha Chama kwa lengo la kuelekeza na kuongoza shughuli ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi. uu ni mradi wa tatu katika historia ya CCM. Lazima tufanye kila tuwezalo kuhakikisha kuwa malengo na madhumuni ya Mradi huo yanatekelezwa kwa ukamilifu. atuna budi kutambua kuwa uhai na maendeleo ya CCM sasa na kwa miaka mingi ijayo yatategemea ufanisi wetu katika utekelezaji wa Mradi wa Tatu wa uimarisha Chama.
 
 Ndugu (iongozi na WanaCCM"
Description: http://htmlimg1.scribdassets.com/2djl38adds3g314z/images/2-34b01d28f3.jpg
 
Kwa sababu ya Uchaguzi wa !erikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani kazi ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ina umuhimu wa kipekee. Lazima tupate mafanikio katika jambo hilo kwani yanakipa Chama chetu nguvu ya kutuwezesha kupambana na kupata ushindi katika chaguzi hizo. azi nzuri tuliyo"anya katika utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Chama miaka iliyopita ndiyo iliyotupa mafanikio makubwa. Hivyo basi tukifanya vizuri mwaka huu tutapata ushindi kama ule au hata zaidi. Bila shaka sote tunatambua kuwa kazi ya kuimarisha Chama inahusisha mambo matatu wanza, kujenga na kuimarisha Chama kama taasisi. ili kufanya kazi ya Chama ndani ya umma. Na tatu ni kufanya kazi ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama, sera na maamuzi ya Chama unaofanywa na Serikali na vyombo vyake. Naamini wote mnajua kuwa sizungumzii mambo mapya. Mambo yote matatu tunayajua kwani tumekuwa tunayafanya kwa miaka mingi. Ninachokifanya leo ni kukumbushana juu ya umuhimu wa kuendelea kufanya kazi hiyo ila tuifanye kwa ufanisi zaidi, kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi.
 
 
Ndugu (iongozi Wenzangu"
Jambo la kwanza muhimu kwetu kufanya ni kuona kuwa viungo vyote vya Chama chetu viko kamilifu na vinafanya kazi vizuri. Chama kiwe na wanachama wengi ambao wanatimiza ipasavyo wajibu wao kwa Chama chao. Viongozi wa Chama wawe hodari kufanya kazi ndani ya Chama na ndani ya umma.  Tasiwe mangimeza bali watoke waende kwa wanachama kuimarisha uhai wa Chama. Tuaende kwa wananchi kukisemea Chama, kusikiliza shida zao na kusaidia kutafuta ufumbuzi. Lazima Chama kiwe mlezi na kimbilio la wananchi.   Tukifanya hivyo watu wetu watakuwa na imani na mapenzi na CCM hivyo watakiunga mkono katika chaguzi za dola. Tuhakikishe kuwa
 

vikao vinafanyika ipasavyo kwani vikao ndiyo msingi mkuu wa demokrasia ndani ya Chama. Maamuzi ya Chama hufanywa na vikao siyo kiongozi peke yake. Lazima pia Chama kiwe na uwezo wa rasilimali Fedha na vifaa ili viongozi na wanachama waweze kufanya kwa ufanisi kazi ya Chama ndani ya Chama na nje ya Chama na ndani ya umma.  Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha agizo letu la siku nyingi la kila ngazi ya Chama kuwa na shughuli za kuwaingizia mapato na kuw ana Mfuko wa Uchaguzi. Maagizo haya hayajatekelezwa ipasavyo kote nchini. Uhodari wa uongozi hupimwa kwenye matatizo.
 
Lazima viongozi wa CCM tuwe wabunifu ili tulipatie jawabu endelevu, tatizo la ukwasi hasi. Tatizo linalohatarisha murua wa Chama cha Mapinduzi kwani baadhi ya viongozi na wanachama sasa hawachagui nani anachangia Chama. Tunachukua hata mtu mwenye pesa chafu au wenye nia chafu. ata wanaotoa rushwa nao hupokewa kishujaa badala ya kuwanyanyapaa na kuwaweka mbali nasi. Jambo lingine muhimu kuhusu kuimarisha CCM kama taaasisi ni kuwa na Jumuiya zilizo imara ili kukiongezea Chama wanachama, wapenzi na washabiki wa kukiunga mkono wakati wote na hasa wakati wa uchaguzi. Jambo la mwisho kubwa na muhimu ni kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi kwa viongozi, wanachama kwa wanachama na baina ya viongozi na wanachama. Hii ndiyo silaha ya kuangamiza adui na kujihakikishia ushindi. Unapokosekana umoja na mshikamano, adui hupata nafasi ya kupenya. Ndiyo maana wakati mwingine hata pale tusipostahili kushindwa tunashindwa. Hivyo tuzingatie na kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya CCM ya Umoja ni Ushindi.
 
 Ndugu viongozi na Ndugu Wanahama
 Uwezo na sifa ya Chama cha Mapinduzi kupata ushindi kunategemea pia taswira yake katika jamii. Kama taswira yake ni nzuri Chama hukubalika kwa watu hivyo wanakuwa tayari kukiunga mkono.
 
Kama taswira ya Chama ni mbaya watu hukichukia na hukataa kukiunga mkono. Katika mazingira hayo kushindwa huwa ni dhahiri. 8li mpate ushindi mnalazimika kufanya kazi ya ziada na kutumia nguvu kubwa mno. Aghalabu, ushindi wenyewe huwa mwembamba. !era nzuri za CCM, utendaji mzuri wa Serikali zake na matendo mema na tabia njema za viongozi na wanaCCM hujenga mapenzi ya jamii kwa Chama na hivyo kuungwa mkono. Sera mbaya, utekelezaji mbaya wa Serikali, vitendo vya rushwa, wizi na ubadhilifu huondoa mapenzi ya wananchi kwa Chama. Kuzaa chuki na hupunguza kuungwa mkono na kuhatarisha ushindi. Lazima wakati wote tuhakikishe kuwa taswira ya Chama chetu mbele za watu ni nzuri. Watu wote na mambo yote ambayo yatakuwa kinyume
 

 

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA,KUHUTUBIA TAIFA




 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono
baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo  mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo.



Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele
cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.



@ Hisani ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.

WAMOJA AAPISHWA RASMI IKULU DAR ES SALAAM


 Rais, Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Bibi. Wamoja Ayubu Dickolangwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 
 


 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi nyaraka za Serikali Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Iringa Bibi Wamoja Dickolangwa baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 



Rais Jakaya Kikwete (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wapya wa Mikoa saba ya Tanzania Bara, baada ya kuwaapisha Ikulu Dar es Salaam juzi. Kutoka kushoto ni Mhandisi Dkt. John Ndunguru (Kigoma), Symthies Pangisa (Rukwa), Alfred Luanda (Mtwara), Wamoja Dickolagwa (Iringa), Mhandisi Omari Chambo (Manyara), Jackson Saitabau (Njombe) na Abdallah Chikota (Lindi).
Picha zote kwa hisani ya Picha na Freddy Maro
 

KIKAO KAZI CHA SIKU 7 CHAANZA JIJINI TANGA, KIKIWAHUSISHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO WA SERIKALI

Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangala (Mb.) wanne waliokaa kuanzia kushoto
 


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangala (Mb.) akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali jijini Tanga

Prof. Elisante Ole Gabriel, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo