Tuesday, December 10, 2013

HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA MKOA IRINGA, WAKATI WA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU LILILOFANYIKA 9/12/2013 SIASA NI KILIMO




Ndugu, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa,
Viongozi wa Wanafunzi kutoa Vyuo Vikuu,
Wawezeshaji,
Maafisa Mbalimbali wa Serikali,
Wanafunzi wote wa Vyuo Vikuu,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana,

Awali ya yote napenda kuungana nanyi nyote kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutulinda sisi na Nchi  yetu ya Tanzania tangu tupate uhuru 09/12/1961 hadi leo hii, ikiwa ni miaka 52 Nchi yetu imeendelea kuwa na amani na utulivu pamoja na mafanikio makubwa katika Nyanja za Kiuchumi na Huduma na jamii. Hatuna budi sote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Baraka na ukarimu wake.

Aidha, nichukuwe fursa hii pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanafunzi wa Vyo Vikuu vyote Mkoani Iringa kwa kuhudhuria katika Kongamano hili. Ni imani yangu mtajifunza mengi ambayo yatakuwa na manufaa kwenu na kwataifa kwa ujumla.


Ndugu Washiriki,
Sio rahisi kusherehekea Miaka 52 ya Uhuru bila kukumbuka juhudi zilizofanywa na Baba wa Taifa na Muasisi wa Chama cha TANU katika harakati za kupigania Uhuru. Ni ukweli usiopingika kuwa hali ya nchi yetu ilikuwa duni sana wakati  wa uhuru kutokana na ujenzi wa mfumo wa Ubepari, Ukabaila na Unyonyaji uliojengwa wakati huo na wakoloni.

Hali hii ilihitaji juhudi zenye dhamira ya Kizalendo zilizofanywa kupitia Azimio la Arusha, Siasa ya Ujamaa na kujitegemea, Siasa ni kilimo, Operation Vijiji, Kisomo chenye Manufaa, kuunganishwa kwa TANU na  ASP  na kuzaliwa kwa CCM, kurejeshwa kwa serikali za Mitaa, kuanzishwa kwa Utaratibu wa kung’atuka kwa viongozi(MARAIS) kwa mujibu wa Katiba nk.

Ndugu Washiriki,
Mwaka huu ni mwaka wa 52 wa Uhuru, tumepata maendeleo makubwa katika kipindi chote hiki. Nichambue kwa ufupi wapi “tulikotoka”.

Mwaka 1982 chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa na 7 – 12 ilipitishwa kama maandalizi ya awali kuanzisha serikali za Mitaa nchini.

Nchi ilipopata uhuru haikuwa Taifa ila nchi ya watu wasiozisi milioni 8 wa makabila karibu 126 ambao hawakuwa na mawasiliano ya karibu wala lugha moja ya kitaifa, Tanzania sasa ni nchi na Taifa kamili huru na imara yenye umoja mshikamano, amani na utulivu ikiwa mfano wa kuigwa barani Africa.

Leo hii, Watanzania bila kujali hali halisi ya maisha yao  ya kila siku wanajisikia kuwa huru wana jeuri ya utu wao na wanajisikia kuwa  sawa na binadamu wengine kokote duniani. Wakati wa uhuru na miaka iliyopita baada ya uhuru, nchi haikuwa na wasomi wengi Wazalendo.  Wote tutakumbuka wakati wa uhuru Tanzania bara ilikuwa wahitimu wa kiwango cha Chuo Kikuu 120(wanasheria 2, wahandisi 2, Madaktari wa binadamu 12 na wengineo. Sasa Tanzania bara inao wasomi na wataalam wengi walioshika nafasi za ushauri na uamuzi serikali na katika Taasisi nyeti za kitaifa.

Tulipopata uhuru, kilikuwepo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimoja kilichokuwa na wanafunzi 14 wa kitivo cha Sheria tu. Sasa Tanzania ina vyuo vikuu na vyuo vishiriki zaidi ya 30 ambapo Mkoa wa Iringa unavyo Vikuu 5. Tumepiga hatua kubwa.

Ndugu Washiriki,
Hali ya Miundombinu ya Mawasiliano ilikuwa duni sana mwaka 1961 wakati wa Uhuru.

Mawasiliano ya barabara yalikuwa mabovu ambapo barabara zote zilikuwa za udongo zisizokuwa na Madaraja /Makaravati na zisizopitika wakati waote wa masika. Hakukuwepo na mawasiliano ya simu, Redio wala Televisheni, sasa kuna Televishen, Simu za mkononi, Fax, e-mael na Radio za masafa yote.
Katika kipindi cha miaka 52 ya uhuru wa nchi yetu, barabara zimeboreshwa na mpya kujengwa. Mfano mzuri barabara ya Iringa – Dodoma, Iringa Dar es Salaam, Iringa Mbeya, Iringa Njombe nk. Haya ni mafanikio Makubwa. Haya ni baadhi tu ya mafanikio lakini, tumepata mafanikio katika Nyanja zote, na mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vijana.


Ndugu Washiriki,
Kauli mbiu ya Miaka 52 ya Uhuru ni; “Vijana ni nguzo ya rasilimali watu; Tuwaamini, Tuwawezeshe, na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa letu”.

Mkoa wetu una bahati kubwa ya kuwa na vijana wengi wenye shauku na ari ya kufanya kazi ambao ni rasilimali muhimu sana katika vita ya kupambana na umaskini. Vijana hawa wanawezeshwa na Wadau mbalimbali kupata elimu katika Vyuo Vikuu tulivyo navyo hapa Iringa. Aidha, Mkoa unawahadhiri wengi ambao ni hazina ya mawazo ya kimaendeleo kwa Vijana hawa, wahadhiri hawa hutoa ushirikiano mkubwa kwa Vijana. Hivyo, nitoe wito kwa Vijana kutumia elimu na fursa zilizopo kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla. Kwani Taifa linawategemea sana Vijana.

Aidha, Tuunganishe fikra zetu na nguvu tulizo nazo, tuunde vikundi, tufanye kazi kwa bidii, tutumie muda vizuri, tutambue wajibu wetu katika kulijenga Taifa letu, hakika tutafanikiwa. Fursa za kujiletea maendeleo ni nyingi sana, tuungane pamoja ili tutoke. Naamini tutapata maendeleo makubwa.


Baada ya maelezo haya machache, nimefungua Kongamano hili.

Ahsanteni kwa kunishiliza.

‘Hakuna mahali pa kukanyaga’ msibani kwa Mandela




Waombolezaji wakiwa nje ya makazi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela huko Houghton, Johannesburg, jana. 
Picha na AFP. 

Na Neville Meena, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Decemba 9  2013  saa 9:52 AM

Johannesburg.Makazi ya Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini yaliyopo katika Mtaa wa Laa namba 12, Houghton ambako ndiko alikokuwa hadi alipokutwa na mauti, ni kama hapaingiliki kutokana na wingi wa watu, magari na vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali duniani ambavyo vimeweka kambi katika eneo hilo, usiku na mchana kufuatilia safari ya mwisho ya kiongozi huyo. 

Anga la mtaa huo na sehemu za jirani, limehanikizwa na sauti nyingi za nyimbo zikiongozwa na Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini ‘Nkosi Sikeleli Afrika’ (Mungu Ibariki Afrika), ukifuatiwa kwa zamu na nyimbo za kidini na zile za asili ambazo zinasifu ushujaa wa Mandela.

Katika lango la kuingia kwenye makazi hayo ya Mandela, kuna maombolezo ya aina yake kwani yameambatana na kitu ambacho kwa macho kinaonekana kama shamrashamra kwa nyimbo za sifa na kufurahia kile Waafrika Kusini wanachokiita kazi nzuri ya kutukuka ya Mandela aliyoifanya katika umri wa miaka 95 ya uhai wake.

Mwandishi wetui alitembelea makazi hayo ya Mandela jana na kushuhudia umati mkubwa wa watu wakifika nje ya nyumba yake kwa ajili ya kuomboleza; wakiweka mashada ya maua, mishumaa na kadi zenye ujumbe wa pole kwa familia yake. 

Miongoni mwa waliokuwapo katika eneo hilo ni Mtanzania, Christer Mwageni na watoto wake; Sabina na Faraja.

Mwageni alisema: “Kwa jinsi hali ilivyo, huwezi kukwepa kuwa mwombolezaji, mimi na wanangu tulikuja hapa kutembea tu kwa siku tatu hivi lakini tumejikuta tukishiriki msiba na hata kama tungekuwa hatutaki kushiriki, uhalisia unatulazimisha”.

“Kweli tuna mengi ya kujifunza, inaonekana msiba huu wa Mzee Mandela umewaunganisha zaidi Waafrika Kusini, maana wote bila kujali rangi wala kingine chochote, wanaonekana kuomboleza kwa dhati kutoka mioyoni kabisa.”

Katika eneo hilo la Houghton, ulinzi umeimarishwa na polisi wako kila kona na wamekuwa wakiwaelekeza waombolezaji na watu wengine njia sahihi za kufuata hadi kuyafikia makazi ya Mzee Mandela kutoka na barabara nyingi za kuingia katika eneo kufungwa na nyingine kugeuzwa maegesho ya magari ya waombolezaji.

Kwa ujumla, pilikapilika ni nyingi, lakini katika lango kuu la kuingia makazi ya Mandela, ulinzi ni mkubwa na hakuna anayeruhusiwa kulikaribia isipokuwa wanafamilia, vingozi wa Serikali na watu wengine wenye shughuli maalumu.

 Soweto, Mandela Square

Hali kama hiyo ipo katika makazi yake ya zamani Mtaa wa Vilakazi Na: 8115, Orlando Magharibi, Soweto ambako kuna pilikapilika nyingi zinazoyahusisha makundi ya watu kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini.

Mandela aliishi katika Mtaa wa Vilakazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na alirejea katika nyumba hiyo miaka 27 baadaye alipoachiwa huru na kuishi humo kwa siku kumi na moja kabla ya kuhamia katika nyumba ya aliyekuwa mkewe, Winnie Mandela katika eneo hilohilo la Soweto.

Kama ilivyo Houngton, katika eneo hilo pia ulinzi umeimarishwa na baadhi ya njia zimefungwa kutokana na wingi wa watu na magari. Vyombo vya habari kutoka kila pembe ya dunia navyo vipo vikiendelea kufuatilia maombolezo hayo.

Katika nyumba ya Soweto ambayo sasa ni makumbusho ya Mzee Mandela, idadi kubwa ya watu wanafurika kujifunza historia ya kiongozi huyo na nje vipo vikundi vinavyoimba nyimbo za maombolezo na kumsifu Mandela kwa ushujaa wake.

Eneo la tatu ni Mandela Square lililopo katika Jiji la Sandton, Johannesburg ambako kuna sanamu kubwa ya kiongozi huyo yenye urefu wa mita sita kwenda juu, likimwonyesha katika hali ya kucheza muziki. Iliwekwa katika eneo hilo, Machi 31, 2004.

Katika eneo hilo, pia ulinzi umeimarishwa na askari wanalazimika kusimamia jinsi watu wanaovyoingia na kutoka. Watu wamekuwa wakisimama katika msitari mrefu kupata fursa ya kupiga picha katika sanamu hiyo yenye uzito wa tani mbili na nusu (kilo 2,500).

Pembezoni mwa sanamu hiyo, kama ilivyo Houghton na Malakazi, limetengwa eneo maalumu kwa ajili ya watu wanaoomboleza kuweka maua, nembo, nyaraka na mishumaa.

Maombolezo ya kifo cha Mandela yanaingia katika siku ya nne leo na yataendelea hadi Jumapili ijayo ya Desemba 15 wakati kiongozi huyo atakapozikwa kijijini kwake Qunu, Mthatha Mkoa wa Eastern Cape.

 @Mwananchi

Mizinga nyuki kwa vikundi



Na Zainab Maeda,Mwananchi  
 Posted  Jumanne,Decemba10  2013  saa 12:8 PM

Iringa.Vikundi saba vilivyopo Kata ya Kiwele na Nduli mkoani Iringa vimekabidhiwa mizinga 100 ya nyuki kwa ajili ya ufugaji nyuki ili kujikwamua kiumaskini.

Akikabidhi mizinga hiyo kati ya mizinga 120 Mshauri wa Maliasili Mkoa wa Iringa, Aloyce Mawere kwenye mkutano uliofanyika katika hicho, aliwataka wanakikundi hao kusimamia sheria zilizowekwa ili kufanikiwa katika ufugaji wa nyuki.

Mawere alisema endapo wanavikundi hao watafanyakazi kwa ushirikiano na jamii inayozunguka misitu ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria zilizopo wataona mafanikio na wataachana na umaskini .

Aliongeza kuwa suala la ufugaji wa nyuki ni ajira tosha kwa vijana na si wazee tu “Naomba jamii nzima ielimike kwamba suala la ufugaji siyo kazi ya wazee peke yao pia ni ajira kwa vijana ambao hawana kazi pamoja na akina mama,hivyo sasa hiyo mizinga mliopatiwa mhakikishe mnaitumia ipasavyo na mnaifanyia kazi siyo masnduku ya nguo hayo,” alisema.
@Mwananchi

Obama atikisa msibani




Licha ya kuwa ni siku ya huzuni kwa dunia nzima, hotuba ya Rais wa Marekani, Barack Obama imewagusa maelfu ya watu waliokuwa kwenye Uwanja wa FNB katika ibada ya kitaifa kumwaga Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.



Obama aliyetumia dakika 20 katika hotuba yake iliyokuwa ikikatizwa na kelele za kumshangilia, aliwataka vijana wa Afrika na dunia nzima kuiga maisha aliyoishi Mandela kama yeye alivyojifunza mambo mengi kutoka kwa mzalendo huyo.

“Miaka 30 iliyopita nikiwa mwanafunzi, nilisoma Kitabu cha Mandela na tangu siku hiyo nilijifunza, nikajenga roho ya uthabiti. Iliamsha uwajibikaji kwa ajili yangu na kwa ajili ya watu wangu... hakika Mandela amenifanya niwe hivi nilivyo leo. Michelle na mimi tumenufaika sana na Mandela,” alisema Obama na kuongeza:

“Mandela alinifanya niwe mtu ninayesimama mbele yenu leo, alichangia kunifanya kuwa kiongozi bora. Nitaendelea kuiga mfano wake,”

Katika sherehe hizo, Obama alipokewa kwa shangwe na kushangiliwa kila alipopita na kila alipozungumza tofauti na ilivyokuwa kwa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye alikuwa akizomewa.

Obama alimtaja Mandela kama kiongozi anayefaa kuigwa kwani pamoja na kukaa gerezani kwa miaka 27 akipigania uhuru, hakutaka kung’ang’ania madaraka na badala yake alistaafu kwa hiari yake, tofauti na viongozi wengi wa Afrika.

“Mandela alionyesha uongozi wa vitendo na kujaribu, alikuwa ni mwanamume, binadamu wa kawaida, mume, baba na kiongozi shupavu,” alisema Obama.

Pia Obama alisema, Mandela aliachiwa huru kama mfungwa, lakini kama mwalimu ambaye alitumika kutuonyesha kuwa, ni lazima kuwaamini wenzako ili nao wakuamini.

“Kufundisha upatanisho, hakuhitaji kudharau historia mbaya ya nyuma bali ni kuikabili kwa umakini, ukweli na uhalisia wake. Mandela alibadili sheria, lakini alibadili mioyo yetu pia,” alisema.
Katika risala hiyo, Obama alimtaja Mandela kama mwanamapinduzi mkubwa wa karne ya 20 aliyeibadilisha mioyo ya watu wake, akaimarisha mapatano na maelewano kwa wazungu na weusi.

“Amezaliwa kipindi cha Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, kijana aliyekuwa akichunga ng’ombe na kuteswa na wakubwa zake wa kikabila, lakini ameibuka na kuwa mwanamapinduzi mkuu wa karne ya 20,” alisema Obama.

Vilevile, Obama alimfananisha Mandela na Abraham Lincoln, Rais wa zamani wa Marekani kwa kuiunganisha nchi yake pale ilipokuwa inataka kuvurugika.

Rais huyo aliufanya umati katika uwanja huo ulipuke zaidi kwa furaha baada ya kuzungumza neno la Kizulu, ‘ubuntu’ linalomaanisha utu au ubinadamu ambapo alisema Mandela ameimarisha utu na ubinadamu kwa Waafrika Kusini.

“Alidumisha ‘utu’ miongoni mwetu. Utu ambao tunaweza kuupata kwa kushirikiana na kuwajali wanaotuzunguka,” alisema Rais huyo ambaye anatajwa kuwa Rais wa dunia. Obama alionyesha umahiri wake katika risala hiyo na katika sehemu ya risala hiyo alisema ni wajibu wa kila mmoja kuiga maisha aliyoishi Mandela.

“Ni lazima tujifunze kutoka kwake, kwa sababu Waafrika Kusini kwa jumla wao wameonyesha kuwa, tunaweza kubadilika.”

Obama alimtaja Mandela kama mtu asiyependa kujikweza bali aliyeshiriki kuonyesha mawazo yake na hofu na uhalisia wake hasa kwa kusema kuwa yeye si mtakatifu labda kama mtakatifu ni sawa na mwenye dhambi ambaye hachoki kujaribu. Kiongozi huyo alimalizia hotuba hiyo kwa nukuu muhimu za Mandela zinazosema kuwa, ‘Mimi ni kiongozi wa imani, mustakabali wangu, na mimi ni nahodha wa roho yangu’ na kuwataka Waafrika Kusini kuishi katika maneno hayo ya Mandela katika maisha yao.

“Hakika ilikuwa roho ya ajabu, tutamkumbuka sana. Mungu wabariki Waafrika Kusini,” alimaliza Obama. Kabla ya hotuba hiyo, Obama alifanya jambo la kihistoria kwa kupeana mikono na Rais wa Cuba, Raul Castro, kama ishara ya mapatano baada ya migogoro iliyoko baina ya nchi hizo mbili.

Kabla ya Obama kuzungumza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika hotuba yake alisema kuwa, alijitoa muhanga kwa ajili ya usalama, uhuru na demokrasia ya nchi yake.

“Sherehe hizi za kumbukumbu zinadhihirisha upinde wa mvua wa taifa. Ninatumaini tutaweza kuuona upinde huo punde, kupitia mvua ya simanzi,” alisema Ki-Moon. Ki-Moon alimtaja Mandela kuwa ni kiongozi aliyejiandaa kupoteza kila kitu kwa ajili ya uhuru na demokrasia.

“Dunia imepoteza rafiki na mwalimu. Alikuwa ni zaidi ya viongozi wakubwa wa nyakati zetu; mwalimu mkuu aliyetufundisha kwa mifano,” alisema Ki-Moon.

Wakati huo huo, Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Thanduxolo Mandela kwa niaba ya familia ya Mandela alipata nafasi ya kutoa risala yake kwa Rais huyo na alisema kuwa, familia hiyo ina bahati ya kuwa na mzazi kama Mandela.

“Utakumbukwa daima, hatuwezi kuusahau mchango wako katika familia na katika maisha ya Waafrika Kusini wote,” alisema Thanduxolo.

Baada ya Thanduxolo, walikuja wajukuu na vitukuu wa Mandela kwa niaba ya wajukuu wote, Pumla, Andile na Mbuso Mandela ambao walisema wana mengi waliyojifunza kwa babu yao ambaye walimtaja kuwa kioo cha familia na kuahidi kuwa wataishi na matendo yake.

Mandela atazikwa Jumapili.

@Mwananchi, Jumatano
Decemba 11,  2013

Dunia yaomboleza kifo cha Mandela




 6 Disemba, 2013 - Saa 17:22 GMT 

Mandela atazikwa tarehe 15 mwezi Disemba
Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Nelson Mandela Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii, familia na marafiki wao.
Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Je uko Afrika Kusini? Unaweza kututumia picha au video kuhusu yanayojiri huko na tutayaweka hapa kwenye mtandao wetu. Tutumie picha au ujumbe wako wowote kupitia ukurasa wetu waFacebookbbcswahili
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe wako kupitia ukurasa wetu wa Bofya Facebook ambao kisha nitauweka kwenye mtandao wa Bofya bbcswahili
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa Mzee Mandela, miongoni mwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki na wengine, walijitlea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki na kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na wakatekeleza. Sasa ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya Mandela.''
Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza kijana wa Afrika Dr.
Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu alivyopigania."
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.
Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.
Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."
@bbc.co.uk/swahili/habari/2013/12/131206_mandela_dunia_omboleza.shtml