Sunday, July 21, 2013

MDAHALO WA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA WASOMI





TANGAZO LA MDAHALO
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Integrated Communication and Culture (CICC) anawatangazia vijana wote wahitimu wa vyuo vikuu na wanaosoma katika vyuo vikuu nchini kujitokeza kushiriki katika mdahalo wa fursa za Ajira nchini.
MADA itakayojadiliwa ni Mchango wa Vijana wasomi katika upatikanaji wa Ajira nchini.
Mdahalo huo utafanyika katika ukumbi wa Highland, Iringa siku ya Jumanne tarehe 23/07/2013 kuanzia saa 4:00Asubuhi hadi saa 6:00 Mchana.
Vijana wote waliohitimu vyuo vikuu na wanaosoma katika vyuo vikuu nchini mnakaribishwa.
Mzungumzaji Mkuu katika Mdahalo huo atakuwa Mhe. Mch. Peter Msigwa- Mbunge wa Iringa Mjini.

HAKUNA KIINGILIO

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na;
Bi. Neema Mwamoto,
Mkurugenzi Mtendaji CICC
SLP 554, Iringa
Mob: 0752090900,