Thursday, July 12, 2012



WAGANI KAZI KUWEZESHWA IRINGA


Serikali Mkoani Iringa ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo na wapani kazi ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao wa kukuza kilimo katika maeneo waliyopo na kupunguza umasikini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma wakati akigawa baisketi 373 zenye thamani ya shilingi milioni 54 kwa wagani kazi walioshiriki mafunzo ya ugani kazi mwaka 2009, tukio lililofayika katika uwanja wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dr. Christine Ishengoma 
akikabidhi baiskeli kwa Mganikazi

Dkt. Christine amesema kuwa Serikali ya Mkoa inatambua umuhimu wa Wagani kazi katika kukuza sekta ya Kilimo Mkoani Iringa na kuwakumbusha kuwa Wagani kazi ndiyo mabwana na mabibi shamba katika maeneo yao. Amesema kuwa kutokana na umuhimu huo kwa wakulima, Serikali itaendelea kuwasaidia Wagami kazi hao kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa amra na mbinu bora za kilimo cha kisasa pamoja na kuwapatia nyenzo za kufanyia kazi ili kuleta mapinduzi katika Kilimo Kwanza.

Amesema lengo la kuwakabidhi baiskeli hizo kuwawezesha Wagani kazi hao kuwafikia wakulima wengi kwa urahisi na haraka zaidi. Amesema “nawakabidhi baiskeli hizi ili mkafanye kazi iliyokusudiwa”. Amesema kuwa nilazima wakafanye kazi kwa nguvu zaidi kwa sababu watapimwa kutokana na kazi walizozifanya.

Akiongelea pembejeo za kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa utaratibu utaendelea uleule isipokuwa sasa mawakala watatoka juu ambao watasambaza pembejeo hizo wenyewe kwa wakulima na kuwataka wakuu wa Wilaya kusimamia vizuri zoezi hilo ili pembejeo ziweze kuwafikia walengwa.

Katika Taarifa fupi ya utendaji kazi wa Wagani kazi Mkoani Iringa iliyowasilishwa na Shenal Nyoni, Afisa Kilimo Mkuu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, imesema kuwa mwanzoni wa mwaka 2000 Mkoa w Iringa ulikuwa unakabiliwa na tatizo la uhaba wa wataalam wa kilimo na mifugo katika ngazi ya Kijiji na Kata baada ya Serikali kusimama katika kuajiri wataalamu katika Sekta ya Kilimo pamoja na Sekta nyingine.

Amesema kutokana na hilo Mkoa wa Iringa ulibuni utaratibu wa kuwa na Wagani kazi ambao watasaidia kutoa huduma za ugani kwa kushirikiana na wataalam wa kilimo na mifugo vijijini.

Nyoni amesema kuwa mafunzo kwa Wagani kazi yalifanyika katika kila Halmashauri kwa muda wa wiki mbili na Wagani kazi 406 walipatiwa mafunzo kwa lengo la kufundisha Wagani kazi 50 katika kila Halmashauri. Amesema kuwa Wagani kazi hao walifundishwa juu ya kanuni za kilimo na ufugaji bora na fursa ya kujifunza kwa vitendo.

Akionglea mgawanyo wa baiskeli hizo katika mabano, Afisa Kilimo huyo amesema kuwa Manispaa ya Iringa (22), Wilaya ya Iringa (58), Wilaya ya Kilolo (50), Wilaya ya Mufindi (50), Wilaya ya Njombe (50), Njombe Mji (44), Wilaya ya Ludea (49), Wilaya ya Makete (50)  


Ikumbukwe kuwa baiskeli hizo ni ahadi aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipofungua mafunzo ya wiki mbili kwa ajili ya Wagani kazi katika Mkoa wa Iringa mwaka 2009. 



Viongozo wa Mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na Waganikazi muda mfupi baada ya kukabidhiwa baiskeli zao





=30=

No comments:

Post a Comment