Monday, September 3, 2012

WAUGUZI WAMETAKIWA KUTUMIA MAFUNZO KUBORESHA UTOAJI HUDUMA



Wauguzi Mkoani Iringa wametakiwa kutumia mafunzo waliyopata ya kuwajengea uwezo katika kutoa huduma nzuri kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao ili mwananchi aweze kunufaika na huduma zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Robert Salim alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo katika utoaji huduma Wauguzi kutoka katika taasisi za serikali na binafsi Mkoani hapa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dr. Robert Salim akifunga mafunzo ya Wauguzi


Dkt. Salim amesema “tumieni mafunzo mliyoyapata katika kuboresha huduma za afya katika mkoa wetu wa Iringa”. Amewaasa wauguzi hao kuwa wanao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa kufuata miiko na maadili ya taaluma zao katika kuihudumia jamii. Amesema lengo la ushirika baina ya serikali na sekta binafsi ni kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora kwa upande mmoja na mtoa huduma kuendelea kutoa huduma katika mazingira salama. Amesema kuwa mafunzo hayo pia yamelenga maeneo yenye changamoto hatarishi kama kuzuia maambukizi ya maradhi baina ya mtoa huduma na mpokea huduma, maadili kwa wauguzi na jinsi ya kupambana na kuzuia magongwa ya kuambukiza.

Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa amewataka waganga wakuu wa Wilaya kuanza kufikiria kuingiza katika bajeti na mipango ya maendeleo ya Halmashauri programu za mafunzo ya kuwajengea uwezo wauguzi ili kuyafanya mafunzo hayo yawe endelevu hata baada ya mradi huo kukamilika mwishoni mwa mwaka 2013.

Akielezea matarajio baada ya mafunzo hayo, Mratibu wa mafunzo, Veronica James amesema kuwa matarajio yake ni wauguzi kutoa huduma kitaalamu na kitaaluma zaidi, na uwezo wa kufikisha huduma bora kwa wananchi. Amesema lengo la mafunzo hayo kutolewa kwa wauguzi katika mkoa wa Iringa pia ni kupunguza na hatimae kuondoa kabisa dhana ya huduma zisizo za kuridhisha kwa baadhi ya wauguzi Mkoani Iringa.

James ambae pia ni Meneja wa Hospitali ya Agakhan- Iringa amesema kuwa ili huduma ziweze kuwa bora zaidi dhana ya ushindani lazima ijengeke niongoni mwa wauguzi katika kutoa huduma bora. Amesema kuwa pamoja na kwamba baadhi ya mambo wauguzi wameyasoka wakiwa vyuoni lakini ipo haja ya kuendelea kuwakumbusha ili kuwaamsha zaidi katika kukabiliana na changamoto na utoaji huduma za kila siku.

Meneja wa Agakhan Hospitali Veronica James akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari hawapo pichani

Akielezea mafanikio ya mradi huo, Daidu Beyai, Mratibu wa Mradi huo amesema kuwa lengo mahususi la mradi huo ni kuwajengea uwezo wauguzi ili waweze kutoa huduma bora za afya katika Mkoa wa Iringa kwa kuwaongezea ulimu na ujuzi. Ameyataja mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu kuwa ni kuwapatia mafunzo wauguzi 510 katika Mkoa wa Iringa. Amesema katika kufuatilia utekelezaji na ufanisi wa mafunzo hayo kwa wauguzi, tathmini imekuwa ikifanyika kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo ili kuona kama mafunzo hayo yanatoa matokeo chanya. Amesema kwa mujibu wa tathmini hiyo wauguzi waliopatiwa mafunzo hayo wameendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuongeza elimu na ujuzi.   

Akielezea umuhimu wa mafunzo hayo, Eligia Lwela, Muunguzi katika hospitali ya Wilaya ya Mufini, amesema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kuboresha utoaji wake huduma na kuleta ufanisi mkubwa wa kazi yake. Aidha, ameomba mafunzo hayo yawe endelevu ili yaweze kuwafikia wauguzi wote katika Mkoa wa Iringa.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wauguzi katika Mkoa wa Iringa yamefadhiliwa na Shirika la misaada la Marekani kupitia mradi wa Intra Health na kusimamiwa na Hospitali ya Agakhan Iringa.

Sunday, August 26, 2012

VYOMBA VYA HABARI VYATAKIWA KUENDELEA KUHAMASISHA SENSA




Vyombo vya habari Mkoani Iringa vimeshauriwa kuendelea kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili liweze kufanikiwa katika Mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma muda mfupi baada ya kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza usiku wa Kuamkia leo nchini kote.
Dkt. Christine amesema kuwa zoezi hilo vimeanza vizuri na mdadisi ameonekana kubobea katika kazi hiyo. Aidha, amewamwagia sifa wakufunzi na wadadasi kwa jinsi walivyoonesha juhudi katika kufundisha na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu uelewa wa zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi.
 Dr. Christine Gabriel Ishengoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Sensa ya Mkoa amevipongeza vyombo vya habari vya Mkoa wa Iringa kwa weledi katika kuhamasisha zoezi hili. Amesema uhamasishaji ni muhimu sana katika kutoa hamasa kwa kazi ya Sensa ili asitokee mtu ambaye atakuwa hakupata taarifa na elimu juu ya umuhimu wa Sensa na kuhesabiwa. Aidha, ametoa wito kwa vyombo hivyo kuendelea na uhamasishaji huo kwa kipindi cha wiki nzima ili kulifanikisha zoezi hili katika Mkoa wa Iringa. “kufanikiwa kwa zoezi hili Mkoani Iringa sit u kutakuwa na manufaa kwa Mkoa wetu, bali kwa nchi nzima na jambo hili litafikiwa pale tu wananchi wote watakapokuwa wameelewa umuhimu wa zoezi hili na kushiriki katika kulifanikisha” alisisitiza Dkt. Christine.

Akiongelea matukio yasiyo ya kawaida katika zoezi hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Iringa amesema kuwa zoezi hilo limeanza katika hali ya utulivu mkubwa na hakuna tukio lolote lisilo la kawaida lililotokea na kuripotiwa. Aidha, amewata wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa pindi watakapopita katika maeneo yao na kujibu kwa usahihi maswali watakayokuwa wakiulizwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka, akitoa maoni yake baada ya kuhesabiwa asubuhi ya leo amesema kuwa kazi ya kuhesabu na kuhesabiwa ni jukumu la kila mtanzania pasipo kujali mipaka ya aina yoyote. Amesema kila mtanzania anayo haki ya kuhesabiwa katika Sensa hii ili kuhakikisha Serikali yake inapata taarifa sahihi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mpaka amesema “miongoni mwa michango ya wananchi katika jitihada za kujiletea maendelea kwa kushirikiana na Serikali yao ni pamoja na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka huu”. Amesema zipo njia mbalimbali za kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kipindi hiki kutoa taarifa sahihi ni jukumu namba moja ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi. 

Sensa ya Watu na Makazi inafanyika kwa mara ya tano nchini ikiongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Sensa kwa Maendeleo, jiandae kuhesabiwa’ ipo katika siku yake ya kwanza nchini kote na itaendelea kwa siku saba ili kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa mara moja tu.
=30=

SENSA YAANZA VIZURI MUFINDI



Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Wilayani Mufindi limeanza kwa hali ya utulivu mkubwa na wananchi wameendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

Akiongea katika mahojiano maalumu na na gazeti la Uhuru, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu amesema kuwa katika siku ya kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi Wilayani Mufindi, “kwa kweli zoezi hili lilianza saa sita kamili usiku katika maeneo ambayo si ya makazi ya kudumu, kazi ilifanyika katika Mji wa Mafinga katika maeneo ya stendi, nyumba za kulala wageni na maeneo yanapopaki magari makubwa ya mizigo. Aidha, zoezi kama hilo lilifanyika pia katika maeneo ya Nyololo, Igowole, Kibao, Malangali, Ihowanza, Mgololo na Usokami hadi asubuhi saa kumi na moja kazi hiyo ilikuwa imekamilika kwa mafanikio makubwa”. Amesema kuwa leo asubuhi pamoja na kuanza zoezi kwenye makazi ya watu, wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vyote vya huduma wamehesabiwa asubuhi na zoezi linaendelea kwenye makazi ya kudumu ya watu.

Akiongelea tathmini yake, amesema kuwa kazi ya kuhesabu watu inaendelea vizuri sana na muitikio wa watu ni mkubwa sana katika zoezi hilo. Amesema ukubwa wa muitikio wa watu katika wilaya yake unatokana uhamasishaji mkubwa unaoendelea kufanyika na kiu kubwa waliyonayo wananchi ya kushirikiana na Serikali katika kujiletea maendeleo.

Evarista ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amesema kuwa ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa asilimia 100, viongozi na jamii kwa ujumla hawana budi kuendelea kutoa hamasa na elimu ili wananchi wote waweze kushiriki kikamilifu katika upatikanaji wa takwimu hizo muhimu kwa mustakabali wa taifa. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa wanaoendelea kupita katika kaya zao kukusanya taarifa mbalimbali. Amesema wananchi watakapo jibu kwa usahihi maswali watakayoulizwa na makarani wa Sensa watakuwa wametimiza wajibu wao wa kushiriki katika kupanga mipango ya maendeleo yao kwa namna moja ama nyingine.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Iringa, Fabian Fundi amesema, “kwa ujumla zoezi hili linaenda vizuri na tulianza saa sita usiku na kuendelea nalo hadi alfajiri. Na asubuhi hii tumeanza kuhesabu kaya binafsi ambazo ni makazi ya kudumu ya watu”. Amesema kuwa kamati ya Sensa Mkoa haijapata taarifa wala matukio yasiyo ya kawaida wala kupokea simu yoyote kutoka kwa makarani kutaarifu kuwa kuna mtu au kaya iliyogoma kuhesabiwa, hii ni dalili nzuri kuwa zoezi hili litakuwa la mafanikio katika Mkoa wa Iringa.

Sensa ya Watu na Makazi inafanyika kwa mara ya tano nchini kote ikiongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Sensa kwa Maendeleo: Jiandae kuhesabiwa’ ipo katika siku yake ya kwanza na itaendelea kwa siku saba ili kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa mara moja tu.
=30=

VYOMBO VYA HABARI IRINGA VYATAKIWA KUENDELEA KUHAMASISHA SENSA



Vyombo vya habari Mkoani Iringa vimeshauriwa kuendelea kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili liweze kufanikiwa katika Mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma muda mfupi baada ya kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza usiku wa Kuamkia leo nchini kote.
Dkt. Christine amesema kuwa zoezi hilo vimeanza vizuri na mdadisi ameonekana kubobea katika kazi hiyo. Aidha, amewamwagia sifa wakufunzi na wadadasi kwa jinsi walivyoonesha juhudi katika kufundisha na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu uelewa wa zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Sensa ya Mkoa amevipongeza vyombo vya habari vya Mkoa wa Iringa kwa weledi katika kuhamasisha zoezi hili. Amesema uhamasishaji ni muhimu sana katika kutoa hamasa kwa kazi ya Sensa ili asitokee mtu ambaye atakuwa hakupata taarifa na elimu juu ya umuhimu wa Sensa na kuhesabiwa. Aidha, ametoa wito kwa vyombo hivyo kuendelea na uhamasishaji huo kwa kipindi cha wiki nzima ili kulifanikisha zoezi hili katika Mkoa wa Iringa. “kufanikiwa kwa zoezi hili Mkoani Iringa sit u kutakuwa na manufaa kwa Mkoa wetu, bali kwa nchi nzima na jambo hili litafikiwa pale tu wananchi wote watakapokuwa wameelewa umuhimu wa zoezi hili na kushiriki katika kulifanikisha” alisisitiza Dkt. Christine.

Akiongelea matukio yasiyo ya kawaida katika zoezi hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mkoa wa Iringa amesema kuwa zoezi hilo limeanza katika hali ya utulivu mkubwa na hakuna tukio lolote lisilo la kawaida lililotokea na kuripotiwa. Aidha, amewata wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa pindi watakapopita katika maeneo yao na kujibu kwa usahihi maswali watakayokuwa wakiulizwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka, akitoa maoni yake baada ya kuhesabiwa asubuhi ya leo amesema kuwa kazi ya kuhesabu na kuhesabiwa ni jukumu la kila mtanzania pasipo kujali mipaka ya aina yoyote. Amesema kila mtanzania anayo haki ya kuhesabiwa katika Sensa hii ili kuhakikisha Serikali yake inapata taarifa sahihi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mpaka amesema “miongoni mwa michango ya wananchi katika jitihada za kujiletea maendelea kwa kushirikiana na Serikali yao ni pamoja na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka huu”. Amesema zipo njia mbalimbali za kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kipindi hiki kutoa taarifa sahihi ni jukumu namba moja ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi. 

Sensa ya Watu na Makazi inafanyika kwa mara ya tano nchini ikiongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Sensa kwa Maendeleo, jiandae kuhesabiwa’ ipo katika siku yake ya kwanza nchini kote na itaendelea kwa siku saba ili kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa mara moja tu.
=30=

Wednesday, August 22, 2012

...AMIA HUKU DIGITALI



Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma amesema kuwa elimu kwa umma ni nyenzo muhimu sana katika kuwaandaa wananchi kuhama kutoka katika mfumo wa utangazaji wa analojia na kuingia katika mfumo wa digitali.

Ameyasema hayo katika mkutano wa viongozi wa mkoa wa Iringa kuhusiana na mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda digitali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu Huria, tawi la Iringa.

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisoma hotuba yake

Picha ya Pamoja ya washiriki wa Warsha hiyo

Amesema katika kufanikisha jitihada hizo, “umeonekana umuhimu wa kuelimisha umma kwa kushirikisha wizara, idara za Serikali pamoja na wananchi wote ili kuweza kufanikisha mabadiliko haya kwa ufanisi bila kuathiri upatikanaji wa huduma za utangazaji nchini”. Ameishauri kamati maalumu ya kitaifa inayofanya kazi ya kuwaelimisha wananchi nchini juu ya mabadiliko ya teknolojia ya utangazaji kuhakikisha wananchi wengi wanapata elimu hiyo ili kuwaandaa na mabadiliko hayo. Amesema maana ya mabadiliko ya teknolojia, matarajio ya baada ya mabadiliko na wajibu wa mwananchi katika kufanikisha mabadiliko hayo ni mambo ya muhimu kutiliwa mkazo katika utoaji wa elimu kwa wananchi.

Akiongelea Sensa ya Watu na Makazi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ametoa wito kwa washiriki hao kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi. Amesema “natoa wito kwenu washiriki wa mkutano huu hasa waandishi wa habari kutumia nafasi hii kuhimiza jambo hili na kutumia muda wenu na vyombo vyenu kuwaelimisha wananchi ili waweze kushiriki katika zoezi hili na kulifanya liwe la manufaa na kuleta tija katika Mkoa wetu wa Iringa na Taifa kwa ujumla” alisisitiza Dkt Christine.
=30=