Saturday, April 28, 2018
Rushwa Yatakiwa Kuwa Historia Iringa -Prof Kahyarara
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imetakiwa
kuhakikisha rushwa inakuwa historia mkoani hapa kwa kushughulikia taarifa za malalamiko
ya rushwa kutoka kwa wananchi ili waendelee kuwa na Imani na taasisi hiyo.
Rai
hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyararavalipotembelea
banda la TAKUKURU katika maonesho ya shughuli na huduma za wafanyakazi
yanayoendelea katika uwanja wa Kichangani mjini Iringa jana.
| Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Kahyarara alipotembelea banda la TAKUKURU Iringa |
Prof.
Kahyarara alisema kuwa TAKUKURU ina wajibu wa kuhakikisha rushwa inakomeshwa
mkoani Iringa ili wananchi waweze watekeleza majukumu yao. Alisema kuwa rushwa
imekuwa ikikwamisha maendeleo ya wananchi na kuwanyima haki ya kupata huduma.
“TAKUKURU mnawajibu wa kuifanya Iringa kuwa eneo huru dhidi ya rushwa. Na huu
ndiyo wajibu wenu wa msingi” alisema Prof. Kahyarara.
Awali
afisa muelimishaji wa TAKUKURU mkoa wa Iringa, Aneth Mwakatobe alieleza kuwa
hali ya rushwa mkoani Iringa imeendelea kushuka katika miaka ya hivi karibuni.
Alisema kuwa hali ya rushwa imeendelea kushuka mkoani hapa kutokana na uelewa
wa wananchi kuwa mkubwa.
“TAKUKURU mkoa
wa Iringa imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusiana na jinsi ya kukabiliana
na rushwa. Katika kuonesha uelewa mkubwa kwa wananchi, wananchi wameendelea
kutoa taarifa kwetu na kusaidia uchunguzi kufanyika na kutoa matokea chanya”
alisema Mwakatobe.
Afisa
huyo aliyataja maeneo yanayolalamikiwa kuwa na vitendo vingi vya rushwa ni yale
ambayo watoa huduma wake wanakutana na wananchi moja kwa moja. Alitolea mfano
wa maeneo hayo kuwa ni halmashauri, polisi, mahakama, ardhi, na afya.
TAKUKURU
ni moja ya waoneshaji wa huduma katika mabanda ya maonesho ya Mei Mosi kitaifa
yanayofanyika katika viwanja vya kichangani mjini Iringa yakitangulia sherehe
ya Mei Mosi kitaifa itakayohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
=30=
Wafanyakazi Rasilimali Muhimu Uchumi wa Viwanda- Waziri Mwijage
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wafanyakazi
ni rasilimali muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kukuza pato la
nchi ikilinganishwa na rasirimali nyingine zote.
Kauli
hiyo ilitolewa na waziri wa viwanda na biashara, Charles Mwijage alipokuwa akifungua
kongamano la Tanzania ya viwanda lililofanyika katika ukumbi wa Kichangani
mjini Iringa jana.
| Waziri wa viwanda na biashara, Charles Mwijage |
Waziri
Mwijage alisema kuwa nchi ina rasilimali nyingi sana. Rasilimali muhimu
aliitaja kuwa ni rasilimali wafanyakazi. Alisema kuwa wafanyakazi ni muhimu
katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kukuza pato la taifa.
Akiongelea
uchumi wa kati, waziri huyo alisema kuwa uchumi wa kati unategemea shughuli za
watu katika kujenga viwanda vinavyochakata na kusindika malighafi za mazao ya
shamba.
Dhamira ya serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa na sekta ya viwanda
iliyo imara, shindani na endelevu. Alisema kuwa viwanda vinavyoongelewa siyo
viwanda vya kufa kama binadamu, bali ikitokea vikafa, vinazaliwa vingine na
kuendeleza nyororo wa thamani. Alisema kuwa watu wengi wamekuwa na mtazamo
tofauti wa dhana ya kiwanda, alisisitiza kuwa mtu akiwa na cherehani nne hicho
tayari ni kiwanda kidogo. Viwanda vidogo vinasaidia kupunguza kusafirisha mazao
na hatari ya mazao hayo kuharibika wakati wa usafirishaji wake.
Waziri
Mwijage alitoa wito kwa jamii kuwashawishi wafanyakazi kuanzisha viwanda
tofauti na utaratibu wa sasa wa kukopa kwa ajili ya kununua magari. Aidha,
alizitaka mamlaka za serikali za mitaa kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji
wa viwanda. Alishauri viwanda vinavyoanzishwa viwe vinavyoongeza thamani.
Waziri
Mwijage, alisema kuwa mipango iliyopo ni kuufanya uchumi ujikite katika
maendeleo ya watu. “Uchumi tulionao ni wa
maendeleo ya vitu zaidi kuliko maendeleo ya watu, hivyo tunataka kufanya
mageuzi ya maendeleo ya watu ambayo yanapimwa kwa vitu vitatu”. Alivitaja
vitu hivyo kuwa ni elimu, afya na kipato kitakachopatikana kutokana na uchumi
wa viwanda.
Alisema
kuwa serikali inajukumu la kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji.
=30=
RC MASENZA IRINGA ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA MEI MOSI 2018
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ameridhishwa na hali ya
maandalizi ya mabanda ya maonesho ya shughuli na huduma zinazofanywa na
wafanyazi nchini.
Akitoa hali ya tathmini ya mabanda ya
maonesho baada ya kuyatembelea jana jioni mbele ya waandishi wa habari katika
uwanja wa maonesho wa Kichangani, Masenza alisema kuwa ameridhishwa na hali ya
mabanda.
| Mkuu wa Mkoa wa Iringa, akipokelewa na Meneja wa TTCL Iringa |
“Hadi sasa mabanda yamekwisha
pambwa vizuri na huduma na bidhaa mbalimbali zimeanza kuoneshwa mezani na
wananchi wakitembelea mabanda hayo makumi kwa mamia”. Aidha, alitoa rai kwa
wajasiriamali wa mkoa wa Iringa kuendelea kujitokeza kuonesha bidhaa zao kwa
sababu nafasi za mabanda bado zipo. Alisema maonesho ya bidhaa na huduma za
wanafanyakazi ni fursa nzuri kujitangaza na kutangaza huduma na bidhaa
zinazofanywa na wafanyakazi ndani na nje ya mkoa.
Mkuu wa mkoa amewataka wananchi wote
katika Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kutembelea
mabanda na kujionea bidhaa na huduma zinazooneshwa pamoja na kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusu masuala afya na usalama mahala pa kazi. Alisema kuwa
maonesho hayo yatafunguliwa rasmi tarehe 27/4/2018.
Awali mkuu wa mkoa alitembelea uwanja
wa michezo wa Samora kuangalia ukarabati kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za
Mei Mosi, 2018.
Mkoa wa Iringa ni mwenyeji wa
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei Mosi) kitaifa na mgeni rasmi atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
=30=
Wednesday, April 25, 2018
WASICHANA MIAKA 14 KUCHANJWA DHIDI YA SARATANI YA KIZAZI IRINGA
Na.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wasichana wenye umri wa miaka 14
mkoani Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea huduma
za chanjo ili kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.
Rai hiyo ilitolewa na mkuu wa
mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akizindua chanjo mpya ya saratani ya
mlango wa kizazi mkoani Iringa iliyofanyika katika uwanja wa mashujaa mjini
Mafinga jana.
| Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akikata utepe kuzindua utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mjini Mafinga |
Masenza alisema kuwa serikali
imeanzisha chanjo mpya ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri
wa miaka 14 nchini. Alisema kuwa chanjo hiyo ina lenga kuwakinga wasichana hao
dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
“Serikali inawaomba wananchi
wetu wawahimize walengwa wote kufika katika kituo cha kutolea huduma za chanjo
na akina mama nao wajitokeze kwa wingi ili waweze kufanyiwa uchunguzi dhidi ya
ugonjwa wa saratani. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwakinga na magonjwa na
vifo, hii itaiwezesha serikali kutumia fedha ambazo zingetumika kugharamia
matibabu zitumike katika miradi mingine ya maendeleo” alisema Masenza.
Alisema kuwa, chanjo ni
uwekezaji katika uchumi wa taifa, serikali inatoa chanjo bila malipo katika
vituo vya serikali, binafsi na mashirika ya dini na yasiyo ya kiserikali.
Kwa kuwa chanjo ni uwekezaji
katika uchumi wa Taifa, serikali hutoa chanjo hizi bila malipo katika vituo
vyote vinavyotoa huduma za chanjo vikiwemo vya serikali, binafsi, mashirika ya
dini na yasiyo ya kiserikali.
=30=
Sunday, April 22, 2018
RAS Iringa Netboli yaibugiza Ngorongoro Magoli 54-3
Timu ya Netiboli ya RAS Iringa imeiduwaza timu ya netiboli ya
mamlaka ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwa kuibugiza magoli 54-3.
Katika mchezo ulioanza kwa kasi kubwa ilionekana dhahiri kabisa
kuwa timu ya RAS Iringa imedhamiria kuibuka na ushindi ambapo dakika za mwanzo
walionekana kuwapeleka kasi Ngorongoro jambo lilitotafsiriwa na wengi kuwa timu
hiyo toka kaskazini mwa nchi ilipata hofu hata kabla ya mchezo.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa chuo kikuu cha kikatoliki
cha Ruaha (RUCU) ulishuhuriwa na mamia ya wananchi wapenda michezo.
Baada ya mchezo huo, mratibu wa timu zote za RAS Iringa, Issa
Matea alisema kuwa ushindi huo ni salamu za awali kwa timu pinzani. Akiongelea
ushindi huo, alisema kuwa ni ushindi huo ni chachu na hamasa aliyoitoa katibu
tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu kwa timu hiyo yenye wanadada mahiri.
=30=
RAS Iringa yaiburuza 2-0 MUHAS Kamba
Timu ya kuvuta kamba ya RAS Iringa wanawake imeishinda timu ya
kuvuta kamba ya MUHAS wanawake kwa mivuto 2-0. Katika mvutano wa aina yake
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege na kushuhudiwa na mamia
ya wapenda michezo wa mkoa wa Iringa na wageni kutoka sehemu mbalimbali
waliofika mkoani hapa kwa ajili ya sherehe za Mei Mosi, 2018.
Akiongea baada ya mvutano huo, Mratibu wa timu zote za RAS
Iringa, Issa Matea alisema kuwa timu ya RAS Iringa maarufu kama Kisiki imepata ushindi huo kutokana na
mshikamano na kujituma. Alitoa rai kwa timu washindani kuwa chonjo kwa sababu
timu hiyo inalojukumu moja tu katika michezo hiyo.
Alilitaja jukumu hilo kuwa
ni kulinda heshima ya mkoa wa Iringa kwa kuibuka na ushindi katika mivuto yote
katika michezo ya Mei Mosi, 2018.
=30=
Subscribe to:
Posts (Atom)