Thursday, January 3, 2013
Wednesday, December 12, 2012
HOTUBA YA
MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA IRINGA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KAZI NJE-NJE KWA
MKOA WA IRINGA TAREHE 12/12/2012 KATIKA UKUMBI WA CHUO KIKUU HURIA IRINGA.
Mheshimiwa Mkuu wa
Wilaya ya Iringa,
Mhe. Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Iringa,
Mhe. Kaimu Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Mkurugenzi PROMISE
Tanzania,
Viongozi wa Serikali,
Viongozi wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Viongozi wa Taasisi za Dini,
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote natumia fursa hii kutoa
shukrani kwa waandaaji wa uzinduzi wa mradi huu ambao una umuhimu mkubwa kwa
maendeleo ya Vijana wa Mkoa wa Iringa.
Aidha, nawakaribisha wote katika uzinduzi
wa mradi huu, mradi huu binafsi, nimeupenda kwa kuwa malengo yake ni kuelimisha
kundi kubwa la Vijana ili liweze kujiajiri na kufanya kazi kwa maendeleo ya
Taifa.
Nawashukuru
PROMISE
kwa kushirikiana na ILO kwa kuandaa mpango huu wa kusaidia vijana kupitia Mradi wa
Kazi Nje - Nje kwa Vijana wa Mkoa wa
Iringa, hususani kwa Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Mpango
wa Mradi huu wa kazi Nje - Nje kwa
vijana ambao umepewa jina la Oparesheni Moto wa Nyika, ni sehemu ya kuunga mkono
juhudi za Serikali katika kuwasaidia Vijana kupata ajira au kujiajiri wenyewe
ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu, na kufikia lengo
la maisha bora kwa kila Mtanzania. Hivyo, napenda kuwapongeza kwa kuanzisha
mpango huu katika Mkoa wa Iringa.
Mpango
huu katika Mkoa wa Iringa utawasaidia Vijana namna ya kubuni, kuendeleza na kutekeleza wazo la biashara au
ujasiriamali kwa kujua jinsi ya kutayarisha
mpango na namna ya kupata huduma toka
katika taasisi za fedha.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Sote
tunatambua kwamba, vijana wengi mijini na vijijini wamekuwa hawajitumi na hawana
ajira ya kueleweka, hii imesababisha vijana wengi kujiingiza katika uhalifu,madawa
ya kulevya,kukaa tu kwa muda wote bila ya kujishughulisha na kusababisha kuzorota kwa maendeleo.
Pia,
wimbi kubwa la Vijana wanakimbilia Mijini kutoka vijijini wakiamini kwamba
mijini kunakazi na maisha mazuri. Ni ukweli usiopingika vijana hawa wakifika mijini
huhangaika na kurandaranda mitaani.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Vijana
hawa wakipata elimu ya kutosha hususani elimu ya ujasiliamali, watakuwa
wazalishaji wakubwa katika maeneo ya mijini/vijijini na watajikwamua katika
hali ya umaskini na Taifa letu litasonga mbele. Naamini, kupitia mpango huu
tutapunguza wimbi la wahalifu na wazururaji na pia tutapunguza Vijana
wanaokimbilia Mijini kutafuta kazi.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Napenda
kuwaambia vijana kuitumia vizuri sana fursa hii ambayo ni adimu; wajitokeze kwa
wingi kushiriki katika mpango huu wa kuwainua kimaisha. Wewe kijana unayenisikia
mwambie na mwenzio habari hii njema ili vijana wote Mkoani Iringa muweze kujikomboa
kwa kupitia mpango huu. Nchi yetu ya Tanzania tunawataka vijana wote kufanya
kazi kwa bidii, hususani kazi za uzalishaji. Tunawahamasisha vijana kujiunga
katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji kama Kilimo. Ufugaji,Ufugaji Nyuki,
Samaki, Uanzishaji wa Viwanda Vidogo Vidogo vya usindikaji n.k. Kupitia Vikundi
hivyo, Vijana watakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na
hatimae kufanikiwa kimaisha.
Vijana
wakijiunga katika vikundi vya uzalishaji ni rahisi kukopeshwa mitaji ambayo
itawasaidia kusonga mbele. Mfano wa mitaji hiyo ni mikopo ya fedha kutoka
kwenye Taasisi za Kifedha (benki na SACCOS) na Taasisi nyingine nyingi au Mikopo
ya Matrekta kupitia Mpango wa Kilimo Kwanza (SUMA J.K.T.), n.k.
Nawasihi
PROMISE kuwa mpango huu usambae Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na kuweza
kuwafikia vijana wengi.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Kwa
nafasi hii pia naomba Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, taasisi mbali mbali zikiwemo
za Vyuo Vikuu na Mashirika ya Dini katika Mkoa wa Iringa kuiga mfano huu wa kusaidia
na kuinua maendeleo ya vijana, kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa lolote
duniani hivyo tunapaswa kuwaelekeza na kuwawezesha.
Ndugu
Washiriki, Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana,
Kabla
ya kuzindua mpango huu rasmi, niwaase Vijana wa Mkoa wa Iringa mjitokeze kwa
wingi na kuwa karibu sana PROMISE ili kujua utaratibu kamili kuhusiana na
mafunzo haya ambayo yanatolewa bure kwa vijana wote.
Pia
nawasihi Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni vyema kubuni mikakati mizuri ya kuisaidia
jamii kwa kushirikiana na Serikali.nawashukuru wale wote, wanaoendelea na jamii
katika maendeleo yao.
Kipekee,
nawashukuru na kuwapongeza PROMISE na ILO kwa kuandaa mpango huu, na kuwaomba
waendelee kusaidia vijana kama walivyokusudia. Mara tu mtakapowafundisha na
kuwaelekeza Vijana naomba pamoja na Halmashauri husika kufanya tahmini kubaini
waliofanikiwa na mpango huu.
Ndugu
Washiriki, Mwisho,
Baada
ya kusema haya yote, napenda nitamuake rasmi kuwa mpango huu wa Kazi Nje -
Nje kwa vijana wa Mkoa wa Iringa.
UMEZINDULIWA RASMI.
Asanteni
kwa kunisikiliza.
MKOA WAHIMIZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MAJI
Mkoa
wa Iringa umedhamilia kuhakikisha kilimo kinainuka na kukua zaidi kwa
kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo kwa lengo la kumletea maendeleo
mwananchi kupitia sekta ya kilimo.
Rai
hiyo imetolewa na Mhandisi wa Kilimo, Victor Byanjweli wakati akifafanua
mipango ya Mkoa katika kukuza kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa katika
mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ifunda kilichopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa.
Mhandisi
Byanjweli amesema kuwa kilimo ni sekta kubwa inayoajiri idadi kubwa ya wananchi
katika mkoa wa Iringa, kwa msingi huo uongozi wa mkoa umedhamilia kuhakikisha
kilimo kinasonga mbele na kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wake. Amesema
katika kuhakikisha hilo, Mkoa unaendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za
kilimo kwa lengo la kumletea maendeleo mwananchi. Amezitaja zana hizo kuwa ni
pamoja na matrekta makubwa na madogo na kilimo cha kutumia wanyama kazi.
Mhandisi
Byanjweli ambaye pia amebobea katika umwagiliaji na zana za kilimo amesema kuwa
mkakati mwingine wa Mkoa ni kuhakikisha kilimo kinakua kupitia kilimo cha
umwagiliaji. Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na tabia za
kibinadamu za ukataji miti ovyo, sehemu kubwa ya Mkoa wa Iringa imekuwa ikipata
ukame mkubwa kutokana na upungufu wa mvua usio wa kawaida, Mkoa unahimiza
kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na changamoto ya upungufu wa chakula.
Mhandisi Byanjweli amesema kuwa kupitia kilimo cha umwagiliaji Mkoa utakuwa na uhakika wa chakula na kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha njaa.
Wakati
huohuo, Afisa Elimu Mkuu, Mwl. Euzebio Mtavangu ametoa wito kwa ubia baina ya
walimu na wazazi katika kuhakikisha mwanafunzi anahudumiwa na kulelewa vizuri
ili aweze kufanya vizuri katika masomo yao. Amesema miongoni mwa ubai huo ni
kuhakikisha kuwa wazazi wanawapokea vizuri walimu wanaopangiwa katika maeneo
yao jambo litakalowafanya walimu hao nao kujiona ni miongoni mwa wanajamii na
wazazi wa wanafunzi wao. Amesema kufanya hivyo si tu kunamchango kwa mwalimu
kujisikia yupo nyumbani na mikononi mwa watu wanaomjali lakini pia kwa utoaji
mzuri wa elimu kwa wanafunzi.
Aidha,
amewataka wazazi kuhakikisha wanajipanga na kuwapatia wanafunzi chakula cha
mchana. Akielezea umuhimu wa chakula cha mchana kwa wanafunzi, Afisa Elimu Mkuu
amesema kuwa wanafunzi wanapokula chakula cha mchana kunawasaidia kurudi katika
hali ya kawaida na kuondokana na njaa na uchovu jambo linalowafanya wasome kwa
bidii na maarifa. Amesema kuwa mwanafunzi anapokuwa ameshiba hata uwezo wa
kufikiri na kufaulu unaongezeka sambamba na kupunguza utoro usio wa lazima.
Akihitinisha
mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma amewataka
wananchi wa kijiji cha Ifunda kuhakikisha wanaunda vikundi kwa ajili ya
shughuli za kiuchumi na kuimarisha vyama vya kuweka na kukopa Saccos kwa
manufaa yao. Amesema kuwa Serikali muda si mrefu pembejeo zitapitishiwa katika
Saccos imara hivyo wananchi watakao mufaika ni wale watakao kuwa wamejiunga
katika saccos hizo. Amesema kuwa mkoa wake unahamasisha uundaji wa vikundi vya
vijana na vikundi vya kiuchumi kwa malengo ya kuwafanya wananchi wawe na
vikundi vya kuzalisha mali kwa kuunganisha nguvu pamoja. Amesema kuwa umoja ni
nguvu hivyo watu wakiwa pamoja ni tofauti na anavyokuwa mtu mmoja mmoja.
=30=
Tuesday, December 11, 2012

MAFUNZO HAMASA YA KIBIASHARA
NA
UIMARISHAJI WA
BIASHARA NDOGO
Walengwa: Vijana waliomaliza
vyuo/shule; Mtu yoyote anayependa
kujiajiri; Mfanyabishara anayemiliki
biashara ndogo.
|
Aina ya Bidhaa
|
Idadi ya siku
|
Ada
|
|
Usindikaji chakula: Tomato
sauce, Chilli sauce, Jam, Mbilimbi, Mangle pickle, Cakes/Snacks, Juice,
Peanut butter, unga wa lishe
|
Siku 12
|
150,000/-
|
|
Sabuni za unga, vipande
na maji [za harufu tofauti]
|
Siku 10
|
130,000
|
|
Utengenezaji wa Batiki
|
Siku 12
|
120,000
|
|
Utengenezaji wa ‘Tie and dye’
|
Siku 6
|
80,000
|
|
Kutengeneza mishumaa ya aina na harufu mbalimbali
|
Siku 6
|
75,000
|
|
Ufugaji kuku wa kienyeji , mayai na wa nyama kibiashara
|
Siku 5
|
70,000
|
|
Bidhaa za mikono [urembo aina
tofauti]
|
Siku 10
|
100,000
|
Wasiliana
nasi simu Na. 0754 787 133 NA 0754 072 869
Subscribe to:
Posts (Atom)