Thursday, October 10, 2013

SIKU YA KWANZA YA MBIO ZA MWENGE MKOANI IRINGA



Mwenge wa Uhuru unatarajia kuweka mawe ya msingi, kukagua, kuzindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 33 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4 mkoani Iringa.



               Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma
 
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa alipokuwa akitoa taarifa ya mkoa wa Iringa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha IIgomaa wilayani Mufindi uliotokea mkoani Mbeya leo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma amesema “Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri nne za mkoa wa Iringa ambazo ni Mufindi, Iringa, Kilolo na Manispaa ya Iringa tadi tarehe 14 Oktoba, 2013 ambapo mkoa wa Iringa utahitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa”. 

Dk.  Christine amesema “Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Iringa utaweka mawe ya msingi, utakagua, utazindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 33 yote ikiwa na thamani ya shilingi 4,721,017,330”. Amesema kuwa akti ya fedha hizo michango ya wananchi ni shilingi 576,317,400, Serikali kuu shilingi 1,251,479,577, Halmashauri 179,470,900 na wadau wa maendeleo 2,713,749,453.

Akiongelea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2013, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameutaja kuwa ni “Watanzania ni Wamoja” chini ya kaulimbiu “tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zenu za dini, itikadi, rangi na rasilimali”.  Amesema kuwa ujumbe huo ni muhimu sana kwa Taifa la Tanzania hasa katika kipindi hiki ambapo watanzania wanatakiwa kushikamana zaidi na kuwa wamoja kuelekea katika mchakato wa kupata Katiba mpya ambayo itakuwa dira ya kuliongoza Taifa. 

Akitoa salamu za kuwaaga wananchi wa mkoa wa Mbeya, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Juma Ali Simai amekemea vikali wale wote wenye tabia ya kuubeza na kuusemea vibaya Mwenge wa Uhuru kuwa si wazalendo hata kidogo na hawajui msingi wa Uhuru wa Tanzania. Amesema kuwa chimbuko la Mwnge wa Uhuru na Tanzania ni pale Mwalimu Julius Nyerere alipotoa azimio mwaka 1959 wakati akihutubia Bunge la kikoloni na kusema “sisi (watanganyika) tunataka kuwasha Mwenge  na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”. 

Akiongea kwa ukali, Simai amesema kuwa Mwenge ni alama ya Taifa hivyo wale wote wanaopotosha wananchi juu ya Mwenge na kudhohofisha jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo kupitia falsafa ya Mwenge wa Uhuru wachukuliwe hatua. Amewataka watu na viongozi wa aina hiyo  kujadili amendeleo na wasiotaka watafute Jamhuri yao.



Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma (kulia) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.



=30=

Wednesday, October 9, 2013

PICHA ZA MATUKIO YA SIKU YA UZINDUZI WA WIKI YA VIJANA KITAIFA MKOANI IRINGA

                                                   Moja ya Ubunifu wa Kijana

                            Burudani mbal;imbali ziliweza kusuuza nyoyo za wananchi

                                                   Burudani ni jadi ya Vijana

                                                                 Toyota ubunifu wetu

                             Viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo

                   Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akisalimia wananchi

                          Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akiongea na wananchi

                            Mkuu wa Wilaya yaKilolo, G. Guninita akisalimia wananchi


                                 G. Guninita Mkuu wa Wilaya ya Kilolo

                      Viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo

                                                Mpemba asilia akiwa kazini

                                                        Mpemba asilia akiwa kazini

                   Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akiwatambulisha wageni

                                  Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi

                  Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akisoma salamu za Mkoa

                   Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Uchumi,  Alhaji Adam M. Swai akifuatilia jambo


                           Viongozi wa Serikali wafuatilia kwa umakini mambo yanavyokwenda

                      Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akisoma salamu za Mkoa

 NW wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala (Mb.) akijiandaa kuhutubia wananchi

                NW wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala (Mb.) akihutubia wananchi

            NW wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala (Mb.) akihutubia wananchi

              NW wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala (Mb.) akihutubia wananchi

                            Viongozi wa Serikali wafuatilia kwa umakini mambo yanavyokwenda

                       Viongozi wa Serikali wafuatilia kwa umakini mambo yanavyokwenda

                     Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma akisalimia wananchi

                  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma akisalimia wananchi

           NW wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akizindua Wiki ya Vijana kitaifa mkoani Iringa

                                                        Ndani ya mabanda

                                                      Ndani ya mabanda

                                                             Ndani ya mabanda


                                                                   Ndani ya mabanda

                                                                    Ndani ya mabanda

                                                     Ndani ya mabanda

                                                        Ndani ya mabanda

                                                  Ndani ya mabanda

                                                      Ndani ya mabanda

                                                          Ndani ya mabanda

                                                                   Ndani ya mabanda

                                                             Ndani ya mabanda

                                                               Ndani ya mabanda


                                                                Ndani ya mabanda




FIKRA ZA MWL NYERERE ZIAMASISHE VIJANA KUJILETEA MAENDELEO



Maadhimisho ya wiki ya vijana yanalenga kuendeleza fikra za Mwalimu Julius Nyerere za kuhamasisha amani na usawa katika jamii ili wananchi wajiletee maendeleo yao.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, akitoa maelezo mafupi kuhusu wiki ya vijana kitaifa mkoani Iringa, yaliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya vijana-Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege.

Sihaba amesema kuwa serikali iliamua kuziunganisha shughuli za vijana na madhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999. Amesema “maamuzi ya Serikali yalizingatia haja ya  kuendelea kuenzi  fikra za Baba wa Taifa za kuutumia Mwenge wa Uhuru kama chombo maalum cha kuhamasisha amani na umoja, kuondoa dhuluma, kukuza moyo wa kujitolea hasa kwa Vijana, na kuleta maendeleo ya watu katika nchi yetu na nje ya mipaka yetu”.

Akiongelea fursa watakazopata vijana katika wiki hiyo ya maonesho, Katibu Mkuu amesema kuwa vijana watapata fursa ya kukutana, kuonyesha shughuli wanazozifanya na kutathimini mchango wao katika kulijenga Taifa la Tanzania. Amesema kuwa vijana wataweza kutumia wiki hiyo kutengeneza mitandao na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali yanayohusu maisha yao ya kila siku.

Akielezea shughuli za wiki ya vijana kitaifa, Sihaba amesema kuwa shughuli hizo zimegawanyika katika sehemu tatu. Amezitaja sehemu hizo kuwa ni maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana ambayo yatakuwa kwenye mabanda maalum. Shughuli nyingine ni midahalo ya vijana, ambapo vijana watapata fursa ya kujadili na kujifunza mambo mengi kupitia mada mbalimbali. 

Mada hizo ni Ujue Mkoa wa Iringa, Maudhui ya Wiki ya Vijana, Fursa za ajira kwa Vijana, Ushiriki na ushirikishwaji wa Vijana katika maendeleo, Huduma ya hifadhi ya Jamii kwa Vijana na Wajibu wa Vijana katika kutunza amani ya nchi. Shughuli ya mwisho ni huduma ya kupima virusi vya ukimwi kwa hiyari itakayotolewa bure.

Washiriki wa maonesho hayo ni vijana kutoka mikoa yote ya Tanznia Bara na Visiwani kupitia kwenye vikundi vyao vya uzalishaji mali, makampuni na taasisi za vijana, mashirika na idara za Serikali pamoja wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana hapa nchini.
=30=


RC ASISITIZA AMANI NA UMOJA WA KITAIFA



Wananchi wametakiwa kudumisha amani na umoja wa kitaifa kwa kuenzi juhudi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alizoziweka wakati wa kuweka misingi ya Taifa kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na wiki ya vijana kitaifa mkoani Iringa. 

Dk. Christine amesema kuwa wananchi wanawajibu wa kuhakikisha amani na umoja wa kitaifa vinadumu na kuwa endelevu nchini. Amesema kudumisha amani na utulivu ni njia mojawapo ya kuenzi misingi na kazi alizofanya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa Taifa la Tanzania. Amesema “sehemu yoyote yenye amani na utulivu, yapo maendeleo kwa sababu wananchi wanafanya shughuli za maendeleo kwa uhuru, hii ndiyo maana yam bio za Mwenge wa Uhuru” alisisitiza Dk. Christine.

Akiongelea ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2013, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013, zimebeba ujumbe usemao: “watanzania ni wamoja” wenye kaulimbiu “tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali”. 

Amesema lengo la ujumbe huo ni kutoa msisitizo kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuimarisha umoja na amani nchini. Amesema kuwa ni ushahidi kwa nchi jirani unaonesha madhara ya kuichezea amani na kuongeza kuwa ni rahisi sana kupoteza amani na umoja lakini ni vigumu sana kuirejesha. Amesema kutokana na umuhimu huo, Serikali imeona ni vizuri kutumia mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013 kuhimiza umoja wa kitaifa. 

Akiongelea wiki ya vijana kitaifa iliyoanza tarehe 08/10/2013, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa maonesho hayo yameandaliwa vizuri ili yaweze kuwa na mvuto muda wote. Amesema kuwa vijana kutoka nchi nzima wanashiriki katika maonesho hayo na kutoa rai kwa vijana wote kutumia maonesho hayo kujifunza shughuli wanazofanya za kujiletea kipato. 
   
Ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kutembelea mabanda ya maonesho katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege kuanzia ufunguzi hadi kilele tarehe 14/10/2013.

Amesema kuwa sambamba na maonesho hayo kutakuwa na midahalo ya vijana itakayofanyika kuanzia tarehe 9/10/2013-13/10/2013 katika ukumbi wa chuo cha VETA itakayohusisha vijana zaidi ya 300 kila siku. Amesema kuwa midahalo hiyo itarushwa na vyombo vya habari na kuwataka vijana kushiriki kikamilifu katika midahalo hiyo.
  =30=