Tuesday, January 7, 2014
SERIKALI IONGEZE SHULE ZA VIPAJI MAALUM
Serikali
imeshauriwa kuandaa mkakati wa kitaifa wa kuongeza idadi ya shule za sekondari
za bweni na vipaji maalum kutokana na idad ya wanafunzi kufaulu na kupanda kila
mwaka ili kuwatendea haki na kulinda vipaji vya watoto.
Ushauri huo
umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bibi. Evarista Kalalu wakati akichangia
katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza kwa
mkoa wa Iringa kilchofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
Bibi. Kalalu
amesema ufaulu wa wanafunzi unapanda na kuongezeka lakini sekondari za bweni na
vipaji maalum haziongezeki jambo linalosababisha kutokuwatendea haki wanafunzi
wengi waliofaulu vizuri kukosa nafasi katika shule hizo. Ameshauri kuwa uwepo
mkakati wa kitaifa wa kuongeza shule za bweni na vipaji maalum ili kuwapatia
fursa watoto wengi zaidi.
Wakati huohuo,
Mbunge wa Mufindi Kusini, Bw. Menrad Kigola ameshauli viwepo vyuo vikuu vya
vipaji maalum nchini ili kulinda vipaji vya wanafunzi wanaomaliza shule za
sekondari. “Tunazo shule za sekondari za vipaji maalum chakushangaza watoto
wetu wanapomaliza sekondari wanajiunga na vyuo vikuu vya kawaida jambo
linalochangia kupoteza vipaji vya watoto wetu. Umefika wakati wa serikali kuwa
na vyuo vikuu vya vipaji maalum ili kulnda na kuendeleza vipaji vya watoto
wetu” amesisitiza Bw. Kigola.
Akifunga kikao
hicho, Mwenyekiti wa kikao hicho ambae pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Iringa, Bibi. Wamoja Ayubu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha
wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti na kuanza masomo shule
zitakapofunguliwa. Aidha, amewataka kuhakikisha vikao vya tathmini ya elimu na
kuzipongeza shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
mwaka 2013.
Bibi. Ayubu
amewata kuweka mikakati endelevu ili mwaka 2014 Mkoa wa Iringa ufikie asilimia
70 ambalo ni lengo la Matokeo Makubwa Sasa kwa mwaka huo. Vilevile, amewataka
kuhakikisha Kata ambazo zimechukua wanafunzi wengi zaidi kuliko uwezo wa vyumba
vya madarasa vilivyopo, kuhakikisha madarasa yanajengwa haraka ili kukidhi
idadi ya wanafunzi stahili. Katika kuendeleza ubora wa elimu mkoani, Kaimu
Katibu Tawala Mkoa amewataka wakurugenzi kuhakikisha usimamizi na ufuatiliaji
unakuwa wa karibu zaidi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara shuleni ili kuondoa
tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
=30=
HALMASHAURI ZA MKOA WA IRINGA ZAPONGEZWA KUVULA MALENGO YA BRN
Halmashauri za
Mkoa wa Iringa zimepongezwa kwa kazi nzuri katika sekta ya elimu hadi
kufanikisha kuvuka lengo la Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kuuwezesha Mkoa
kushika nafasi ya tatu kitaifa katika Mtihani wa darasa la saba kitaifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wanafunzi wa kujunga na kidato
cha kwanza Mkoa wa Iringa, Bibi. Wamoja Ayubu katika hotuba yake ya ufunguzi wa
kikao cha Kamati ya Uchaguzi wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
2013 Mkoa wa Iringa kilchofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini
Iringa.
Bibi. Ayubu
amesema “kiwango cha ufaulu ni kizuri sana na Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya
tatu kati ya mikoa 25 ya Tanzania bara. Pia kiwango cha ufaulu kimepanda kwa
Halmashauri zote. Kwa hiyo, nachukua nasafi hii kuzipongeza Halamshauri zote
kwa kuvuka lengo la matokeo makubwa sasa ambalo ni asilimia 60 kwa mwaka 2013”.
Akiwasilisha
taarifa ya mwelekeo wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka
2013 Mkoa wa Irnga, Afsa Elimu Mkoa wa Iringa, Mwalimu Joseph Mnyikambi amesema
kuwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika tarehe 11-12 Septemba,
2013. Amesema kuwa shule za msingi 449 kati ya shule 482 ndizo likukuwa na
watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Akiongelea
mahudhurio siku za mitihani, Mwalimu Mnyikambi amesema kuwa mahudhurio
yameongezeka kutoka asilimia 98.3 ya mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 99 mwaka
2013 likiwa ni ongezeko la asilimia 0.7. Amesema kuwa kiwango cha kumaliza
elimu ya msingi kimeongezeka kutoka asilimia 82 (2012) hadi kufikia asilimia 84
(2013) likiwa ni ongezeko la asilimia 2. Aidha, wanafunzi ambao hawakufanya
mtihani mwaka 2013 ni asilimia 1 ukilinganisha na asilimia 1.2 mwaka 2012
kutokana na sababu za utoro, vifo, ugonjwa na mimba.
Akiongelea hali
ya ufaulu kwa kila Halmashauri katika Mkoa wa Iringa, Afisa Elimu Mkoa amesema
kuwa Iringa Manispaa asilimia 81.9 (1), Mufindi asilimia 63.9 (2), Iringa
asilimia 62.2 (3) na Kilolo asilimia 60.3 (4).
Amezitaja shule
10 bora katika Mkoa wa Iringa kuwa ni Sipto (1), Ummu Salaama (2), Ukombozi
(3), St. Dominic Savio (4), Star (5),
Wilolesi (6), St. Charles (7) zote za Manispaa ya Iringa. Nyingine ni Brooke
Bond (8), Southern Highland (9) Mufindi na Mapinduzi (10) Manispaa ya Iringa.
=30=
Friday, January 3, 2014

OFISI
YA WAZIRI MKUU
RATIBA
YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA
DKT.
WILLIAM A. MGIMWA
|
TAREHE
|
SIKU
|
MUDA
|
TUKIO
|
WAHUSIKA
|
|
4.1.2014
|
JUMAMOSI
|
7.00 MCHANA
|
MWILI WA MAREHEMU KUWASILI UWANJA WA
NDEGE WA MWALIMU NYERERE – TERMINAL II NA KUPELEKWA NYUMBANI MIKOCHENI B
|
NDUGU
VIONGOZI
WANANCHI
KAMATI
|
|
11.00 JIONI
|
MWILI KUPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO
|
KAMATI
|
||
|
5.1.2014
|
JUMAPILI
|
3.00 – 4.00 ASUBUHI
|
CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU
|
KAMATI
|
|
4.30 ASUBUHI
|
MWILI KUWASILI NYUMBANI
|
KAMATI
|
||
|
5.30 – 8.00 MCHANA
|
MWILI KUPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE,
KWA AJILI YA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO
|
KAMATI
|
||
|
8.00 MCHANA
|
MWILI KUPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA
MWALIMU NYERERE – TERMINAL 1
|
KAMATI YA KI - TAIFA
|
||
|
10.00 JIONI
|
MWILI KUWASILI IRINGA
(NDULI AIRPORT)
NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO - IRINGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
||
|
11.30 JIONI
|
KUELEKEA KIJIJINI MAGUNGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
||
|
6.1.2014
|
JUMATATU
|
6.00 MCHANA
|
SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA
MAREHEMU MAGUNGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
TANZIA
TANZIA
WAKUU
WA IDARA/VITENGO
WATUMISHI
WOTE
WIZARA
YA FEDHA
TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA
WAZIRI WA FEDHA MHE. DKT. WILLIAM A.
MGIMWA (MB) KILICHOTOKEA TAREHE 01 JANUARI, 2014 HUKO AFRIKA KUSINI, KATIKA
HOSPITALI YA KLOOF MEDI – CLINIC, PRETORIA. MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI SIKU YA
JUMAMOSI TAREHE 04/01/2014 NA
UTASAFIRISHWA KWENDA MKOANI IRINGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 05/01/2014 KWA MAZISHI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
2
JANUARI, 2014
Sunday, December 29, 2013
IRINGA YAVUKA LENGO LA BRN KATIKA ELIMU
Mkoa wa Iringa
imevuka lengo la matokeo makubwa sasa (BRN) kwa zaidi ya asilimia 60 kwa
kiwango cha ufaulu kwa mtokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2013 ukishika
nafasi ya tatu kitaifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga
kidato cha kwanza mkoa wa Iringa mwaka 2014, Wamoja Ayubu katika hotuba yake ya
ufunguzi wa kikao cha kamati ya uchaguzi mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa
ni Kilimo mjini Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wamoja Ayubu (kulia) akifungua kikao (kushoto) ni Afisa Elimu Mkoa wa Iringa Mwalimu Joseph Mnyikambi
Wamoja amesema
“kiwango cha ufaulu ni kizuri sana na mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya tatu
kati ya mikoa 25 ya Tanzania bara. Pia kiwango cha ufaulu kimepanda kwa
Halmashauri zote. Kwa hiyo, nachukua nafasi hii kuzipongeza Halmashauri zote
kwa kuvuka lengo la matokeo makubwa sasa ambalo ni asilimia 60 kwa mwaka 2013”.
Amesema kuwa mwaka 2013 mkoa wa Iringa ulikuwa na watahiniwa 23,148
waliosajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wavulana 10,752 na wasichana 12,396.
Amesema miongoni mwao watahiniwa 22,922 wavulana wakiwa 10,630 na wasichana
12,292 sawa na asilimia 99 walifanya mtihani.
Akiongelea
ufaulu, Wamoja ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amesema kuwa
watahiniwa 14,956 (wavulana 7,042 na wasichana 7,914) ndio waliofaulu kwa
kupata alama kati ya 100-250 sawa na asilimia 65.25. Aidha, amekieleza kikao
hicho kuwa ni wakati muafaka kuweka mikakati ya kuongeza ufaulu zaidi hadi
kufikia asilimia 70 ambalo ni lengo la matokeo makubwa sasa kwa mwaka 2014.
Akiwasilisha
taarifa ya mwelekeo wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka
2013 mkoa wa Iringa, Afisa elimu mkoa wa Iringa, Mwalimu Joseph Mnyikambi amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza elimu
ya msingi uliofanyika tarehe 11-12 Septemba, 2013 shule za msingi 449 kati ya
shule 482 ndizo zilizokuwa na watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi.
Mwalimu Mnyikambi
amesema kuwa mahudhurio katika siku za mitihani yameongezeka kutoka asilimia 98.3
mwaka 2012 hadi asilimia 99 mwaka 2013 likiwa ni ongezeko la asilimia 0.7 . Amesema
kuwa kiwango cha kumaliza elimu ya msingi kimeongezeka kutoka asilimia 82 (2012)
hadi asilimia 84 (2013) ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 2.
Afisa Elimu Mkoa
wa Iringa amezitaja shule 10 bora za serikali na binafsi kimkoa kutoka kila
Halmashauri kwenye mabano kuwa ni:- Sipto, Ummusalaama, Ukombozi, St. Dominic
Savio, Star, Wilolesi, St. Charles (zote za Manispaa ya Iringa) nyingine ni
Brooke Bondi na Southern Highland (Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi) na
Mapinduzi (Manispaa ya Iringa).
Akiongelea
mwongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014,
Mwalimu Mnyikambi amesema kuwa nafasi zilizotengwa kwa shule za vipaji maalum
kwa mkoa wa Iringa ni Mzumbe (6), Kibaha (7) kwa wavulana na Kilakala (8) na
Msalato (5) kwa wasichana. Nafasi za shule za bweni zilizotengwa kwa mkoa wa
Iringa ni Malangali (12) na Songea (9) kwa wavulana na Sekondari ya wasichana
ya Iringa (9) na Mgugu (8) wasichana. Shule za ufundi ni Ifunda (15), Iyunga
(10) wavulana na Tanga (2) wasichana.
=30=
Subscribe to:
Posts (Atom)