Wednesday, September 13, 2017

UTALII KARIBU KUSINI KUFANIKISHWA NA KAMATI NDOGO

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Kamati ya maandalizi ya Utalii Karibu Kusini imeunda kamati ndogo za ufuatiliaji na usimamizi wa kufanikisha maadhimisho ya siku ya Utalii Karibu Kusini na maonesho ya shughuli za viwanda vidogo kanda ya nyanda za juu kusini.

Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Fikira Kisimba alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Utalii Karibu Kusini na maonesho ya shughuli za viwanda vidogo kanda ya nyanda za juu kunisi kwa viongozi wakuu wa mikoa nyanda za juu kusini walipotembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha na kufanya kikao cha pamoja katika hifadhi hiyo iliyopo nje kidogo ya mji wa Iringa.

Kisimba alisema kuwa katika kufanikisha maonesho hayo, kamati ya maandalizi imefanya shughuli mbalimbali pamoja na kuunda kamati ndogondogo. Kamati zilizoundwa alizitaja kuwa ni kamati ya Mipango na Fedha; Kamati ya Mapokezi, Usafiri na Malazi; Kamati ya Chakula, Afya na usafi wa Mazingira. 

Nyingine ni Kamati ya Miundombinu na Mapambo; Kamati ya Ulinzi na Usalama; Habari na Uenezi na Kongamano na Maonesho ya nje. Kisimba aliongeza kuwa kamati hizo saba zimeundwa kwa kushirikisha sekta binafsi na sekta ya umma ili kutoa uwiano sawia.

Akiongelea uhamasishaji wa jamii na mialiko, mwenyekiti huyo wa maandalizi alisema kuwa uhamasishaji unaendelea kufanyika kwa wadau mbalimbali. Alisema kuwa ofisi za SIDO katika mikoa ya nyanda za juu kusini imekwisha wataarifu wajasiriamali waliopo katika mikoa yao. Wadau wakubwa 51 wameandikiwa barua za kuomba michango na ushiriki. 

“Taarifa ya mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati wa Maonesho ya Nane Nane - Mbeya kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya na Katibu Tawala Mkoa; Vikao mbalimbali vya Maandalizi na vikao vingine vya wadau vinavyofanyika  na kushirikisha vyombo vya Habari” alisema Kisimba.

Wakuu wa mikoa ya nyanda za juu kusini walioshiri ziara hiyo ni Amina Masenza mkuu wa Mkoa wa Iringa, Luteni (Mst) Chiku Galawa Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Christopher Ole Sendeka mkuu wa mkoa wa Njombe.

Maonesho ya Utalii yatafanyika pamoja na Maonesho shughuli za Viwanda Vidogo (SIDO) kanda ya nyanda za juu kusini kwa Mwaka 2017.  Maonesho haya yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 29/09/2017 hadi tarehe 02/10/2017.
=30=

HIFADHI YA RUAHA YAATHIRIWA NA KUKAUKA KWA MTO RUAHA MKUU

Na. Mwandishi Maalum, Iringa
Hifadhi ya taifa ya Ruaha inaathiriwa na changamoto ya kukauka kwa mto Ruaha mkuu jambo linalohatarisha maisha ya wanyama na uendelevu wa hifadhi hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na kaimu mkuu wa hifadhi ya Ruaha, Halima Kiwango alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa wakuu wa mikoa ya nyanda za juu kusini waliotembelea hifadhi hiyo na kufanya kikao cha pamoja cha maandalizi ya Utalii Karibu Kusini hifadhini hapo.

Kiwango alisema kuwa changamoto kwa uhifadhi ni kukauka kwa mto Ruaha mkuu jambo linalohatarisha uhai wa wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Akiongelea sababu za kukauka kwa mto Ruaha mkuu, Kiwango alizitaja kuwa ni kilimo cha umwagiliaji mashamba makubwa na madogo ya mpunga katika bonde la mto Ruaha mkuu. Sababu nyingine alizitaja kuwa ni ongezeko la mifugo katika bonde la Usangu na watumia maji katika bonde hilo. Nyingine ni uvamizi wa wanyamapori katika maeneo ya nje ya hifadhi na ujangili wa Tembo.
Mhifadhi Halima Kiwango

Kaimu mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha alizitaja changamoto nyingine kuwa ni barabara kuu kutoka Iringa hadi lango kuu la kuingia hifadhi ya Ruaha kutokuwa ya kiwango cha lami inachangia idadi ndogo ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo. 

“Kutokuwa na lango la kuingilia hifadhini upande wa Usangu kumekuwa kukisababisha watalii wengi kutokufika katika hifadhi ya Ruaha. Changamoto nyingine ni hifadhi bado haijajulikana sana kwa watalii wa nje na ndani” alisema Kiwango.

Thursday, August 31, 2017

UTALII KARIBU KUSINI NA SIDO KULETA WANYAMAPORI HAI IRINGA

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Kamati ya maandalizi ya maonesho ya utalii ya karibu kusini na shughuli za viwanda vidogo (SIDO) kanda ya nyanda za juu kusini imetakiwa kuhakikisha wanyamapori hai wanakuwepo katika maonesho hayo.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiendesha kikao cha tatu cha maandalizi ya maonesho ya Utalii Karibu Kusini na shughuli za viwanda vidogo (SIDO) kanda ya nyanda z juu kusini kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Veta mjini Iringa.

Masenza alisema kuwa wanyamapori hai ni muhimu katika maonesho hayo kwa sababu wananchi wengi wanapenda kuwaona wanyamapori hai moja kwa moja. Aidha, alishauri kasi ya kufuatilia wanyamapori hao inayofanywa baina ya kamati ya maandalizi na wizara ya Maliasili na Utalii iongezwe.

Katika taarifa ya kamati ya maandalizi iliyowasilishwa na Fikira Kisimba alisema kuwa ufuatiliaji unaendelea kufanyika kwa kushirikiana na wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kupata wanyama hao. “Wizara imetoa bajeti elekezi ambapo mikoa inawajibika kuchangia jumla ya shilingi 4,000,000 kukodi mabanda yote manne ya wanyama” alisema Kisimba.

Akiongelea wadau waliothibitisha kushiriki katika maonesho hayo, alisema kuwa wadau 312 wamethibitisha kushiriki. Aliwataja baadhi ya wadau hao kuwa ni wizara ya Maliasili na Utalii; wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezeji; wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; na TATO. Wengine ni KILI FAIR; Wakala wa Misitu Tanzania; Ngonga beach; UPL Link Mbeya; Uyole cultural Enterprises; Baraza la Biashara la Taifa; Heifer International; Care International na Wajasiliamali 300.
=30=

Thursday, January 26, 2017

KILOLO YATAKIWA KUZIDISHA KASI UJENZI WA MADARASA

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Wilaya ya Kilolo imetakiwa kuongeza juhudi katika ujenzi wa madarasa na majengo ya utawala ili wanafunzi waweze kusoma vizuri bila kubanana jambo linaloathiri ufanisi katika masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipofanya ziara ya kukagua wanafunzi walioripoti shuleni na hali ya miundombinu ya elimu wilayani Kilolo jana.

Masenza alisema “kuna shule za msingi madawati hayajakamilika na vyumba vya madarasa pungufu. Hii maana yake maafisa watendaji wa kata na vijiji hawajatimiza wajibu wao”. Afisa utumishi lazima upitie mipango kazi ya maafisa watendaji wa kata na vijiji ili kujiridhisha kama wameweka katika mipango ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa. Aliongeza kuwa zipo baadhi ya shule za msingi zina upungufu wa miundombinu ya vyoo. Aliutaka uongozi wa wilaya kusimamia ukamilishaji wa miundombinu yote ya elimu ili iwe chachu kwa walimu kufundisha vizuri na watoto kusoma zaidi.

Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wana Kilolo kuwa wamoja na kufanya kazi kwa umoja ili kuzitatua changamoto zinazoikabili wilaya hiyo. “Changamoto katika elimu ni nyingi wilayani hapa, umoja wenu ndiyo njia pekee ya kutatua changamoto hizi” alisema Masenza.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya uandikishaji wanafunzi katika shule ya msingi Utengule, mwalimu mkuu Grayson Kwayu alisema kuwa wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza matarajio yalikuwa kuandikisha wanafunzi 76 hadi kufikia tarehe 24/1/2017 jumla la wanafunzi 86 walikuwa wameandikishwa shuleni hapo.

Akiongelea hali ya uandikishaji darasa la awali, mwalimu Kwayu alisema kuwa matarajio yalikuwa kuandikisha watoto 96 kwa darasa la awali, hadi kufikia tarehe 24/1/2017 ni wanafunzi 66 pekee waliokuwa wameandikishwa.

Akiongelea nyumba za walimu, mwalimu mkuu huyo alisema kuwa shule yake inaupungufu wa nyumba za walimu tano. Alisema kuwa mahitaji ya nyumba za walimu ni 14 wakati nyumba zilizopo ni tisa. ”Kamati ya shule kwa kushirikiana na serikali ya kijiji imeandaa mpango kazi kwa ajili ya kujenga maboma matano ya nyumba za walimu kwa kipindi cha mwaka 2017-2020” alisema Kwayu.

Shule ya msingi Utengule ina jumla ya walimu 14, walimu saba wakiwa wa kiume na walimu saba wa kike.
=30=