Wednesday, September 7, 2011

WAZAZI WASHAURIWA KUTOINGILIA NDOA ZA WATOTO WAO
Wazazi wametakiwa kutoingilia NDOA za watoto wao na kushauriwa kuwaacha wastarehe katika NDOA zao kwa sababu kuwaingilia watoto katika ndoa zao ni kinyume na mpango wa MUNGU na ni chanzo cha mafarakano katika NDOA.

Ushauri huo ulitolewa na Baba Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Iringa, Askofu Jonas Mkane katika nenolake lililotangulia ufungishaji wa NDOA TAKATIFU kati ya Samwel S. Nyagawa na Catherine W. Mdemu.
 Samwel S. Nyagawa akimvisha PETE YA NDOA TAKATIFU Catherine W. Mdemu

Askofu Mkane amesema kuwa baadhi ya NDOA zimekuwa zikivunjika kutokana na wazazi kuingilia ndoa za watoto wao na kusisitiza kuwa ni jambo la aibu kwa wazazi hao kuhusika katika kuharibu NDOA za watoto wao.

Amesema kwa kuwa Samwel ameamua kumuoa Catherine, tendo hilo maana yake ni Dunia mzima hakuna tena mwanamke anayeweza kuwa mke wa Samwel na kusisitiza kuwa NDOA ni utawala Mtakatifu.

Askofu Mkane amesema kuwa mwanzilishi wa Taasisi hiyo (NDOA) ni MUNGU mwenyewe pale Bustani ya Eden aliposema “si vema mtu huyu akawa peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufa-nana naye”.
Amesema kazi kubwa na msingi aliyonayo na anayowajibika kwayo Catherine kwa Samwel ni UTII wakati kwa Samwel yeye ni KUMPENDA Catherine na hayo ndiyo maisha ya NDOA.

Akiongelea changamoto katika NDOA amewataka maharusi hao kutotarajia mteremko katika maisha ha ohayo mapya na kusisitiza kwa mujibu wa maandiko yanavyosema “wanaume kaeni na wake zenu kwa akili…”.

Mwisho Baba Askofu amewashauri kuweka pamoja rasilimali zao na kupanga mipango yao ya kimaisha pamoja ili kufikia mafanikio ya pamoja haraka.

Katika muda wote wa ibada hiyo ya NDOA TAKATIFU maharusi hao walionekana wenye utulivu mkubwa mbele za MUNGU huku wakianikizwa na tabasamu na bashasha za haja wakati nyuso zao zikitawaliwa na furaha isiyo kifani na dim-pose zisizojificha. 
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe bab kubwa ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha RUCO.
                                                                                                                       

1 comment:

  1. Kaka Gondwe hapo inakuwa vipi mara bro sam anaidondosha chini hiyo PETE watu weweeeee!

    Mzee wa utata

    ReplyDelete