Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza
amewatakia heri na kupona haraka majeruhi wote wa ajali ya basi ili waweze kuungana
na familia zao na kuendelea na majukumu yao.
Kauli hiyo aliitoa muda mfupi baada
ya kufanya ziara ya kustukiza katika hospitali ya rufaa ya Iringa kujionea
jinsi majeruhi wa ajali ya basi la kampuni ya New Force wanavyohudumiwa
hospitalini hapo.
Masenza akiyeambatana na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Iringa alisema kuwa ajali hiyo imemuhuzunisha yeye
binafsi na mkoa kwa ujumla. Alisema kuwa anawaombea kwa Mungu majeruhi wote
kupata nafuu na kupona kabisa ili waweze kuendelea na majukumu yao ya ujenzi wa
Taifa.
Akiongelea hali ya huduma hospitali
hapo, Masenza alisema kuwa ameridhishwa na jinsi majeruhi wa ajali hiyo
walivyopokelewa na kutibiwa hospitalini hapo. Aidha, aliwataka madaktari na
wauguzi kuendelea kuonesha moyo wa huruma na uwajibikaji wanapowahudumia
majeruhi wa ajali hiyo. Aidha, aliwahakikishia majeruhi hao kuwa serikali ipo
pamoja nao kuhakikisha wanapata huduma bora ili wapone haraka na kuendelea na
majukumu yao.
Ajali hiyo ilitokea kwa basi kugongana
na lori ilitokea tarehe 18 Disemba, 2015 mchana baada ya tairi la lori lori
namba T 616 DES la kampuni ya Ranfad Ltd kupasuka kupasuka na lori kukosa
muelekeo na kuligonga basi la kampuni ya New Force namba T 483 CTF na
kusababisha vifo vya abiria 12 na majeruhi 28. Miongoni mwa majeruhi hao,
watatu ni raia wa Kongo DRC na mmoja raia wa Afrika Kusini.
=30=
No comments:
Post a Comment