Sunday, January 21, 2018

TIMU YA RAS IRINGA WAPOTEANA UWANJANI BAADA YA KICHAPO CHA 5-0 TOKA TANROADS



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  
Timu ya mpira wa miguu ya RAS Iringa imechapwa magoli 5-0 na  wakala wa Barabara (TANROADS) katika mechi ya ufunguzi iliyoshuhudiwa na mamia wa wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.

Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la chuo cha Ualimu Kleruu kilichopo manispaa ya Iringa ilianza kwa kasi ndogo huku kila timu ikosoma mchezo wa mwezake. Hadi kipinci cha kwanza kinaisha timu ya RAS IRINGA ilikuwa nyuma kwa goli Moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kidogo. 
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akisalimiana na Peter Nyakigera
Jitihada za RAS IRINGA kurudisha goli zilionekana wazi kabla ya juhudi hizo kufifishwa baada ya golikipa wao namba moja Mashaka Mwanage kuumia mkono wa kuume na kushindwa kuendelea na mchezo. Pigo hilo kwa RAS IRINGA lilifungulia mvua ya magoli hadi kufikia magoli matano.

Tangu awali TANROADS walionekana kukamia mechi hiyo huku wakiwa na kikundi cha washangiliaji mahili. Muda wote wa mchezo meneja wa TANROADS Mhandisi Daniel Kindole alikuwa akifuatilia kwa makini mechi hiyo.

Baada ya kipeng cha mwisho watumishi wa RAS walionekana kuondoka mmoja mmoja kwa njia yake jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya soka kuwa ni kuvurugwa na kichapo hicho.
=30=

No comments:

Post a Comment