Tuesday, September 19, 2017

MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA IRINGA KULETA MABADILIKO CHANYA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya katika ofisi ya mkuu wa mkoa Iringa yataleta mabadiliko chanya katika utumishi wa umma mkoani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Takwimu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Iringa, Hildegarda Kimaro katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa jana.
Afisa Takwimu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hildegarda Kimaro

Kimaro alisema “mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya ni mazuri, tumejifunza mambo mbalimbali ambayo hatukuyafahamu awali. Mfano sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake na utunzaji wa kumbukumbu”. 

Aliongeza kuwa awali utunzaji kumbukumbu lilifahamika kuwa ni jukumu la watunza kumbukumbu wasaidizi katika ofisi ya mkuu wa mkoa, lakini baada ya mafunzo imebainika kuwa utunzaji kumbukumbu ni jukumu wa watumishi wote wa umma kwa nafasi zao.

Akiongelea umuhimu wa mafunzo hayo elekezi ya awali kwa watumishi wa umma, Kimaro alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutokuvunja sheria za utumishi. “Mafunzo haya ni muhimu na yatatusaidia kutokuvunja sheria ambazo tungevunja bila kufahamu. Kwa mafunzo haya tumeweza kufahamu jambo ambalo ni sahihi kufanya katika utumishi wa umma na ambayo si sahihi kufanya katika utumishi wa umma” alisema Kimaro.     

Kimaro alishauri kuwa watumishi wapya wanapoajiriwa wapewe mafunzo elekezi ya awali angalau ndani ya miezi mitatu ya awali. 

“Katika kuongeza umakini wa mafunzo, ni vizuri mafunzo hayo yakatolewa nje ya eneo la kazi ili kuwawezesha washiriki wa mafunzo kujikita katika mafunzo kuliko kutekeleza majukumu mengine ya kiutumishi jambo linaloathiri utulivu na usikivu wakati wa mafunzo” alishauri Kimaro.

Mafunzo elekezi ya awali ya siku tano kwa watumishi wapya wa umma yameandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na chuo cha utumishi wa umma (TPSC) yakishirikisha watumishi wapya 107 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi za wakuu wa wilaya na hospitali ya rufaa ya mkoa.
=30=





WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA NIDHAMU IRINGA



Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Watumishi wa umma mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu katika kutekeleza majukumu yao wanapowahudumia wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa umma walioajiliwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa, mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa jana.

Ayubu alisema kuwa msingi wa utumishi wa umma umejikita katika uadilifu, hivyo mtumishi wa umma lazima afanye kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Magufuli imejipambanua kwa kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma. Aliwataka watumishi wa umma mkoani Iringa kuwa mfano mzuri wa kuingwa katika nidhamu na uwajibikaji wanapowahudumia wananchi ili wabaki na kumbukumbu ya huduma njema.

Akiongelea umuhimu wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wa umma, Katibu Tawala mkoa alisema kuwa watumishi wengi wanatoka katika maeneo tofauti yenye mitazamo tofauti hivyo, kuitaji kufundishwa utaratibu wa kazi katika serikali. 

“Mafunzo haya ni muhimu sana unapoingia katika utumishi wa umma. Tunatoka katika vyuo tofauti na tamaduni tofauti hivyo, hata tabia zinakuwa tofauti. Mafunzo haya yanalenga kutufundisha namna utumishi wa umma ulivyo na jinsi mtumishi wa umma anavyotakiwa kuonekana na kutenda kazi” alisema Ayubu.

Aliwataka watumishi hao kubadilika baada ya mafunzo kimtazamo na kiutendaji na kuzingatia viwango vya juu katika utumishi wao. 

“Unajua unapoingia katika utumishi wa umma, unajikuta unafanya makosa, ila tunashindwa kukuchukulia hatua za kiutumishi badala yake tunalazimika kukufanyia ushauri zaidi. Tunabadilika na kuwa wazazi na walezi katika kuwaelimisha watumishi” alisema Ayubu. 

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo haya watakuwa wakiwachukulia hatua stahili za kiutumishi watumishi wote watakaotenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Alisema kuwa katika mafunzo hayo watumishi wa umma watafundishwa muundo wa serikali, uendeshaji wa shughuli za serikali, utunzaji wa kumbukumbu, maadili ya utumishi wa umma, maboresho ya utumishi wa umma, huduma kwa mteja, sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake, mpango wa kudhibiti ukimwi kwa watumishi wa umma na upimaji wa wazi utendaji kazi kwa watumishi wa umma.

Mafunzo elekezi ya awali ya siku tano kwa watumishi wapya wa umma yameandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na chuo cha utumishi wa umma (TPSC) yakishirikisha watumishi wapya 107 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi za wakuu wa wilaya na hospitali ya rufaa ya mkoa.
=30=
  

Wednesday, September 13, 2017

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA NIDHAMU IRINGA



Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Watumishi wa umma mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu katika kutekeleza majukumu yao wanapowahudumia wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa umma walioajiliwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa, mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa jana.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akiongea na watumishi wapya, kulia ni Katibu Tawala Msaidi Utawala, Lucas Kambelenje (kulia) kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dr Robert Salim

Ayubu alisema kuwa msingi wa utumishi wa umma umejikita katika uadilifu, hivyo mtumishi wa umma lazima afanye kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Magufuli imejipambanua kwa kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma. 

Aliwataka watumishi wa umma mkoani Iringa kuwa mfano mzuri wa kuingwa katika nidhamu na uwajibikaji wanapowahudumia wananchi ili wabaki na kumbukumbu ya huduma njema.

Akiongelea umuhimu wa mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wa umma, Katibu Tawala mkoa alisema kuwa watumishi wengi wanatoka katika maeneo tofauti yenye mitazamo tofauti hivyo, kuitaji kufundishwa utaratibu wa kazi katika serikali. 

“Mafunzo haya ni muhimu sana unapoingia katika utumishi wa umma. Tunatoka katika vyuo tofauti na tamaduni tofauti hivyo, hata tabia zinakuwa tofauti. Mafunzo haya yanalenga kutufundisha namna utumishi wa umma ulivyo na jinsi mtumishi wa umma anavyotakiwa kuonekana na kutenda kazi” alisema Ayubu.

Aliwataka watumishi hao kubadilika baada ya mafunzo kimtazamo na kiutendaji na kuzingatia viwango vya juu katika utumishi wao. “Unajua unapoingia katika utumishi wa umma, unajikuta unafanya makosa, ila tunashindwa kukuchukulia hatua za kiutumishi badala yake tunalazimika kukufanyia ushauri zaidi. 

Tunabadilika na kuwa wazazi na walezi katika kuwaelimisha watumishi” alisema Ayubu. Aliongeza kuwa baada ya mafunzo haya watakuwa wakiwachukulia hatua stahili za kiutumishi watumishi wote watakaotenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Alisema kuwa katika mafunzo hayo watumishi wa umma watafundishwa muundo wa serikali, uendeshaji wa shughuli za serikali, utunzaji wa kumbukumbu, maadili ya utumishi wa umma, maboresho ya utumishi wa umma, huduma kwa mteja, sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake, mpango wa kudhibiti ukimwi kwa watumishi wa umma na upimaji wa wazi utendaji kazi kwa watumishi wa umma.

Mafunzo elekezi ya awali ya siku tano kwa watumishi wapya wa umma yameandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na chuo cha utumishi wa umma (TPSC) yakishirikisha watumishi wapya 107 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi za wakuu wa wilaya na hospitali ya rufaa ya mkoa.
=30=

IRUWASA YAPONGEZWA KUTENGA SIKU YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, IRINGA
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Iringa mjini (IRUWASA) imepongezwa kwa utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa wa Iringa la kutenga siku ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero na malalamiko ya wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipotembelea Iruwasa kukagua utekelezaji wa agizo lake mkoani Iringa.
Afisa Uhusiano IRUWASA Restituta Sakila (kushoto) akimuonesha jambo Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipotembelea taasisi hiyo kukagua wanavyopokea na kusikiliza Malalamiko ya wananchi

“Nianze kwa kuwapongeza IRUWASA kwa kazi nzuri mnayofanya kupokea na kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi. Mheshimiwa Rais Dr John Magufuli amekuwa akipokea barua nyingi za malalamiko ya wananchi. Malalamiko mengine ni madogo madogo ambayo sisi wasaidizi wake tunaweza kuyatatua. Ni matarajio ya mheshimiwa Rais kuona kero na malalamiko yote ya wananchi yanapatiwa ufumbuzi. Hili mnalotekeleza IRUWASA ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya mheshimiwa Rais” alisema mheshimiwa Masenza.

Akiongelea changamoto ya upotevu wa maji inayowakabili wananchi wengi wanaohudumiwa na IRIWASA, mkuu wa mkoa aliwataka kuweka utaratibu maalum wa kupitia miundombinu ya mtandao wa mabomba ili kujiridhisha na uimara wake. Aidha, aliwataka IRUWASA kutafuta ufumbuzi wa mita za maji za malipo kabla ya huduma ya maji ambazo wateja wengi wametokea kuzipenda.

Katika taarifa ya mkurugenzi mtendaji wa IRUWASA, Gilbert Kayange kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kuhusu usikilizaji na utatuzi wa kero na malalamiko ya wananchi alisema kuwa, jumla ya wananchi 79 waliwasilisha kero na mlalamikoa yao. 

“Kati ya kero na malalamiko 79 yaliyowasilishwa, 71 yalipatiwa ufumbuzi na wananchi kuridhika. Kero nane tunaendelea kuzishughulikia ambazo ni wananchi kuhitaji huduma ya kuunganishwa na mtandao wa maji” alisema Kayange.

Kayange alisema kuwa IRUWASA imefanikiwa kufikisha huduma ya maji kwa 96% ya wakazi wa Manispaa ya Iringa. Aliongeza kuwa mamlaka yake inaendelea kushughulikia tatizo la kufikisha huduma ya maji katika maeneo ya Kitwiru, Igumbilo na Isakalilo.

Mkurugenzi mtendaji wa IRIWASA, alisema kuwa 90% ya malalamiko ya wananchi yanatokana na ukubwa wa bili za maji na mivujo ya maji. Aliongeza kuwa awali wananchi walikuwa wakifanyiwa tathmini ya vifaa na wananchi kununua vifaa wenyewe jambo lililosababisha ununuzi wa vifaa vilivyo chini ya kiwango na kuchangia katika uvujaji wa maji. 

Alitaja changamoto ya mita za huduma ya malipo kabla kuwa zinapendwa na wateja wengi zaidi na mamlaka haina uwezo wa kuwafungia wateja wote na kusababisha mita hizo kufungwa kimkakati.

Mkuu wa mkoa wa Iringa, yupo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo lake kwa taasisi za umma kutenga siku maalum ya akusikiliza kero na malalamiko ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi. Katika siku yake ya kwanza alitembelea taasisi za IRUWASA, TANESCO, TRA na Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa.
=30=