Saturday, December 8, 2012

RC ATAKA BONDE LA MGOLOLO LITUMIKE VIZURI


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma amewataka wananchi wa Kata ya Makungu na Kiyowela kulitumia vizuri bonde la Mgololo kwa kujihakikishia chakula cha kutosha na kulima klibiashara.

Ushauri huo ameutoa alipofanya ziara ya siku mbili ya kutembelea, kuhamasisha na kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya ya Mufindi.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma

Dkt. Christine amesema kuwa ili bonde hilo liweze kuwa na manufaa kwa wananchi ni lazima litumiwe vizuri kwa wananchi kulima kwa kufuata nanuni la kilimo bora ili waweze kujihakikishia chakula cha kutosha. Amesema kuwa uhakika wa chakula cha kutosha ni muhimu sana kumuwezesha mwananchi kutekeleza majukumu yake ya kujiletea maendeleo. Amesema “ili mtu uweze kufanya shughuli za maendeleo ni lazima awe ameshiba, ili awe ameshiba, ni lazima awe na chakula na uhakika wa chakula cha kutosha, hivyo litumieni bonde hili kwa kujihakikishia chakula cha kutosha”.

Aidha, amesisitiza kutanuliwa kwa skimu ya umwagiliaji maji katika bonde hilo ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Amesema “katika kilimo cha umwagiliaji hakuna kupumzika, yaani unapanda, unavuna na kupanda tena”. Amesema kupitia kilimo cha umwagiliaji, wakulima hao waangalie kuboresha zaidi kilimo chao na kuwa kilimo cha kibiashara. Amesema kuwa kufanya hivyo kutawakikishia uhakika wa chakula na kuuza mazao yao jambo litakalowawezesha kuwa na fedha nyingi kwa ajili ya matumizi mengine.

Akiwasilisha taarifa ya mradi wa umwagiliaji maji Mgololo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Emelitha Nganung’a amesema kuwa ujenzi wa banio na mfereji mkuu wa mita 400 ulifanyika mwaka2007/2008 sambamba na barabara ya Lugolofu hadi mashambani yenye km 9 ilitengenezwa. Mwaka 2009-2011 ujenzi wa mfereji mkuu wenye urefu wa km 4.8 na mifereji ya kati km 12.33 pia ilijengwa. Amesema kuwa aktika mfereji mkuu madaraja matano makubwa na madaraja matano madogo yamejengwa. Aidha, amesema vigawa maji 12 na makaravati 13 vilijengwa. Mifereji ya kati vijawa maji 54 vilijengwa. Mifereji midogo ilipimwa na kuwa na urefu wa km 23.80. Amesema jumla ya hekta 259 zimepimwa kati ya hekta 600 na wakulima 91 wamegawiwa mashamba.

Akizungumzia ushirika wa wakulima, Nganung’a amesema kuwa mwaka 2007 wakulima waliunda ushirika wa vijiji vya Lugolofu na Makungu ambao ni ushirika wa wamwagilia maji Mgololo. Amesema kuwa idara ya kilimo wilaya ya Mufindi iliwezesha mafunzo ya uundaji na uendeshaji wa ushirika huo na kufikisha wanachama 788. katika kuleta ufanisi kwa vitendo, wanachama 50 waliwezeshwa kutembelea skimu ya umwagiliaji ya Igomelo na Uturo zilizopo wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya. 

Akielezea shughuli walizofanya wanachama, amesema kuwa walishiriki katika katika upandaji majani kuzunguka inteki, kupanga mawe chiin ya kibanio, kufyeka eneo lote la shamba kabla ya upimaji mifereji midogo ya ndani na kushiri katika uchimbaji wa mifereji midogo ndani.
=30=


 




No comments:

Post a Comment