Wednesday, June 25, 2014

KILOLO YAKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA NA RUSHWA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- KILOLO
Wilaya ya kilolo imeendelea kukabiliana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya na rushwa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya na maisha bora.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya kilolo Gerald Guninita katika risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete iliyosomwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo, Yusuph Msawanga mjini Kilolo.
Gininita amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni moja kati ya changamoto zinazolikabili taifa katika kipindi hiki. Amesema kuwa wilaya ya Kilolo katika kupambana na dawa za kulevya inatekeleza kaulimbiu isemayo “furahia afya siyo dawa za kulevya”. Amesema kuwa wananchi wamekuwa wakielimishwa kwa njia mtambuka athari za dawa za kulevya kiafya, kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa wilaya yake imeemdela kufanya uhamasishaji kwa vijana kuanzisha shughuli za kiuchumi.
Akiongelea mapambano dhidi ya rushwa, Guninita amesema kuwa wilaya ya Kilolo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatekeleza kaulimbiu isemayo “palipo na rushwa hakuna maendeleo”. Utekelezaji huo ameutaja kuwa ni kutoa elimu kwa umma pamoja na kuzindua club za wapinga rushwa katika shule za sekondari (33) na shule za msingi (15). Mkakati mweingine ameutaja kuwa ni kufanya tafiti ndogo ndogo zenye matokeo ya haraka katika kutambua mianya ya rushwa ili zisaidie kukabiliana na tatizo la rushwa. Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni kupokea taarifa za malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria.
=30=

No comments:

Post a Comment