WAGANI KAZI KUWEZESHWA IRINGA
Serikali Mkoani Iringa ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo na wapani kazi ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao wa kukuza kilimo katika maeneo waliyopo na kupunguza umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma
wakati akigawa baisketi 373 zenye thamani ya shilingi milioni 54 kwa wagani
kazi walioshiriki mafunzo ya ugani kazi mwaka 2009, tukio lililofayika katika
uwanja wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dr. Christine Ishengoma
akikabidhi baiskeli kwa Mganikazi
Dkt. Christine amesema kuwa Serikali ya Mkoa inatambua umuhimu wa Wagani
kazi katika kukuza sekta ya Kilimo Mkoani Iringa na kuwakumbusha kuwa Wagani
kazi ndiyo mabwana na mabibi shamba katika maeneo yao. Amesema kuwa kutokana na
umuhimu huo kwa wakulima, Serikali itaendelea kuwasaidia Wagami kazi hao kwa
kuwapatia mafunzo ya mara kwa amra na mbinu bora za kilimo cha kisasa pamoja na
kuwapatia nyenzo za kufanyia kazi ili kuleta mapinduzi katika Kilimo Kwanza.
Amesema lengo la kuwakabidhi baiskeli hizo kuwawezesha Wagani kazi hao
kuwafikia wakulima wengi kwa urahisi na haraka zaidi. Amesema “nawakabidhi
baiskeli hizi ili mkafanye kazi iliyokusudiwa”. Amesema kuwa nilazima wakafanye
kazi kwa nguvu zaidi kwa sababu watapimwa kutokana na kazi walizozifanya.
Akiongelea pembejeo za kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa
utaratibu utaendelea uleule isipokuwa sasa mawakala watatoka juu ambao
watasambaza pembejeo hizo wenyewe kwa wakulima na kuwataka wakuu wa Wilaya
kusimamia vizuri zoezi hilo ili pembejeo ziweze kuwafikia walengwa.
Katika Taarifa fupi ya utendaji kazi wa Wagani kazi Mkoani Iringa
iliyowasilishwa na Shenal Nyoni, Afisa Kilimo Mkuu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, imesema kuwa mwanzoni wa mwaka 2000 Mkoa w Iringa ulikuwa
unakabiliwa na tatizo la uhaba wa wataalam wa kilimo na mifugo katika ngazi ya
Kijiji na Kata baada ya Serikali kusimama katika kuajiri wataalamu katika Sekta
ya Kilimo pamoja na Sekta nyingine.
Amesema kutokana na hilo Mkoa wa Iringa ulibuni utaratibu wa kuwa na
Wagani kazi ambao watasaidia kutoa huduma za ugani kwa kushirikiana na wataalam
wa kilimo na mifugo vijijini.
Nyoni amesema kuwa mafunzo kwa Wagani kazi yalifanyika katika kila
Halmashauri kwa muda wa wiki mbili na Wagani kazi 406 walipatiwa mafunzo kwa
lengo la kufundisha Wagani kazi 50 katika kila Halmashauri. Amesema kuwa Wagani
kazi hao walifundishwa juu ya kanuni za kilimo na ufugaji bora na fursa ya
kujifunza kwa vitendo.
Akionglea mgawanyo wa baiskeli hizo katika mabano, Afisa Kilimo huyo
amesema kuwa Manispaa ya Iringa (22), Wilaya ya Iringa (58), Wilaya ya Kilolo
(50), Wilaya ya Mufindi (50), Wilaya ya Njombe (50), Njombe Mji (44), Wilaya ya
Ludea (49), Wilaya ya Makete (50)
Ikumbukwe kuwa baiskeli hizo ni ahadi aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipofungua mafunzo ya wiki
mbili kwa ajili ya Wagani kazi katika Mkoa wa Iringa mwaka 2009.
Viongozo wa Mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na Waganikazi muda mfupi baada ya kukabidhiwa baiskeli zao
=30=