Sunday, November 19, 2017

WANAIRINGA WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO KUKABILIANA NA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-IRINGA
Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na mfumo wa maisha usiozingatia lishe bora.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa akizindua kampeni tambuzi ya kifua kikuu na magonjwa yasiyoambuliza katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora mjini Iringa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza
Mheshimiwa Masenza alisema kuwa magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mara nyingi hutokana na mfumo wa maisha usiozingatia afya. Alisema magonjwa hayo hutokana na kutokufanya mazoezi, kuwa na uzito wa juu na kula vyakula visivyozingatia lishe bora. 

Alivitaja vyanzo vingine vya magonjwa hayo kuwa ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri.

Kwa bahati mbaya, magonjwa haya hayana dalili katika hatua za mwanzoni lakini dalili huanza kuonekana pale madhara sugu yanapoanza kuonekana. Magonjwa haya ni kisukari, shinikizo la damu na saratani” alisema mheshimiwa Masenza. 

Alisema kuwa mazoezi ni jambo la msingi katika kuhakikisha jamii inaepuka magonjwa hayo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa aliwomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika bustani ya Manispaa kupima afya ili ugonjwa ukigundulika tiba ianze mara moja. Aliwakumbusha wananchi kuwa huduma hiyo ni muitikio wa nia ya Rais Dr. John Magufuli ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na afya njema ili waweze kuchapa kazi na kuivusha Tanzania kwenda nchi ya uchumi wa kati.

Akiongelea maandalizi ya kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza, mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza mkoa wa Iringa, Dr Tatu Mbotoni alisema kuwa timu ya madaktari na madaktari bingwa imejipanga vizuri. Alisema kuwa huduma hiyo itatolewa kwa kasi na viwango ili kuwawezesha wananchi wa Iringa kutumia muda mfupi katika kupata huduma hiyo.

Aidha, alizitaja huduma zitakazotolewa katika bustani ya Manispaa kuwa ni upimaji wa ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, VVU na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake.

Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children kwa kuunga juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema limefadhili zoezi la upimaji afya katika mkoa wa Iringa.
=30=

KAMPENI TAMBUZI TB KUTOA ELIMU NA KUPIMA WANANCHI IRINGA

Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- IRINGA
Kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza inalenga kutoa elimu kwa jamii na kupima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ili matibabu yaweze kuanza mapema.

Kauli hiyo ilitolewa na daktari bingwa wa kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu kutoka hospitali ya Kibong’oto Dr. Isaya Jelly alipokuwa akiongea na wanahabari mkoani Iringa kuhusu kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza katika bustani ya Manispaa ya Iringa.
 
Dr Isaya Jelly
Dr. Jelly ambae pia anaratibu shughuli za shiriki la Save the Children kupitia mpango wa Taifa wa kifua kikuu na ukoma (NTLP) alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwasogeza wananchi karibu na huduma za upimaji na tiba. “Kampeni hii imelenga kuwasogeza karibu wananchi kupata habari na kupima kama wanavimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuanza dawa” alisema Dr. Jelly.

Dr. Jelly alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kampeni hiyo ni mzuri. “Hali ya kimaisha inafanya watu wasizifuate huduma katika vituo vya afya, kwa kuongopa mlolongo uliopo katika vituo vya huduma. Huduma za hapa uwanjani ni za haraka haraka” alisema Dr. Jelly. 

Alisema kuwa wananchi watakao pima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu baada ya uchunguzi majibu yao watatumiwa kupitia simu zao za mkononi. Aidha, kwa wananchi watakaopima virusi vya ukimwi majibu watapewa baada ya kupewa somo la kuwekwa sawa kisaikilojia.

Katika kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza, imelenga kuwafikia wagonjwa 100 katika Manispaa ya Iringa na zoezi hilo litaelekea katika gereza la Iringa kesho kwa ajili ya kuwapima na kuwaanzishia tiba wanaorekebishwa tabia watakaogundulika na vimelea vya kifua kikuu.
=30=

IRINGA KUIBUA WAGONJWA WA TB NA KUWATIBU

Na Mwandishi Maalum Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-IRINGA
Mkoa wa Iringa umejizatiti kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu ili waanze matibabu mapema na kuzuia ugonjwa huo kuambukiza wengine.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa akizindua kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora mjini Iringa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Amina Masenza
Mheshimiwa Masenza alisema “njia kuu ya kuzuia kuenea kwa kifua kikuu ni mgonjwa kugunduliwa mapema pale anapoanza kuonyesha dalili za awali na kuwekwa katika matibabu bila kuchelewa. Mgonjwa mmoja anaweza kuwaambukiza watu wasiopungua 20 kwa mwaka. Bila ya kuweka juhudi za kuwapata wagonjwa mapema na kuwatibu, kifua kikuu kitaendelea kuenea na kuwamaliza watu wengi nchini”. 

Alisema kuwa kwa kipindi cha Januari 2016-Juni 2017, mkoa wa Iringa umeweza kugundua wagonjwa wapatao 455. Alisema kuwa kwa lengo la Manispaa ya Iringa ni kupima na kugundua watu 528 kwa kila watu 100,000. Alisema kuwa hali hiyo, inadhihirisha uhiotaji wa kupima na kugundua watu wengi zaidi.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa ni rahisi kujikinga na ugonjwa wa kifua kikuu. Alizitaja dalili za kifua kikuu kuwa ni kukohoa kwa wiki mbili au zaidi na homa za mara kwa mara hasa nyakati za jioni. Dalili nyingine ni kutokwa na jasho lisilo la kawaida wakati wa usiku hata kama kuna baridi. Kutoa makohozi yaliyochanganyika na damu na kupungua uzito ni miongoni mwa dalili hizo. 

Nawashukuru sana wenzetu wa shirika la Save the Children kwa kuunga juhudi za Serikali za kuwatambua na kuwapima wale watakaobainika kuwa na dalili za kifua kikuu katika jamii yetu” alisema mheshimiwa Masenza.

Alishauri kuwa mtu anapoona mojawapo ya dalili hizi kuwahi katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba. “Serikali bado inaendelea kutoa dawa za kifua kikuu bila ya malipo yoyote. Dawa zinapatikana katika vituo vyote vya umma na vile vya binafsi” alisisitiza mheshimiwa Masenza.
=30=

WANAIRINGA WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI YA VIOUNGO KUKABILIANA NA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-IRINGA
Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na mfumo wa maisha usiozingatia lishe bora.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa akizindua kampeni tambuzi ya kifua kikuu na magonjwa yasiyoambuliza katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora mjini Iringa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Amina Masenza
Mheshimiwa Masenza alisema kuwa magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mara nyingi hutokana na mfumo wa maisha usiozingatia afya. 

Alisema magonjwa hayo hutokana na kutokufanya mazoezi, kuwa na uzito wa juu na kula vyakula visivyozingatia lishe bora. Alivitaja vyanzo vingine vya magonjwa hayo kuwa ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri.

Kwa bahati mbaya, magonjwa haya hayana dalili katika hatua za mwanzoni lakini dalili huanza kuonekana pale madhara sugu yanapoanza kuonekana. Magonjwa haya ni kisukari, shinikizo la damu na saratani” alisema mheshimiwa Masenza. Alisema kuwa mazoezi ni jambo la msingi katika kuhakikisha jamii inaepuka magonjwa hayo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa aliwomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika bustani ya Manispaa kupima afya ili ugonjwa ukigundulika tiba ianze mara moja. Aliwakumbusha wananchi kuwa huduma hiyo ni muitikio wa nia ya Rais Dr. John Magufuli ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na afya njema ili waweze kuchapa kazi na kuivusha Tanzania kwenda nchi ya uchumi wa kati.

Akiongelea maandalizi ya kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza, mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza mkoa wa Iringa, Dr Tatu Mbotoni alisema kuwa timu ya madaktari na madaktari bingwa imejipanga vizuri. Alisema kuwa huduma hiyo itatolewa kwa kasi na viwango ili kuwawezesha wananchi wa Iringa kutumia muda mfupi katika kupata huduma hiyo.

Aidha, alizitaja huduma zitakazotolewa katika bustani ya Manispaa kuwa ni upimaji wa ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, VVU na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake.

Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children kwa kuunga juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema limefadhili zoezi la upimaji afya katika mkoa wa Iringa.
=30=

KAMPENI TAMBUZI TB KUTOA ELIMU NA KUPIMA WANANCHI IRINGA

Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- IRINGA
Kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza inalenga kutoa elimu kwa jamii na kupima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ili matibabu yaweze kuanza mapema.

Kauli hiyo ilitolewa na daktari bingwa wa kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu kutoka hospitali ya Kibong’oto Dr. Isaya Jelly alipokuwa akiongea na wanahabari mkoani Iringa kuhusu kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza katika bustani ya Manispaa ya Iringa.
 
Dr Isaya Jelly
Dr. Jelly ambae pia anaratibu shughuli za shiriki la Save the Children kupitia mpango wa Taifa wa kifua kikuu na ukoma (NTLP) alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwasogeza wananchi karibu na huduma za upimaji na tiba. 

Kampeni hii imelenga kuwasogeza karibu wananchi kupata habari na kupima kama wanavimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuanza dawa” alisema Dr. Jelly.