Sunday, November 19, 2017

KAMPENI TAMBUZI TB KUTOA ELIMU NA KUPIMA WANANCHI IRINGA



Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- IRINGA
Kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza inalenga kutoa elimu kwa jamii na kupima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ili matibabu yaweze kuanza mapema.

Kauli hiyo ilitolewa na daktari bingwa wa kifua kikuu cha kawaida na kifua kikuu sugu kutoka hospitali ya Kibong’oto Dr. Isaya Jelly alipokuwa akiongea na wanahabari mkoani Iringa kuhusu kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza katika bustani ya Manispaa ya Iringa.
 
Dr Isaya Jelly
Dr. Jelly ambae pia anaratibu shughuli za shiriki la Save the Children kupitia mpango wa Taifa wa kifua kikuu na ukoma (NTLP) alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwasogeza wananchi karibu na huduma za upimaji na tiba. 

Kampeni hii imelenga kuwasogeza karibu wananchi kupata habari na kupima kama wanavimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na kuanza dawa” alisema Dr. Jelly.

Dr. Jelly alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kampeni hiyo ni mzuri. “Hali ya kimaisha inafanya watu wasizifuate huduma katika vituo vya afya, kwa kuongopa mlolongo uliopo katika vituo vya huduma. Huduma za hapa uwanjani ni za haraka haraka” alisema Dr. Jelly. 

Alisema kuwa wananchi watakao pima vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu baada ya uchunguzi majibu yao watatumiwa kupitia simu zao za mkononi. Aidha, kwa wananchi watakaopima virusi vya ukimwi majibu watapewa baada ya kupewa somo la kuwekwa sawa kisaikilojia.

Katika kampeni tambuzi za kifua kikuu na magonjwa yasiyoambukiza, imelenga kuwafikia wagonjwa 100 katika Manispaa ya Iringa na zoezi hilo litaelekea katika gereza la Iringa kesho kwa ajili ya kuwapima na kuwaanzishia tiba wanaorekebishwa tabia watakaogundulika na vimelea vya kifua kikuu.
=30=




No comments:

Post a Comment