Monday, August 26, 2013

PICHA ZA MATUKIO YA MKUTANO WA AMANI ULIOANDALIWA NA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (katikati) Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (kushoto) na Mstahiki Meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwingi (kulia)

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (katikati) Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (kushoto) na Mstahiki Meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwingi (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa, Afande Mungi
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt Leticia Warioba (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu (katikati) na kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya 

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt Leticia Warioba (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu (katikati) na kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya

 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita (kushoto)

 Wadau wa amani wakifuatilia mkutano

 Wadau wa amani wakifuatilia mkutano

 Wadau wa amani wakifuatilia mkutano

 Wadau wa amani wakifuatilia mkutano

 Wadau wa amani wakifuatilia mkutano

Ustaadh Rafik akisoma shairi kuhusu Amani

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma akisoma Hotuba



   Amir na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu waahmadiyya Tanznaia, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry

     Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akitoa mchango wake kuhusu Amani

              Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi akichangia kuhusu amani

                   Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo akichangia mkutanoni.

                      Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu akichangia mada

                Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita akichangia mkutanoni

Ag. RAS IRINGA ATAKA WADAU WOTE KUSHIRIKI KULINDA AMANI





Ushirikiano wa wananchi wote na wadau unahitajika katika kuhakikisha serikali inatimiza jukumu lake la kulinda na kusimamia amani na uslama nchini. 

          Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu

              Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi

           Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo


              Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu
 
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alipokuwa akichangia katika mkutano wa amani mkoa wa Iringa uliyoandaliwa na Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa. 

Wamoja amesema “serikali inalojukumu la kuhakikisha kuwa amani na usalama kwa watu wote, lakini katika kutekeleza hilo unahitajika ushirikiano wetu sote”. Amesema kuwa wananchi na wadau wote hawana budi kushirikiana katika kuhakikisha kuwa amani inadumishwa nchini. Amesema kuwa upendo ni nguzo mihumu katika kudumisha amani. Amesema amani haiwezi kuwepo kama hakuna upendo, na kushauri kuwa viongozi wote wajitahidi kuhubiri upendo ili kujihakikishia uendelevu wa amani.

Katika mchango wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amesema kuwaamani haiwezi kutafsiriwa kwa tafsiri moja pekee, bali inatafsiriwa kwa sifa zake. Amezitaja sifa hizo kuwa ni ukosefu wa vurugu na migogoro. Sifa nyingine amezitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa vurugu na uadui. Nyingine ni ukosefu wa chuki na ugomvi. 

Mungi amesema kuwa amani ya kweli inazo tabia sinazoonekana. Amezitaja tabia hizo kuwa ni kujali, kuheshimu, haki kwa watu wengine. Amesema kuwa tabia nyingine ni ukarimu na uvumilivu kwa imani ya watu wengine.

Amesema kuwa amani haishikiki bali ipo katika akili na roho na inapimika kwa kutokuwepo kwa vurugu. 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo amesema kuwa amani ni kichocheo kikubwa cha maendeleo nchini. Amesema kuwa ili jamii iweze kuwa na maendeleo ni lazima watu na makundi yote waweze kutii mamlaka zilizopo kisheria kwa sababu mamlaka zote zinatoka kwa Mungu. 

Evarista Kalalu amewataka wadau wote wa amani kujiuliza wamefanya nini katika kuhakikisha amani iliyopo inadumu na kuwa endelevu. “Tanzania hatuna mahali pa kukimbilia iwapo tutaamua kuvunja amani iliyopo. Wote wasio na amani wanakimbilia kwetu, hivyo sisi tutakimbilia kwa nani?” alihoji Mkuu wa Wilaya ya Mufindi. 

Amesema kuwa ni ukweli usiofichika kuwa katika jamii tunayoishi wapo watu wasiopenda amani hivyo ni jukumu letu kuwaripoti katika mamlaka husika. “Si kila mtu anaweza kuchukua hatua, hivyo tunahitaji kuwalinda wale wote wenye mamlaka za kuchukua hatua” alisisitiza Evarista. 
=30=

KUPUNGUA KWA UPENDO CHANZO CHA KUVUNJIKA AMANI




Kupungua kwa upendo baina ya wananchi ni chanzo cha kuvunjika kwa amani nchini kutokana na watu kukosa hofu ya Mungu.

              Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa akifungua mkutano wa kuzungumzia mchango wa uislam katika kuleta amani Duniani ulioandaliwa na Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo, mjini Iringa.

Dkt. Christine amesema kuwa uvunjifu wa amani nchini unatokana na kupungua kwa upendo baina ya wananchi. Amesema kuwa watu wanapungukiwa upendo kwa sababu wanakosa hofu ya Mungu. Amesema “natumaini kuwa wote tu mashaidi kuwa katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia au kusikia matukio yasiyo ya kawaida ya ukiukaji na uvunjifu wa amani nchini katika maeneo mbalimbali. Tumuombe Mwenyezi Mungu, apishe mbali, tuweze kudumisha amani na utulivu kwa kila mmoja”. 

Amesmea “matukio haya ni dalili mbaya kwa nchi yetu ambayo waasisi wetu walitujengea misingi mizuri ya umoja, amani, upendo na mshikamano wa kitaifa. Kutonaka na misingi hiyo ndiyo maana watanzania hatuna ubaguzi katika misingi ya udini na ukabila. Misingi hii ni mizuri na hatunabudi kuidumisha muda wote”. 

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kuhakikisha wanadumisha misingi ya amani iliyowekwa na waasisi wa Taifa kuanzia kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere. “Nawaomba sana ndugu zangu wa Mkoa wa Iringa, kwa umoja wetu tuhakikishe tunasimamia na kudumisha misingi hiyo ili kizazi cha sasa na kijacho kiweze kufurahia amani hii tuliyonayo. Tusikubali kuyumbishwa na kuacha amani na utulivu ipotee” alisisitiza Dkt. Christine.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewataka viongozi wote kutikomeza vitendo vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla. Amesema “ni wajibu wetu viongozi wa serikali na dini kuhakikisha tunatokomeza kabisa vitendo vyote vinavyopelekea uvunjifu wa amani katika mkoa wetu wa Iringa na nchi yetu kwa ujumla” Mkuu wa Mkoa wa Iringa.  

Akiongelea mchango wa uislamu katika kuleta amani duniani, Amir na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu waahmadiyya Tanznaia, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema kuwa uislamu maana yake ni amani na utii hivyo ni kitu cha ajabu kuitumia dini kufundisha kinyume na amani. Amesema kwa msingi huo, mwanadamu anatakiwa aishi kwa amani na muumba wake, nafsi yake, wanadamu wenzake na viumbe wengine. Amesmea kuwa muislamu wa kweli siku zote anakuwa ni mtu mnyenyekevu, mpole, mwenye huruma na anayejali haki za kila mtu na kila kitu.  

Sheikh Chaudhry amesema kuwa katika kusisitiza amani, uislamu unafundisha udugu wa wanadamu wote na kuhimiza uadilifu uliokamilika hata mbele ya maadui na kufundisha uhuru kamili wa kuabudu. 

Akiongelea sababu za kuvunjika kwa amani, amezitaja sababu hizo kuwa ni sababu za kiuchumi, kijamii, kisiana na kidini. Amesema kuwa miongoni mwa sababu hizo zote sababu za kidini ndizo zinazopelekea uvunjifu mkubwa wa amani pamoja na kuwa zimeungana na sababu nyingine.
=30=