Tuesday, July 24, 2012

PROF. J.A. MILLS AFARIKI DUNIA



Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Prof. John Attah Mills
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.

Rais Prof. John Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.

Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais  John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.

Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo Prof. John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.

Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.

" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Rais Prof. Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.

Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais Prof. John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.

Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Prof. Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.

Chanzo: BBC SWAHILI



 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA



MKOA WA IRINGA:
Simu Na.  026 2702191   
Fax    Na. 026 2700310
 
  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
   S. L. P. 858,

   IRINGA



YAH: MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA TAREHE 25 JULAI, 2012.


Wafanyakazi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Wananchi wa Manispaa ya Iringa kwa ujumla mnatangaziwa kuwa Tarehe 25 Julai, 2012 kutafanyika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Uwanja wa Bustani ya Manispaa ya Iringa saa 2:00 Asubuhi.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa atakuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo.
Unatakiwa kuhudhuria katika Maadhimisho hayo muhimu kwa Kudumisha Historia ya Ukombozi wa Nchi yetu.



Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
S.L.P 858
IRINGA