Timu ya Netiboli ya RAS Iringa imeiduwaza timu ya netiboli ya
mamlaka ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwa kuibugiza magoli 54-3.
Katika mchezo ulioanza kwa kasi kubwa ilionekana dhahiri kabisa
kuwa timu ya RAS Iringa imedhamiria kuibuka na ushindi ambapo dakika za mwanzo
walionekana kuwapeleka kasi Ngorongoro jambo lilitotafsiriwa na wengi kuwa timu
hiyo toka kaskazini mwa nchi ilipata hofu hata kabla ya mchezo.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa chuo kikuu cha kikatoliki
cha Ruaha (RUCU) ulishuhuriwa na mamia ya wananchi wapenda michezo.
Baada ya mchezo huo, mratibu wa timu zote za RAS Iringa, Issa
Matea alisema kuwa ushindi huo ni salamu za awali kwa timu pinzani. Akiongelea
ushindi huo, alisema kuwa ni ushindi huo ni chachu na hamasa aliyoitoa katibu
tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu kwa timu hiyo yenye wanadada mahiri.
=30=