TAMKO LA ASKOFU METHODIUS KILAINI
Askofu Methodius Kilaini
Kwa masikitiko makubwa
nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na
sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na
wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo.
Ni vibaya kwa gazeti lo
lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana natumaini
watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa kunikwazwa na
hilo.
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic
Diocese