Tuesday, August 31, 2010

ZIARA YA GADDAFI ITALIA UTATA MTUPU!

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amewasili mjini Rome siku ya jumapili katika ziara yake ya siku mbili nchini Italia.


Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi

Vyombo vya habari nchini Italia vimeikosoa vikali ziara hiyo hasa baada ya Gaddafi kufanya mkutano na wanawake vijana takribani 700 akiwaelezea umuhimu wa uislam katika nchi iliyobobea katika ukristo na hasa imani ya kikatoliki. Mkutano huo uliandaliwa na Mrembo wa zamani wa Italia Mara Carfagna ambae pia ni mtangazaji maarufu wa TV na mwaka uliopita aliteuliwa na waziri mkuu kuwa waziri wa haki sawa. Aidha katika mkutano huo taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema kuwa wanawake vijana walilipwa karibia Euro 70 na zawadi ya Qu’ran na watatu kati yao walislimu katika mkutano huo.



Warembo wa kiitaliano wakielekea katika mkutano na Gaddafi

Katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa katika jumba la kifalme la Ourinal na Rais Napolitano, alichukua nafisi hiyo kuipongeza ziara hiyo na kusema kuwa ziara hiyo itachangia kuleta amani katika mashariki ya kati na mediteranian. Aidha alimpongeza Gaddafi na kumuita kuwa kichicheo cha madabiliko ya kisasa barani Afrika. Katika dhifa hiyo ya kitaifa waitaliano walihudumiwa mvinyo mweupe ‘white wine’ wakati ujumbe wa Libya ulijiburudisha kwa juice ya machungwa.

Kiongozi huyo alipata wakati ngumu kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Roma wanaopinga ziara hiyo na wajimbe wa Seneti wa mlengo wa shoto, na Seneta wa chama cha Christian Democratic alisema kuwa uamuzi wa kumualika Gaddafi kulihutubia baraza la hilo la juu haukuwa sahihi. Aidha Waziri mkuu wa Italia hakuonesha kushtushwa na kelele hizo za wapingaji wa ziara hiyo na kusema kuwa hao ni wafungwa wa mawazo ya kale.


Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi (kushoto) na Warizi Mkuu

wa Italia Silvio Berlusconi (kulia)

Baadae, Waziri Mkuu, Silvio Berlusconi na Gaddafi walizindua maonesho ya picha na sherehe za kumbukumbu ya maadhimisho ya pili ya mkataba baina ya Italia na Libya ambapo Italia ilikubali kuilipa Libya fidia ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa kuikalia kimabavu. Aidha kama sehemu ya makubaliano hayo, Libya ilikubali kuwazuia maelfu ya waafrika wanaozamia Italia.

Wakati wa mazungumzo hayo ya jioni baina wa Berlusconi, Gaddafi na watu wengine wenye majina makubwa katika biashara nchini Italia, Gaddafi aliitaka Jumuiya ya Ulaya kutoa Euro bilioni 7.1 kwa mwaka kwa ajili ya kupambana na uhamiaji haramu.

Nyota ya Gaddati kimataifa ilianza kung’ara mwaka 2008 baada ya kusaini makubaliano ya mabilioni ya fidia na sasa Italia ni mshirika mkubwa wa kibiashara.

Muammar al- Gaddafi (Muʿammar alQadhdhafi) alizaliwa 1942 katika mji wa Surt, kaskaazini mwa Libya na amekuwa kiongozi wa Libya tangu mwaka 1969. Gaddafi alizaliwa katika hema jangwani na amehitimu masomo ya chuo kikuu cha Libya na shule ya kijeshi ya Libya. Akiwa katika cheo cha Kaptaini jeshini aliongoza mapinduzi yaliyomuangusha mfalme Idris I.

(Habari hii imeandaliwa kwa msaada wa Reuters euronews)