Na. Afisa Habari Mkoa wa Mwanza
Jumla ya wanafunzi wapatao ishini na saba wamejeruhiwa
vibaya kufuatia ajali mbaya iliyo lihusisha garia aina ya Roli
lililokuwa likisafiri kutoka Kasororo kwenda Misasi kwenye shughuli za
Umiseta.
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Afisa Michezo wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, nikuwa gari hilo lilikuwa
likiwasafirisha wanafunzi kwenda kwenye Michezo ajali imetokea katika
Tarafa ya Mbarika Wilaya ya Misungwi Mkoani hapa.
Majeruhi 12 wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya
Missungwi na kumi na watano(15), walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa
Bugando kwa Matibabu zaidi.
Taarifa hiyo imesema pia kuwa hali ya Majeruhi mmoja sio
nzuri sana kwani sehemu kubwa ya kichwa ndio iliyojeruhiwa vibaya, huku
mwalimu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja akiwa amechanwa na
kitu kinacho zaniwa kuwa ni chuma sehemu ya kifua.
Hata hivyo Ninaendelea kufatilia juu ya tukio hili na
habari kamili juu ya Majina ya Majeruhi hao nitawatumia kupitia mtandao
wetu wa Mawasiliano.