Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa-IRINGA
Wananchi
wa mkoa wa Iringa wametahadharishwa kutumia maji ya mto Ruaha kutokana na
vipimo kuonesha kuwa maji hayo yanavimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu.
Tahadhari
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa
akiongea mahojiano ya moja kwa moja kwenye kipindi cha nyota ya asubuhi kinachorushwa
na kituo cha redio Furaha cha mjini Iringa leo.
Mheshimiwa
Masenza alisema “maji ya mto Ruaha siyo
safi na salama. Baada ya kuyapima imegundulika yana vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu”.
Hivyo, amewataka wananchi kuchukua tahadhari katika matumizi ya maji hayo.
Wakati
huohuo, aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuongeza kasi ya ujenzi wa vyoo
bora. Alisema kuwa choo bora ni kile kisichomruhusu mtumiaji kukutna na kile
anachokitoa ili kisimsababishie maradhi.
Alisema kuwa choo ni sehemu ya
kupumzika hivyo, kinatakiwa kutayarishwa vizuri ili kumstiri anayekitumia kwa
kuwa na nafasi ya kutosha na kuruhusu hewa ya kutosha kupita. Aliwataka wananchi
kuunga mkono juhudi za Serikali zinazohamasisha kujenga jamii yenye afya njema.
=30=