Sunday, October 1, 2017

MAONESHO YA UTALII KARIBU KUSINI NA SIDO KUTANGAZA FURSA

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Maonesho ya utalii karibu kusini na wajasiriamali wa SIDO yatumike kutangaza shughuli, fursa na vivutio vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati wa kufungua maadhimisho ya siku ya utalii Duniani, maonesho ya Karibu Kusini na maonesho ya shughuli za viwanda vidogo (SIDO) mjini Iringa jana.
Prof. Jumanne Maghembe

Prof. Maghembe alisema “kipekee nimefurahishwa na maonesho ya karibu kusini mwaka 2017 ambayo kwa mwaka huu yamejumuisha wajasiriamali wa SIDO ambao ni wazalishajai wa bidhaa mbalimbali zinazoweza pia kutumiwa na watalii na kutoa huduma za kitalii nchini. Karibu kusini ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa ya nyanda za juu kusini na kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea vivutio hivyo”. 

Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania ina maeneo mengi yenye fursa za uwekezaji ambazo hazijaendelezwa ipasavyo.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni ukanda wa nyanda za juu kusini wenye vitutio vingi na vizuri vya utalii wakiwemo wanyama pori. Vivutio vingine alivitaja kuwa ni hifadhi za misitu asili, mandhari nzuri za kuvutia, bonde la usangu na mto ruaha, ziwa nyasa na kimondo. 

Vivutio hivi hutoa fursa na kuendeleza utalii katika ukanda huu. Aidha, ni wakati muafaka wa kuzitangaza fursa hizi ili kuvutia wawekezaji waje kuwekeza katika ukanda huu” alisema Prof. Maghembe.

Nae mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alisema kuwa mkoa wake daima utakuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ya mfano na kukua kwa kasi.
 =30=

VYUO VIKUU IRINGA KUJENGA MABANDA YA KUDUMU KIHESA-KILOLO

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Vyuo vikuu wilayani Iringa vimetakiwa kujipanga kuwa na mabanda ya kudumu katika maonesho ya Utalii Karibu Kusini mwaka 2018.

Rai hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika salamu zake kwenye usiku wa Utalii Karibu Kusini uliofanyika katika chuo cha ualimu Kreluu mjini Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela

Kasesela alisema kuwa mwaka 2018, maonesho ya Utalii Karibu Kusini yatafanyika katika uwanja wa Kihesa Kilolo na kuvitaka vyuo vikuu kuwa na mabanda ya kudumu kama taasisi za kitaaluma katika uwanja huo mpya. Alisema kuwa anatoa kipaombele kwa vyuo vikuu kutokana na mchango wao mkubwa katika kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya wilaya ya Iringa.

Wilaya ya Iringa tunajiandaa mwakani kuwapokea kwa nguvu. Lengo letu katika maonesho ni kuwa namba moja au mbili baada ya maonesho ya Dar es Salaam. Sisi tunataka kufanya maonesho si biashara” alisema Kasesela.

Akiongelea utofauti katika utalii na maeneo mengine, mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ndiyo hifadhi pekee utakayokuta wanyama wengi wakubwa katika kundi moja. Hii inatofutisha na meneo mengine na kutengeneza kivutio cha kipekee mtalii anapokuwa hifadhini.

Wakati huohuo, mkuu wa wilaya ya Iringa aliitaka jamii kumlinda ndege Tumbusi ambaye pia ni kivutio kizuri cha utalii wa ndege dhidi ya kutoweka kwake.

JAMII YATAKIWA KUJIVUNIA RASILIMALI ZA NCHI

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Jamii imetakiwa kujivunia nchi na rasilimali zilizopo pamoja na vivutio vya utalii na kuvilinda ili viwe endelevu.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamhuri William aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza katika usiku wa Utalii Karibu Kusini uliofanyika katika chuo cha ualimu Kreluu mjini Iringa jana.

William alisema kuwa jamii ya mikoa ya nyanda za juu kusini inatakiwa kujivunia nchi yao na rasilimali zilizopo hasa utunzaji na uhifadhi wa vivutio vya utalii. “Utalii ni uzalendo, lazima tujivunie nchi yetu na rasilimali tulizonazo. Vivutio vya utalii vyote tunavyoviona na kuvisikia ni sehemu ya rasilimali muhimu za nchi ambazo lazima tuzitunze ili nazo zituletee uchumi” alisema William.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William

Mkuu wa wilaya ya Mufindi alishauri rasilimali vivutio vya utalii kuhifadhiwa na kutunzwa ili visiharibiwe na kutoweka. “Katika utunzaji wa vivutio vya kitalii, ndiyo vitatuletea fedha nyingi na hatimae kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema William.

Alisema kuwa serikali imeamua kuutangaza utalii kisayansi ili ulete matokeo kwa wananchi. Aliwaomba wananchi kuwa sehemu ya kutangaza utalii ili kuleta mafanikio makubwa zaidi.

Akitoa maoni yake, mwanafunzi wa chuo cha ualimu Kreluu, Yuster Tweve alisema kuwa usiku wa Utalii Karibu Kusini ni fursa nzuri ya kuwakutanisha wadau mbalimbali pamoja na kujadili fursa zilizopo katika sekta ya utalii. Alishauri kuwa usiku wa utalii uwe unafanyika siku zote za maonesho ya Utalii Karibu Kusini ili wadau mbalimbali wapate nafasi ya kukaa na kubadilishana mawazo yatakayochangia katika kukuza utalii.
=30=

TANROADS IRINGA KUBORESHA BARABARA ILI WATALII WANUFAIKE

Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Wakala wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Iringa kuendelea kujenga na kuimarisha barabara ili watalii waweze kunufaika na huduma ya usafiri bora.

Kauli hiyo ilitolewa na msimamizi wa banda la TANROADS mkoa wa Iringa, Subira Anyisile alipokuwa akielezea nafasi ya TANROADS katika kukuza sekta ya utalii mkoa wa Iringa kwenye siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na shughuli za wajasiriamali wa viwanda vidogo - SIDO katika uwanja wa Kichangani mjini Iringa.
Msimamizi wa Banda la TANROADS

Anyisile alisema kuwa Wakala wa barabara una mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini. “Sisi TANROADS tunahusika na ujenzi na ukarabati wa barabara nchini. Utakubaliana nami kuwa barabara ndiyo kichocheo kikubwa cha kukuza sekta ya utalii nchini. Watalii hawawezi kufika mbugani au katika eneo la kivutio cha utalii bila barabara” alisema Anyisile. 

Katika kuhakikisha watalii wa ndani na nje wanaendelea kufurahia huduma za barabara, TANROADS imekuwa ikifanya ukarabati mkubwa na mdogo katika baadhi ya barabara zake ili zipitike muda wote. Alisema kuwa lengo la ujenzi na ukarabani wa barabara ni kurahisisha usafiri na kuchochea watalii kutembelea maeneo ya vivutio na kuuza na kununua bidhaa za kitalii. 

“Katika biashara hiyo mzunguko wa fedha unakuwepo na uchumi unakuwa kwa sababau maeneo mengi yanafunguka baada ya kuwa na mtandao wa barabara” alisema Anyisile.  

Akiongelea ujenzi wa barabara inayoelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Iringa- Msembe) kwa kiwango cha lami, Anyisile alisema kuwa upembuzi na usanifu umekamilika zinasubiriwa fedha tu.  
Wakala wa barabara mkoa wa Iringa unasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa km 1,192.9, kati ya hizo km 417.1 ni za lami na km 775.8 ni changarawe.
=30=