Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Mikoa
ya nyanza za juu kusini imetakiwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika
mikoa yao ili vifahamike na kutoa fursa ya kukuza uchumi wa wananchi.
Kauli
hiyo ilitolewa na naibu waziri wa maliasili na utalii mhandisi Ramo Makani
katika salamu zake katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya utalii Duniani,
maonesho ya Karibu Kusini na shughuli za viwanda vidogo (SIDO), yaliyofanyika
katika uwanja wa kichangani Manispaa ya Iringa jana.
Mhandisi
Makani alisema kuwa mikoa ya nyanda za juu kusini ina vivutio vingi na vya
kipekee. Alisema kuwa vivutio hivyo vikitangazwa na kufahamika kwa watu
watavutiwa kuvitembelea na kununua bidhaa zinazotokana na utalii.
Aidha,
aliitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kukuza utalii kwa kanda ya
nyanda za juu kusini. Alisema kuwa sekta binafsi ina mchango muhimu sana katika
kukuza uchumi.
=30=
No comments:
Post a Comment