Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Vyuo
vikuu wilayani Iringa vimetakiwa kujipanga kuwa na mabanda ya kudumu katika
maonesho ya Utalii Karibu Kusini mwaka 2018.
Rai
hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika salamu zake
kwenye usiku wa Utalii Karibu Kusini uliofanyika katika chuo cha ualimu Kreluu
mjini Iringa.
Kasesela
alisema kuwa mwaka 2018, maonesho ya Utalii Karibu Kusini yatafanyika katika
uwanja wa Kihesa Kilolo na kuvitaka vyuo vikuu kuwa na mabanda ya kudumu kama
taasisi za kitaaluma katika uwanja huo mpya. Alisema kuwa anatoa kipaombele kwa
vyuo vikuu kutokana na mchango wao mkubwa katika kukuza sekta ya utalii ndani
na nje ya wilaya ya Iringa.
“Wilaya ya Iringa tunajiandaa mwakani kuwapokea
kwa nguvu. Lengo letu katika maonesho ni kuwa namba moja au mbili baada ya
maonesho ya Dar es Salaam. Sisi tunataka kufanya maonesho si biashara”
alisema Kasesela.
Akiongelea
utofauti katika utalii na maeneo mengine, mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa
katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ndiyo hifadhi pekee utakayokuta wanyama wengi
wakubwa katika kundi moja. Hii inatofutisha na meneo mengine na kutengeneza
kivutio cha kipekee mtalii anapokuwa hifadhini.
Wakati
huohuo, mkuu wa wilaya ya Iringa aliitaka jamii kumlinda ndege Tumbusi ambaye
pia ni kivutio kizuri cha utalii wa ndege dhidi ya kutoweka kwake.
=30=
No comments:
Post a Comment