Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Iringa wameshauriwa kujiandaa mapema kabla ya kipindi cha kustaafu
kufika ili kuondokana na msongo wa mawazo baada ya kustaafu.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu
mstaafu Mkoa wa Iringa, Salum Maduhu wakati katika salamu zake za kuwaaga
watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika tafrija fupi ya kuwaaga watumishi
waliostaafu na kuhamia katika vituo vipya vya kazi iliyoandaliwa na Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum
Maduhu
Maduhu amesema “ndugu zangu
watumishi lazima mjiandae mapema msisubiri ubaki mwaka mmoja wa kabla ya
kustaafu ndiyo uanze kujiandaa anzeni mapema”. Amesema kuwa Serikali ni nzuri
sana na pia inazotaratibu nzuri kwa watumishi wake wanaostaafu kwa kuwaandalia
mafao yao baada ya muda wa utumishi wa Umma. Amesema pamoja na jambo hilo jema
bado suala la kujiandaa kustaafu linabaki kwa mtumishi mwenyewe.
Wakati huohuo suala la watumishi
kuongea elimu limefafanuliwa vizuri na aliyekuwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu,
Onoria Ambrose. Amesema “wafanyakazi msome, pale wafanyakazi mnaposoma hasa
wale wa kada za chini kipato kinaongezeka na pindi unapostaafu mafao nayo
yanaongezeka”. Aidha, amewataka wafanyakazi kujiunga na kikundi cha kusaidiana
na kukuza uchumi cha MSHIKAMANO kwa ajili ya kusaidiana.
Katika taarifa fupi ya Katibu Tawala
Mkoa wa Iringa, Bibi. Gertrude Mpaka amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
imeandaa tafrija fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu katika utumishi wa Umma
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwaaga watumishi waliohama na kuhamia vituo
vingine vya kazi.
Kwa upande wa watumishi wastaafu,
Mpaka amesema “ndugu wastaafu tumefanya kazi pamoja kwa muda mrefu sana, kwa upendo
na ushirikiano mkubwa na kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo na weledi
katika Utumishi wa Umma. Ushirikiano wenu ulisaidia Mkoa wetu kufanya kazi kwa
ufanisi mkubwa. Kwa msingi huo natumia fursa hii kuwashukuru kwa yale yote
mazuri na utumishi uliotukuka mliyoyafanya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa
kipindi chote tukiwa pamoja”.
Amesema
“Sote tunatambua kwamba ninyi mlikuwa kiungo muhimu katika kufanikisha shughuli
zote za Mkoa huu. Japo kuwa mmekwisha
kustaafu katika Utumishi wa Umma, bado ninyi ni nguzo muhimu sana katika
mafanikio ya Mkoa wetu, tunaomba daima tuendelee kuwatumia katika ushauri na
tunaamini kuwa ninyi ni hazina kubwa katika utendaji kazi kwa kuwa bado mnao
uzoefu mkubwa ambao unahitajika katika kuendeleza Mkoa wetu wa Iringa” amesisitiza
Mpaka.
Akiongelea
watumishi waliohama, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amewakumbusha kipindi
kilichopita cha utendaji kazi, na kusema “wote mtakumbuka kuwa katika kipindi
chote mkiwa Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, tulifanya kazi kwa
ushirikiano mkubwa kwa lengo la kuupa mafanikio Mkoa wetu. Mtakumbuka pia kuwa
kuna kipindi tulifanya kazi katika mazingira magumu yote ikiwa ni kuhakikisha
shughuli za Serikali zinaendelea na kufanikiwa”. Ametoa wito kwa wafanyakazi
hao kuwa nidhamu na uadilifu walivyokuwa navyo katika Mkoa wa Iringa
wakaviendeleze huko walipohamia na kuwa mfano wa kuigwa kwa watumishi wengine.
Watumishi
waliostaafu ni;
1.
|
Bibi. Zahara Kimela
|
Msaidizi Mtendaji Mkuu
|
2.
|
Bw. Esau Sigalla
|
Mchumi Mkuu
|
3.
|
Bw. Agapiti Msimbe
|
Mpima Ardhi Mkuu
|
4.
|
Bw. Stanley Munisi
|
Afisa Wanyamapori Mkuu I
|
5.
|
Bw. Robert Kinyunyu
|
Mlinzi Mkuu
|
6.
|
Bw. Salum Maduhu
|
Afisa Elimu Mkuu
|
7.
|
Bw. Ephraim Mdegela
|
Mlinzi Mwandamizi
|
8.
|
Bw. Cletus Karigo
|
Daktari wa Mifugo Mkuu
|
9.
|
Bw. Vicent James
|
Katibu Tawala
Msaidizi Miundo mbinu
|
10.
|
Bibi. Onoria Ambrose
|
Msaidizi wa Mtendaji Mkuu
|
Watumishi
waliohama ni;
1.
|
Bw. Barnabas Ndunguru
|
DAP, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
|
2.
|
Bw. Leornad Msigwa
|
Afisa Elimu Sekondari,
DED – Iringa
|
3.
|
Dkt. Ezekiel Mpuya
|
Mganga Mkuu wa Mkoa,
RAS Dodoma
|
4.
|
Bibi. Grace Manga
|
Mhasibu Daraja la II
RAS Morogoro
|