Sunday, November 11, 2012

MATUKIO YA KUKABIDHI KIKOMBE CHA MSHINDI WA PILI WANAWAKE KUVUTA KAMBA A

 Kombe la mshindi wa pili kuvuta kamba wanawake

 Nahodha wa timu Agnes Mlula akimkabidhi kombe mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka

 Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya Shimiwi Ras Iringa Gillian Bukori akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Mkoa mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka.





 Baadhi wa wachezaji wa timu hiyo ya kuvuta kamba wanawake




  




 Picha ya pajama baina ya wachezaji, viongozi wa Mkoa na mgeni rasmi.

Wakati wa Burudani



RAS IRINGA AKABIDHIWA KOKOMBE CHA SHIMIWI




Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Getrude K. Mpaka ameishauri Wizara ya Fedha kuangalia uwezekano wa kuongeza wigo wa fedha katika bajeti za Mikoa ili kuweza kuiwezesha mikoa kushiriki kikamilifu katika michezo ya shirikisho la michezo kwa Wizara na Idara za Serikli (SHIMIWI).

Ushauri huo ameutoa katika hafla fupi ya kukabidhiwa kikombe na kuipongeza timu ya kuvuta kamba wanawake ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka mshindi wa pili nyuma ya timu ya Ikulu kwa mchezo wa kuvuta kamba wanawake kutoka klabu ya Ras Iringa iliyoshiriki katika mashindano hayo mjini Morogoro.
 Nahodha wa timu Agnes Mlula (kulia) akimkabidhi kombe mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka

Mpaka amesema “ni vizuri Wizara ya Fedha iangalie jinsi ya kuongeza ceiling kwa Mikoa ili watumishi wetu waweze kushiriki kikamilifu kama watumishi wa timu za Wizara na kutokujiona ni wanyonge”. Amesema kuwa mwakani Ofisi yake itajipanga vizuri zaidi ili iweze kupeleka timu kubwa zaidi ya wachezaji wengi katika michezo tofauti tofauti. 

Ameitaka timu hiyo kutobweteka na kuendelea na mazoezi makali ili mwakani iweze kuibuka mshindi wa kwanza. Katika kufanikisha hilo amemuagiza Afisa Michezo Mkoa wa Iringa, Kenneth Komba kuhakikisha anaandaa mabonanza ya michezo mengi ili kuweza kupata wanamichezo mahiri watakaouletea Mkoa sifa kubwa zaidi.
Akielezea mafanikio ya timu hiyo Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu SHIMIWI RAS Iringa, Gillian Bukori amesema kuwa timu hiyo iliondoka Mkoani hapa tarehe 20/09/2012 baada ya kuagwa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa na kuitaka timu hiyo irudi na kikombe cha ushindi. 

Bukori amesema kuwa mafanikio hayo ni kutokana na ushiriki binafsi wa Katibu Tawala Mkoa, Getrude Mpaka, Uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi wote. Amesema kuwa ushindi huo umechangiwa na mshikamano, upendo na kujituma kwa mtu mmoja mmoja ndani ya timu. 

Amesema matarajio ya timu hiyo ni mwakani kuibuka na ushindi wa kwanza na kuutaka uongozi ulioingia madarakani awamu hii kuendeleza upendo na mshikamano ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika Mkoa.

Akitoa neno la shukrani, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa, Wamoja Ayubu amesema kuwa Mkoa utaendelea kuomba wigo kuongezwa katika bajeti ili kuiwezesha timu ya Mkoa kushiriki kikamilifu katika michezo hiyo. Amesema Mkoa utakuwa bega kwa bega na timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri katika mashindano hayo. 

Akiongelea mazoezi, Ayubu amesema kuwa mazoezi ni jambo la muhimu sana si kwa mwanamichezo tu, bali kwa kila mtumishi na wakati wote ni muafaka kwa kufanya mazoezi si mpaka wakati wa michezo pekee. 

Wamoja ambaye pia ni mchezi mahiri wa mchezo wa pete amesema kuwa ili timu hiyo iendelee kuwa juu suala la kujituma ni la muhimu sana.

Timu ya kuvuta kamba wanawake ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo kitaifa yaliyofanyika Morogoro ikiwa ni hatua nzuri zaidi ikilinganishwa na mwaka uliotangulia ilipoibuka mshindi wa nne.

 Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya Shimiwi Ras Iringa Gillian Bukori akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Mkoa mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka.




=30=