Tuesday, December 11, 2012



Text Box:             MAFUNZO HAMASA YA KIBIASHARA
NA
           UIMARISHAJI WA BIASHARA NDOGO

Walengwa:  Vijana waliomaliza vyuo/shule; Mtu yoyote anayependa
                   kujiajiri; Mfanyabishara anayemiliki biashara ndogo.
Aina ya Bidhaa
Idadi ya siku
Ada
Usindikaji chakula: Tomato sauce, Chilli sauce, Jam, Mbilimbi, Mangle pickle, Cakes/Snacks, Juice, Peanut butter, unga wa lishe
Siku 12
150,000/-
Sabuni za unga, vipande na maji [za harufu tofauti]
Siku 10
130,000
Utengenezaji wa Batiki
 Siku 12
120,000
Utengenezaji wa ‘Tie and dye’
Siku 6
80,000
Kutengeneza mishumaa ya aina na harufu mbalimbali
Siku 6
75,000
Ufugaji kuku wa kienyeji , mayai na wa nyama kibiashara
Siku 5
70,000
Bidhaa za mikono [urembo aina tofauti]
Siku 10
100,000
Wasiliana nasi simu Na. 0754 787 133   NA  0754 072 869

RC AKEMEA WIZI YA VIFAA VYA UJENZI




Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma amekemea vikali wizi wa vifaa katika ujenzi wa barabara unaoendelea katika maeneo mengi ya Mkoa wa Iringa na kuwataka wananchi kuimarisha ulinzi shirikishi na kuwabaini wale wote wanaohusika na uhalifu huo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Kauli hiyo ameitoka katika kijiji cha Nyang’oro kilichopo katika Wilaya ya Iringa alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma kwa kiwango cha lami na kuzungunza na wananchi wa maeneo yanayozunguka mradi huo.

Dkt. Christine amesema kuwa Serikali ya awamu ya nne inatengeneza barabara kwa fedha nyingi lengo likiwa ni kuharakisha kuwaletea maendeleo wananchi wake. Amesema kuwa jitihada hizo za Serikali zimekuwa zikikwamishwa na baadhi ya watu wasio na mapenzi mema na nchi niongoni mwao ni wananchi wanaozunguka ujenzi wa mradi huo wa barabara kwa kufanya vitendo vya wizi wa mafuta na vifaa mbalimbali vya ujenzi kama saruji. Amesema “wizi si kitu kizuri, wizi unaupa sifa mbaya mkoa wetu na nchi yetu, ninyi wezi mnaonisikia tafadhali acheni wizi huo mara moja” alisisitiza Dkt. Christine.

Amewataka wananchi kufanya mikutano ya kuwabaini wezi hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya dola na kusisitiza ulinzi shirikishi. Akionesha masikitiko yake na kwa ukali alisema kuwa kama watafumbia macho vitendo hivyo ni dhahiri kwamba ujenzi huo wa barabara utakapokamilika wezi hao watawaibia wananchi wenyewe.

Aidha, amewataka vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kwa ajili ya kufanya kazi za maendeleo. Amesema kwa kuwa mvua zinanyesha, ni vizuri vijana hao wakajikita katika kilimo.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa- Dodoma kwa kiwango cha lami (Km 260) Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Iringa, Mhandisi Bashiri Rwesingisa amesema kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB), Shirika la Misaada la Japan (JICA) na Serikali ya Tanznaia umetekelezwa kwa asilimia 35 na muda uliotumika ni miezi 16 sawa na asilimia 47 ya muda wote wa utekelezaji wa mradi huo na Mkandarasi yupo nyuma kwa miezi minne. Amesema ili kuongeza kasi ya utekelezaji, katika sehemu ya kwanza ya (Lot 1) Iringa- Migori (Km 95.2) Mkandarasi anatumia timu nne. Amezitaja timu hizo kuwa ya kwanza imeanzia Nyang’oro kuelekea Izazi, timu ya pili imeanzia Izazi kuelekea Migori, timu ya tatu inafanya kazi ya kupasua miamba eneo la mlima Nyang’oro wakati timu ya nne inafanya kazi kati ya Nyang’oro na Igingilanyi.

Sehemu ya pili (Lot 2) Migori- Fufu Escarpment (Km93.8) kiwango cha utekelezaji wake hadi Septemba, 2012 kilikuwa wastani wa asilimia 40 wakati muda uliotumika ni miezi 18 sawa na asilimia 50 na Mkandarasi yupo nyuma kwa miezi mitatu.

Aidha, Sehemu (Lot 3) Fufu Escarpment – Dodoma (Km 70.9), amesema kuwa sehemu hiyo inasimamiwa na Meneja wa Wakara wa barabara Mkoa wa Dodoma.
Akielezea changamoto katika mradi huo, Mhandisi Rwesingisa amesema kuwa wizi wa vifaa vya ujenzi kama mafuta na saruji umekuwa ukikwamisha maendeleo ya utekelezaji wa miradi kwa kuwa Makandarasi wamekuwa wakitumia muda mwingi kujaribu kupambana na wizi huo badala ya kutumia muda huo kufanya kazi za mradi. Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni migomo ya wafanyakazi wakidai nyongeza ya mishahara na posho. Nyingine ameitaja kuwa ni upasuaji wa miamba yam awe mlima Nyang’oro kwa ajili ya kupanua barabara umbali wa Km. 15 na ukosefu wa maji katika eneo hilo.
=30=