Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mafanikio
ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yamebadilisha fikra na kuongeza
ufanisi kwa watendaji wa sekta ya umma katika mikoa ya Iringa na Njombe katika
utekelezaji masuala ya ubia.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa
akiwasilisha taarifa fupi ya mafanikio ya SAGCOT kwa Mkoa wa Iringa wakati wa
ziara ya Katibu mkuu Ofisi ya waziri mkuu anayehusika na sera na mipango mkoani
Iringa jana.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu akisoma taarifa ya Mafanikio ya SAGCOT kwa Mkoa wa Iringa |
Ayubu
alisema “moja ya mafanikio ya ubia
uliyopo ni kubadilika kwa fikra na kuongezeka kwa ufanisi kwa watendaji wa
sekta ya umma katika utekelezaji wa masuala yanayohusu ubia na sekta binafsi”.
Alisema kuwa Mkoa uliweza kufuatilia changamoto mbalimbali na kufanikisha
upatikanaji wa umeme kwenye kiwanda cha kusindika nyanya kiitwacho Darch
Industries Ltd. Aliongeza kuwa upatikanaji wa barabara kutoka kiwanda hicho cha
kusindika nyanya hadi barabara kuu ya Iringa-Mbeya uliwezeshwa. “Upatikanaji wa maeneo kwenye vijiji
vinavyozalisha zao la nyanya kwa ajili ya kujenga vituo vya kukusanyia nyanya.
Vituo vinane vimejengwa na wabia wa kiwanada cha kusindika nyanya” alisema
Ayubu.
Katibu
Tawala Mkoa alizitaja juhudi zilizofanywa na Mkoa kuwa ni pamoja na kutatua
mgogoro wa matumzi ya maji kati ya muwekezaji (Silverlands) na wananchi ambapo
hati ya makubaliano ya matumizi ya maji ilisainiwa na pande zote mbili. Pia, Mkoa
umefanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika kiwanda cha kusindika chai
cha Unilever.
Kongani
ya Ihemi (Iringa na Njombe) inajumuisha wilaya za Iringa, Kilolo, Mufindi,
Njombe na Wanging’ombe ilianza utekelezaji chini ya mpango wa SAGCOT mwaka 2015
ikiwa ya kwanza kati ya kongani sita za SAGCOT.
=30=