Wednesday, June 25, 2014
IRINGA DC YAKOPESHA VIJANA MIL 34
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Halmashauri
ya wilaya ya Iringa imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 34 kwa ajili ya
kuviwezesha vikundi vya vijana vinavyojihusisha na ujasiliamali ili kuongeza
mtaji na kujiletea maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba katika risala
ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyosomwa na Afisa Utumishi Mkuu wakati
wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Iringa iliyosomwa katika eneo la Isimani
tarafani wilayani Iringa.
Dkt.
Warioba amesema “katika kipindi cha mwaka 2013/2014 halmashauri ya wilaya
imetoa mikopo yenye jumla ya shilingi 34,500,000 kwa vikundi 18 vya
ujasiliamali vya vijana”. Amesema kuwa halmashauri hiyo ina vikundi 177 vya
vijana vyenye jumla ya wanachama 1,358 kati yao wanaume 825 na wanawake 531.
Akiongelea
mikopo kwa vikundi vya wanawake, mkuu wa wilaya ya Iringa amesema “katika
kipindi cha mwaka 2013/2014 halmashauri imetoa mikopo yenye jumla ya shilingi
74,950,000 kwa vikundi 50 vya ujasiliamali vya wanawake.
Kuhusu
ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, mkuu wa wilaya amesema kuwa ujumbe uliobebwa mwaka
huu 2014 “katiba ni sheria kuu ya nchi” chini ya kauli mbiu isemayo ‘jitokeze
kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.
Amesema
kuwa katika kutekeleza ujumbe huo wananchi na viongozi wa serikali, vyama vya
siasa na madhehebu ya dini wameshiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata
katiba mpya kwa kupiga kura ya maoni kupitia mabaraza ya katiba yaliyoundwa
katika halmashauri ya wilaya ya Iringa. Amesema kuwa wananchi wote walishiriki kikamilifu
katika mchakato wa kupata katiba mpya. Amesema kuwa pamoja na wananchi
kushiriki kupitia makundi mbalimbali serikali imeendelea kuwahimiza wananchi
kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura ya maoni ili kupata katiba mpya.
=30=
KILOLO YAKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA NA RUSHWA
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- KILOLO
Wilaya
ya kilolo imeendelea kukabiliana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya na
rushwa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya na maisha bora.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya kilolo Gerald Guninita katika risala ya
utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete iliyosomwa
na Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo, Yusuph Msawanga mjini Kilolo.
Gininita
amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni moja kati ya changamoto
zinazolikabili taifa katika kipindi hiki. Amesema kuwa wilaya ya Kilolo katika
kupambana na dawa za kulevya inatekeleza kaulimbiu isemayo “furahia afya siyo
dawa za kulevya”. Amesema kuwa wananchi wamekuwa wakielimishwa kwa njia
mtambuka athari za dawa za kulevya kiafya, kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa
wilaya yake imeemdela kufanya uhamasishaji kwa vijana kuanzisha shughuli za
kiuchumi.
Akiongelea
mapambano dhidi ya rushwa, Guninita amesema kuwa wilaya ya Kilolo kwa
kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatekeleza
kaulimbiu isemayo “palipo na rushwa hakuna maendeleo”. Utekelezaji huo ameutaja
kuwa ni kutoa elimu kwa umma pamoja na kuzindua club za wapinga rushwa katika
shule za sekondari (33) na shule za msingi (15). Mkakati mweingine ameutaja
kuwa ni kufanya tafiti ndogo ndogo zenye matokeo ya haraka katika kutambua
mianya ya rushwa ili zisaidie kukabiliana na tatizo la rushwa. Ameutaja mkakati
mwingine kuwa ni kupokea taarifa za malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa na
kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria.
=30=
MWENGE KUTEKELEZA MIRADI YA BIL. 3.1
Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mwenge
wa Uhuru kutekeleza miradi ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi bilioni 3.1
katika siku nne za kukimbizwa kwake mkoani Iringa.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma
alipowasilisha taarifa ya mkoa wa Iringa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Morogoro leo.
Dkt.
Ishengoma amesema Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa utaweka mawe ya msingi,
utakagua, utazindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 42 yote ikiwa na
thamani ya shillingi 3,109,958,020”.
Amesema kuwa kati ya fedha hizo serikali kuu imechangia shilingi 1,329,471,899, halmashauri za
wilaya na manispaa shilingi 946,005,221. Amesema kuwa michango
ya wananchi ni shilingi 500,877,000 na shilingi 333,603,900 ni michango ya wadau wa maendeleo.
Amesema
kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Iringa utakimbizwa katika halmashauri nne za
Kilolo, Iringa, Manispaa ya Iringa na Mufindi. Amesema kuwa Mwenge huo
utakimbizwa umbali wa kilometa 1,159 na kukabidhiwa mkoani Njombe tarehe 28
Juni, 2014.
Akiongelea
ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2014, Dkt. Ishengoma ameutaja ujumbe huo kuwa
ni “katiba ni sheria kuu ya nchi” wenye kaulimbiu ‘jitokeze kupiga kura ya
maoni tupate katiba mpya’.
Akiongelea mchanganuo wa miradi hiyo, mkuu wa mkoa wa
Iringa amesema kuwa jumla ya miradi 10 itafunguliwa, miradi 16 itazinduliwa,
miradi 7 itawekwa mawe ya msingi na miradi 9 itakaguliwa. Ameitaja miradi hiyo kuwa
inatokana na sekta za kilimo, ufugaji, maji, maliasili, ujenzi na barabara, afya,
elimu na maendeleo ya jamii.
=30=
IRINGA WATAKIWA KUJITOKEZA KUUPOKEA MWENGE
Na. Dajali Mgidange, IRINGA
Wananchi
wametakiwa kujitokeza kwa winngi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo
mbalimbali utakayokimbizwa mkoani Iringa.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa
Uhuru mkoani Iringa mwaka 2014 ofisini kwake leo.
Dkt.
Ishengoma amesema kuwa ni vizuri wananchi wakajitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge
wa Uhuru pindi utakapopita katika maeneo yao. Amesema “ninawasihi wananchi
kuendela kudumisha amani na utulivu wakati wote ambapo Mwenge wa Uhuru utakuwa
ukikimbizwa katika mkoa wetu na hata baada ya kuhitimisha mbio hizo katika mkoa
wetu”.
Akiongelea
uhamasishaji katika halmashauri, Mkuu wa Mkoa amesema “ninapenda kutumia fursa
hii kuviomba vyombo vya habari na ninyi waandishi wa habari kuwahamasishwa
wananchi katika halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kuulaki
Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki katika mikesha ya
Mwenge pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2014”.
Amesema
kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Iringa utakagua, kuweka mawe ya
msingi, kufungua na kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo 42 yenye thamani ya
Tsh. 3,109,958,020/=. Amesema kuwa Mwenge
wa Uhuru utatoa ujumbe katika maeneo yote ambako utakimbizwa. Ameitaja miradi itakayotembelewa
na Mwenge wa Uhuru kuwa ni miradi ya barabara, elimu, afya, kilimo na ufugaji.
Miradi mengine ameitaja kuwa ni miradi ya vijana na wanawake na hifadhi ya
mazingira.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2014 unaongozwa na ujumbe usemao “katiba ni sheria kuu ya nchi’’
wenye kauli mbiu isemayo ’ jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.
=30=
Subscribe to:
Posts (Atom)