Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mwenge
wa Uhuru kutekeleza miradi ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi bilioni 3.1
katika siku nne za kukimbizwa kwake mkoani Iringa.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma
alipowasilisha taarifa ya mkoa wa Iringa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Morogoro leo.
Dkt.
Ishengoma amesema Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa utaweka mawe ya msingi,
utakagua, utazindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 42 yote ikiwa na
thamani ya shillingi 3,109,958,020”.
Amesema kuwa kati ya fedha hizo serikali kuu imechangia shilingi 1,329,471,899, halmashauri za
wilaya na manispaa shilingi 946,005,221. Amesema kuwa michango
ya wananchi ni shilingi 500,877,000 na shilingi 333,603,900 ni michango ya wadau wa maendeleo.
Amesema
kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Iringa utakimbizwa katika halmashauri nne za
Kilolo, Iringa, Manispaa ya Iringa na Mufindi. Amesema kuwa Mwenge huo
utakimbizwa umbali wa kilometa 1,159 na kukabidhiwa mkoani Njombe tarehe 28
Juni, 2014.
Akiongelea
ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2014, Dkt. Ishengoma ameutaja ujumbe huo kuwa
ni “katiba ni sheria kuu ya nchi” wenye kaulimbiu ‘jitokeze kupiga kura ya
maoni tupate katiba mpya’.
Akiongelea mchanganuo wa miradi hiyo, mkuu wa mkoa wa
Iringa amesema kuwa jumla ya miradi 10 itafunguliwa, miradi 16 itazinduliwa,
miradi 7 itawekwa mawe ya msingi na miradi 9 itakaguliwa. Ameitaja miradi hiyo kuwa
inatokana na sekta za kilimo, ufugaji, maji, maliasili, ujenzi na barabara, afya,
elimu na maendeleo ya jamii.
=30=
No comments:
Post a Comment