Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- KILOLO
Wilaya
ya kilolo imeendelea kukabiliana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya na
rushwa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya na maisha bora.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya kilolo Gerald Guninita katika risala ya
utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete iliyosomwa
na Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo, Yusuph Msawanga mjini Kilolo.
Gininita
amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni moja kati ya changamoto
zinazolikabili taifa katika kipindi hiki. Amesema kuwa wilaya ya Kilolo katika
kupambana na dawa za kulevya inatekeleza kaulimbiu isemayo “furahia afya siyo
dawa za kulevya”. Amesema kuwa wananchi wamekuwa wakielimishwa kwa njia
mtambuka athari za dawa za kulevya kiafya, kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa
wilaya yake imeemdela kufanya uhamasishaji kwa vijana kuanzisha shughuli za
kiuchumi.
Akiongelea
mapambano dhidi ya rushwa, Guninita amesema kuwa wilaya ya Kilolo kwa
kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatekeleza
kaulimbiu isemayo “palipo na rushwa hakuna maendeleo”. Utekelezaji huo ameutaja
kuwa ni kutoa elimu kwa umma pamoja na kuzindua club za wapinga rushwa katika
shule za sekondari (33) na shule za msingi (15). Mkakati mweingine ameutaja
kuwa ni kufanya tafiti ndogo ndogo zenye matokeo ya haraka katika kutambua
mianya ya rushwa ili zisaidie kukabiliana na tatizo la rushwa. Ameutaja mkakati
mwingine kuwa ni kupokea taarifa za malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa na
kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria.
=30=
No comments:
Post a Comment