Na. Dajali Mgidange, IRINGA
Wananchi
wametakiwa kujitokeza kwa winngi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo
mbalimbali utakayokimbizwa mkoani Iringa.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa
Uhuru mkoani Iringa mwaka 2014 ofisini kwake leo.
Dkt.
Ishengoma amesema kuwa ni vizuri wananchi wakajitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge
wa Uhuru pindi utakapopita katika maeneo yao. Amesema “ninawasihi wananchi
kuendela kudumisha amani na utulivu wakati wote ambapo Mwenge wa Uhuru utakuwa
ukikimbizwa katika mkoa wetu na hata baada ya kuhitimisha mbio hizo katika mkoa
wetu”.
Akiongelea
uhamasishaji katika halmashauri, Mkuu wa Mkoa amesema “ninapenda kutumia fursa
hii kuviomba vyombo vya habari na ninyi waandishi wa habari kuwahamasishwa
wananchi katika halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kuulaki
Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki katika mikesha ya
Mwenge pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2014”.
Amesema
kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Iringa utakagua, kuweka mawe ya
msingi, kufungua na kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo 42 yenye thamani ya
Tsh. 3,109,958,020/=. Amesema kuwa Mwenge
wa Uhuru utatoa ujumbe katika maeneo yote ambako utakimbizwa. Ameitaja miradi itakayotembelewa
na Mwenge wa Uhuru kuwa ni miradi ya barabara, elimu, afya, kilimo na ufugaji.
Miradi mengine ameitaja kuwa ni miradi ya vijana na wanawake na hifadhi ya
mazingira.
Mwenge
wa Uhuru mwaka 2014 unaongozwa na ujumbe usemao “katiba ni sheria kuu ya nchi’’
wenye kauli mbiu isemayo ’ jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.
=30=
No comments:
Post a Comment