Tuesday, January 7, 2014
SERIKALI IONGEZE SHULE ZA VIPAJI MAALUM
Serikali
imeshauriwa kuandaa mkakati wa kitaifa wa kuongeza idadi ya shule za sekondari
za bweni na vipaji maalum kutokana na idad ya wanafunzi kufaulu na kupanda kila
mwaka ili kuwatendea haki na kulinda vipaji vya watoto.
Ushauri huo
umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bibi. Evarista Kalalu wakati akichangia
katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza kwa
mkoa wa Iringa kilchofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
Bibi. Kalalu
amesema ufaulu wa wanafunzi unapanda na kuongezeka lakini sekondari za bweni na
vipaji maalum haziongezeki jambo linalosababisha kutokuwatendea haki wanafunzi
wengi waliofaulu vizuri kukosa nafasi katika shule hizo. Ameshauri kuwa uwepo
mkakati wa kitaifa wa kuongeza shule za bweni na vipaji maalum ili kuwapatia
fursa watoto wengi zaidi.
Wakati huohuo,
Mbunge wa Mufindi Kusini, Bw. Menrad Kigola ameshauli viwepo vyuo vikuu vya
vipaji maalum nchini ili kulinda vipaji vya wanafunzi wanaomaliza shule za
sekondari. “Tunazo shule za sekondari za vipaji maalum chakushangaza watoto
wetu wanapomaliza sekondari wanajiunga na vyuo vikuu vya kawaida jambo
linalochangia kupoteza vipaji vya watoto wetu. Umefika wakati wa serikali kuwa
na vyuo vikuu vya vipaji maalum ili kulnda na kuendeleza vipaji vya watoto
wetu” amesisitiza Bw. Kigola.
Akifunga kikao
hicho, Mwenyekiti wa kikao hicho ambae pia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Iringa, Bibi. Wamoja Ayubu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha
wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti na kuanza masomo shule
zitakapofunguliwa. Aidha, amewataka kuhakikisha vikao vya tathmini ya elimu na
kuzipongeza shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
mwaka 2013.
Bibi. Ayubu
amewata kuweka mikakati endelevu ili mwaka 2014 Mkoa wa Iringa ufikie asilimia
70 ambalo ni lengo la Matokeo Makubwa Sasa kwa mwaka huo. Vilevile, amewataka
kuhakikisha Kata ambazo zimechukua wanafunzi wengi zaidi kuliko uwezo wa vyumba
vya madarasa vilivyopo, kuhakikisha madarasa yanajengwa haraka ili kukidhi
idadi ya wanafunzi stahili. Katika kuendeleza ubora wa elimu mkoani, Kaimu
Katibu Tawala Mkoa amewataka wakurugenzi kuhakikisha usimamizi na ufuatiliaji
unakuwa wa karibu zaidi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara shuleni ili kuondoa
tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
=30=
HALMASHAURI ZA MKOA WA IRINGA ZAPONGEZWA KUVULA MALENGO YA BRN
Halmashauri za
Mkoa wa Iringa zimepongezwa kwa kazi nzuri katika sekta ya elimu hadi
kufanikisha kuvuka lengo la Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kuuwezesha Mkoa
kushika nafasi ya tatu kitaifa katika Mtihani wa darasa la saba kitaifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wanafunzi wa kujunga na kidato
cha kwanza Mkoa wa Iringa, Bibi. Wamoja Ayubu katika hotuba yake ya ufunguzi wa
kikao cha Kamati ya Uchaguzi wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
2013 Mkoa wa Iringa kilchofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini
Iringa.
Bibi. Ayubu
amesema “kiwango cha ufaulu ni kizuri sana na Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya
tatu kati ya mikoa 25 ya Tanzania bara. Pia kiwango cha ufaulu kimepanda kwa
Halmashauri zote. Kwa hiyo, nachukua nasafi hii kuzipongeza Halamshauri zote
kwa kuvuka lengo la matokeo makubwa sasa ambalo ni asilimia 60 kwa mwaka 2013”.
Akiwasilisha
taarifa ya mwelekeo wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka
2013 Mkoa wa Irnga, Afsa Elimu Mkoa wa Iringa, Mwalimu Joseph Mnyikambi amesema
kuwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika tarehe 11-12 Septemba,
2013. Amesema kuwa shule za msingi 449 kati ya shule 482 ndizo likukuwa na
watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Akiongelea
mahudhurio siku za mitihani, Mwalimu Mnyikambi amesema kuwa mahudhurio
yameongezeka kutoka asilimia 98.3 ya mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 99 mwaka
2013 likiwa ni ongezeko la asilimia 0.7. Amesema kuwa kiwango cha kumaliza
elimu ya msingi kimeongezeka kutoka asilimia 82 (2012) hadi kufikia asilimia 84
(2013) likiwa ni ongezeko la asilimia 2. Aidha, wanafunzi ambao hawakufanya
mtihani mwaka 2013 ni asilimia 1 ukilinganisha na asilimia 1.2 mwaka 2012
kutokana na sababu za utoro, vifo, ugonjwa na mimba.
Akiongelea hali
ya ufaulu kwa kila Halmashauri katika Mkoa wa Iringa, Afisa Elimu Mkoa amesema
kuwa Iringa Manispaa asilimia 81.9 (1), Mufindi asilimia 63.9 (2), Iringa
asilimia 62.2 (3) na Kilolo asilimia 60.3 (4).
Amezitaja shule
10 bora katika Mkoa wa Iringa kuwa ni Sipto (1), Ummu Salaama (2), Ukombozi
(3), St. Dominic Savio (4), Star (5),
Wilolesi (6), St. Charles (7) zote za Manispaa ya Iringa. Nyingine ni Brooke
Bond (8), Southern Highland (9) Mufindi na Mapinduzi (10) Manispaa ya Iringa.
=30=
Subscribe to:
Posts (Atom)