UBALOZI
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WASHINGTON D.C.
UNAWALETEA
SIKU YA MTANZANIA
Mahali: Tanzania House, 1232 22Nd Street, N.W. Washington
D.C.; 20037 Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012 Kiingilio: BURE Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12
Jioni)
Ubalozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C.
unawakaribisha Watanzania wote waishio
maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji
vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo Watanzania watashiriki kwenye
kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (Wamarekani
na wa Mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.
Madhumuni
makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa
Marekani kuhusu Tanzania.
Pili kuitangaza zaidi Tanzania
kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania. Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na huduma
zitolewazo na Watanzania waishio hapa Marekani.
Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa
mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni), vikundi vya ngoma, muziki,
mitindo, na Watanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia
tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.
Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea
kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:
Dkt. Switbert Mkama 202 884 1087 au
barua pepe smkama@tanzaniaembassy-us.org
Asia Dachi 202 884 1096 barua pepe adachi@tanzaniaembassy-us.org
Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.
Karibuni Wote.