Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa barabara ya Iringa –Dodoma
itakapokamilika itasaidia kuinua uchumi wa mkoa wa Iringa na maeneo ya jirani
na kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanaitunza ili iweze kudumu kwa muda
mrefu.
Kauli hiyo ameitoa leo mchana katika hotuba yake muda mfupi
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara
ya Iringa-Dodoma Km 260 kwa kiwango cha lami katika eneo la Migoli.
Dkt. Kikwete amesema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia
kuinua uchumi wa mikoa ya Iringa na Dododma na maeneo ya jirani kutokana na
kuwa itafungia milango ya kibiashara kwa kurahisisha usafiri kwa abilia na
usafirishaji wa mizigo. Akiongelea jukumu la wananchi katika kunufaika vizuri
na ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, Rais Kikwete amewataka
wananchi hao kijipanga katika kuongeza uzalishaji mali na kutumia vizuri fursa
zilizopo ili kunufaika kiuchumi.
Rais Kikwete amesema pamoja na minong’ono iliyopo kwa Serikali
yake inatumia fedha nyingi sana klatika ujenzi wa barabara badala ya kupeleka
fedha hizo katika maeneo mengine, amesema kuwa “kama taifa tumechelewa sana
kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara”. Amesema kuwa huo ni uamuzi
wa makusudi wa kuwekeza kwa kasi katika miundombinu ya barabara ili kuweza
kufungua fursa nyingine nyingi. Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuunganisha
kwa lami mtandao wa barabara zote nchini.
Rais Dkt. Kikwete amekemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi
kuiba mafuta na vifaa mbalimbali katika miradi ya ujenzi wa barabara. Amesema
kuwa wizi huo umekuwa ukirudisha nyuma muda wa utekelezaji na ukamilishaji wa
miradi ya ujenzi wa barabara nchini. Amewataka wananchi kuwa walinzi dhidi ya
wizi wa vifaa hivyo vya ujenzi na mafuta ili kuharakisha ujenzi ujenzi na
ukamilishaji wa miradi hiyo.
Akimkaribisha Rais Kikwete kuhutubia, Waziri wa Ujenzi, Dkt.
John Magufuli amepongeza mahusiano mazuri yanayofanywa na Rais Kikwete kwa
wadau mbalimbali wa maendeleo jambo linalowezesha ujenzi wa mirandi mingi ya
barabara nchini.
Dkt Magufuli ameseam kuwa mradi uliowekwa jiwe la msingi
Iringa-Migori- Fufu Escarpment Km 189 unagharimu zaidi ya Tshs. Bilioni 164.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipokea maelekezo ya mradi
Akiongelea umakini katika kusimamia miradi ya ujenzi, Waziri wa
Ujenzi amesema “Mkandarasi atakayezembea tutamfukuza” na msimamizi mshauri
atakayeshindwa kuongoza atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
=30=