Wednesday, September 7, 2011

SHEREHE YA HARUSI YA BW N BIBI. SAMWELI S. NYAGAWA

 Wenyewe sasa Bw n Bibi. Samweli S. Nyagawa wakiingia ukumbini

Keki ya uhakika shukrani kwa mpambaji 

Mama Harry...! Mama Harry...! Mama Harry...! 

Mwenyewe Neema G. Mwaipopo kama sio wa nchi hii vile!

Bw na Bibi. Jonas Kilima na mtoto wao wakiwa katika tabasamu ukumbini 

Mr n Mrs. Dr. E. Mpuya ambaye pia ni Mkuu wa Kazi wa Bw. Samwel Nyagawa 

Mama Chota na ujumbe wake katika ukumbi wa RUCO kushuhudia sherehe ya harusi ya Sam 


Familia ya Mama Mdemu ikiingia ukumbini 

Mr n Mrs. Prof. S. Nyagawa wakiingia ukumbi wa chuo cha RUCO katika sherehe ya harusi ya kijana wao wa mwisho Samwel Nyagawa 

Bibi. Modesta Kaweni na Bibi Kiula katika sherehe ya harusi ya Sam

Bibi. Kiula, Bibi. Ambrose na Bibi. Chambala wamejiachia katika sherehe ya Harusi ya kijana wao Samwel S. Nyagawa 

Mr n Mrs. Bahati F. Golyama wakijinafasi katika sherehe ya Harusi ya Bw n Bibi. Samwel S. Nyagawa
WAZAZI WASHAURIWA KUTOINGILIA NDOA ZA WATOTO WAO
Wazazi wametakiwa kutoingilia NDOA za watoto wao na kushauriwa kuwaacha wastarehe katika NDOA zao kwa sababu kuwaingilia watoto katika ndoa zao ni kinyume na mpango wa MUNGU na ni chanzo cha mafarakano katika NDOA.

Ushauri huo ulitolewa na Baba Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Iringa, Askofu Jonas Mkane katika nenolake lililotangulia ufungishaji wa NDOA TAKATIFU kati ya Samwel S. Nyagawa na Catherine W. Mdemu.
 Samwel S. Nyagawa akimvisha PETE YA NDOA TAKATIFU Catherine W. Mdemu

Askofu Mkane amesema kuwa baadhi ya NDOA zimekuwa zikivunjika kutokana na wazazi kuingilia ndoa za watoto wao na kusisitiza kuwa ni jambo la aibu kwa wazazi hao kuhusika katika kuharibu NDOA za watoto wao.

Amesema kwa kuwa Samwel ameamua kumuoa Catherine, tendo hilo maana yake ni Dunia mzima hakuna tena mwanamke anayeweza kuwa mke wa Samwel na kusisitiza kuwa NDOA ni utawala Mtakatifu.

Askofu Mkane amesema kuwa mwanzilishi wa Taasisi hiyo (NDOA) ni MUNGU mwenyewe pale Bustani ya Eden aliposema “si vema mtu huyu akawa peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufa-nana naye”.
Amesema kazi kubwa na msingi aliyonayo na anayowajibika kwayo Catherine kwa Samwel ni UTII wakati kwa Samwel yeye ni KUMPENDA Catherine na hayo ndiyo maisha ya NDOA.

Akiongelea changamoto katika NDOA amewataka maharusi hao kutotarajia mteremko katika maisha ha ohayo mapya na kusisitiza kwa mujibu wa maandiko yanavyosema “wanaume kaeni na wake zenu kwa akili…”.

Mwisho Baba Askofu amewashauri kuweka pamoja rasilimali zao na kupanga mipango yao ya kimaisha pamoja ili kufikia mafanikio ya pamoja haraka.

Katika muda wote wa ibada hiyo ya NDOA TAKATIFU maharusi hao walionekana wenye utulivu mkubwa mbele za MUNGU huku wakianikizwa na tabasamu na bashasha za haja wakati nyuso zao zikitawaliwa na furaha isiyo kifani na dim-pose zisizojificha. 
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe bab kubwa ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha RUCO.
                                                                                                                       

NDOA YA SAMWEL S. NYAGAWA NA CATHERINE W. MDEMU ILIVYOACHA HISHORIA

Nae Catherine W. Mdemu akasaini cheti cha ndoa yake.  

Hapa Samwel S. Nyagawa anaondoa ule ubishi wa kama umeoa tuoneshe cheti cha ndoa kwa kusaini cheti cha ndoa yake huku Catherine akihakiki saini inayotelewa..sasa watu wanajiuliza kwani alishaiona saini ya Sam?? 

Catherine W. Mdemu nae akamvisha PETE ya Ndoa Samwel S. Nyagawa. Sasa hebu mwangalie Catherine hapa...!! 

 Wakati wa Samwel S. Nyagawa kumvisha PETE ya Ndoa Catherine W. Mdemu ukawadia na tendo hilo likafanyika kwa ustadi mkubwa yaani kama wanataniana vile!

Sikiliza maneno hayo ya maharusi  

Unaweza kudhani Sam anasinzia eeh! hata mie nilidhani hivyo

Huku akijiamini Samwel S. Nyagawa nae aliutamkia Umma kuwa anamuoa Catherine W. Mdemu

Ulifika wakati wa Catherine W. Mdemu kuutamkia Umma kuwa anakubali kuolewa na Samwel. S. Nyagawa 

Tabasamu la Samwel S. Nyagawa asikwambie mtu, hilo pozi la Catherine W. Mdemu usilihoji

Maharusi Samwel S. Nyagawa na Catherine W. Mdemu (katikati) wakiwa na wapambe wao (pembeni)

Baba Askofu Jonas Mkane akiongoza sala ya Misa ya Ndoa ya Bw. Samwel S. Nyagawa na Bi. Catherine W. Mdemu  

 Maharusi Samwel s. Nyagawa na Catherine W. Mdemu wakiwa kanisani 

Maharusi Samwel s. Nyagawa na Catherine W. Mdemu wakiingia katika nyumba ya Ibada 

Mama mzazi wa Samwel Nyagawa, Mama Prof. Nyagawa (kushoto) na mama ambaye jina lake halikujulikana kwa mara moja wakiwa kanisani 


Maharusi Samwel S. Nyagawa na Mpambe wake wakiingia Kanisani

Maharusi Samwel S. Nyagawa na mpambe wake wakiingia Kanisani