Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
imeweka mkakati wa kuimarisha mazingira mazuri kwa wafanyakazi wake hasa wanaofanya
kazi pembezoni ili kuongeza ari na ufanisi wa kazi.
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dkt. Christine Ishengoma (watatu kushoto) akitoa maelekezo katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo (kushoto) akifafanua jambo mbele ya kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Kauli hiyo imetolewa na Afisa
Utumishi, Robin Gama alipokuwa akijibu swali kutoka kwa wananchi waliotembelea
banda la Halmashauri hiyo na kuhoji ushiriki wa Idara ya Utumishi katika
maonesho ya Nanenane mwaka 2013 tofauti na miaka mingine.
Gama amesema kuwa Idara ya Utumishi
ndiyo inayoajiri na kupanga maeneo ya kufanyia kazi kwa mujibu wa mahitaji
hivyo ushiriki wake katika maoensho hayo ni wa kimkakati kuja kuangalia matunda
halisi ya watumishi wetu. Amesema kuwa mtumishi anapofanya kazi vizuri hupewa
motisha na anapofanya vibaya tofauti na kanuni na taratibu za utumishi wa umma
huwajibishwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.
Akiongelea changamoto ya watumishi
kutopenda kukaa na kufanya kazi maeneo ya pembezoni, Gama amesema kuwa katika
kukabiliana na changamoto hiyo, Halmashauri ya wilaya ya Iringa, kupitia Idara
ya Utumishi imekuwa ikiwapatia motisha ikiwa ni pamoja na kuwapa vipaombele na
vivutio kadhaa ili wabaki na kupenda mazingira ya kazi. Amevitaja vivutio hivyo
kuwa ni pamoja na mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vya
usafiri na mafuta.
Afisa Utumishi amesema kuwa Idara ya
utumishi ndiyo mfano hivyo ikifanya vizuri, watumishi wote watafanya vizuri na
wananchi kunufaika na huduma zitolewazo na Serikali. Amesmea kuwa katika
kutekleleza hilo, halmashauri yake imekuwa ikiishirikisha jamii katika kuibua
na kuandaa mipango ya maendeleo katika vijiji.
Gama amewsema kuwa dhana ya maonesho
ya Nanenane kwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa ni mafanikio makubwa na mazuri
kwa wakulima yanategemea ushauri mzuri kutoka kwa wataalamu wa ugani wa kilimo,
mifugo na ushirikika waliopata mafunzo, wenye uzoefu, ubunifu na utendaji kazi
mzuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa
mufibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 ina watu 254,032 kati yao
wanawake ni 130,789 na wanaume 123,243. Tarafa 6, Kata 25, vijiji 123 na
vitongoji 716. Aidha, Halmashauri ina Idara 13 na vitengo 6.
=30=