Sunday, October 1, 2017

VYUO VIKUU IRINGA KUJENGA MABANDA YA KUDUMU KIHESA-KILOLO



Na Mwandishi Maalum, IRINGA
Vyuo vikuu wilayani Iringa vimetakiwa kujipanga kuwa na mabanda ya kudumu katika maonesho ya Utalii Karibu Kusini mwaka 2018.

Rai hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika salamu zake kwenye usiku wa Utalii Karibu Kusini uliofanyika katika chuo cha ualimu Kreluu mjini Iringa.

Kasesela alisema kuwa mwaka 2018, maonesho ya Utalii Karibu Kusini yatafanyika katika uwanja wa Kihesa Kilolo na kuvitaka vyuo vikuu kuwa na mabanda ya kudumu kama taasisi za kitaaluma katika uwanja huo mpya. Alisema kuwa anatoa kipaombele kwa vyuo vikuu kutokana na mchango wao mkubwa katika kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya wilaya ya Iringa.

Wilaya ya Iringa tunajiandaa mwakani kuwapokea kwa nguvu. Lengo letu katika maonesho ni kuwa namba moja au mbili baada ya maonesho ya Dar es Salaam. Sisi tunataka kufanya maonesho si biashara” alisema Kasesela.

Akiongelea utofauti katika utalii na maeneo mengine, mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ndiyo hifadhi pekee utakayokuta wanyama wengi wakubwa katika kundi moja. Hii inatofutisha na meneo mengine na kutengeneza kivutio cha kipekee mtalii anapokuwa hifadhini.

Wakati huohuo, mkuu wa wilaya ya Iringa aliitaka jamii kumlinda ndege Tumbusi ambaye pia ni kivutio kizuri cha utalii wa ndege dhidi ya kutoweka kwake.
=30=    

No comments:

Post a Comment