Timu ya kuvuta kamba ya RAS Iringa wanawake imeishinda timu ya
kuvuta kamba ya MUHAS wanawake kwa mivuto 2-0. Katika mvutano wa aina yake
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege na kushuhudiwa na mamia
ya wapenda michezo wa mkoa wa Iringa na wageni kutoka sehemu mbalimbali
waliofika mkoani hapa kwa ajili ya sherehe za Mei Mosi, 2018.
Akiongea baada ya mvutano huo, Mratibu wa timu zote za RAS
Iringa, Issa Matea alisema kuwa timu ya RAS Iringa maarufu kama Kisiki imepata ushindi huo kutokana na
mshikamano na kujituma. Alitoa rai kwa timu washindani kuwa chonjo kwa sababu
timu hiyo inalojukumu moja tu katika michezo hiyo.
Alilitaja jukumu hilo kuwa
ni kulinda heshima ya mkoa wa Iringa kwa kuibuka na ushindi katika mivuto yote
katika michezo ya Mei Mosi, 2018.
=30=
No comments:
Post a Comment