Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Saratani
ya mlango wa kizazi imekuwa ikichangiwa na kujamiiana katika umri mdogo na kuwa
na wapenzi wengi na kusababisha vifo vya wanawake wengi mkoani Iringa.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua
mkutano wa wadau wa mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu huria jana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza |
Masenza
alisema kuwa saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na mambo mengi. “Saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na
vitu vingi ikiwemo kuanza kujamiana katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi,
kuwa na ndoa za mitala, kuzaa watoto wengi, na uvutaji wa sigara” alisema
Masenza.
Akiongelea
dalili za saratani hiyo, alisema kuwa mara nyingi hujitokeza ikiwa imeshasambaa
mwilini. Dalili hizo alizitaja kuwa ni kutokwa damu
ya hedhi bila mpangilio pamoja na kutokwa damu baada ya kujamiana. Nyingine
alizitaja kuwa ni maumivu ya mgongo, miguu na kiuno. Nyingine ni kuchoka,
kupungua uzito, kupungukiwa au kokosa hamu ya kula, kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au
wenye damu kwenye uke, maumivu ya miguu au kuvimba.
“Dalili mbaya zaidi zinazoweza
kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na
fistula, na uvimbe wa tezi” alisisitiza Masenza.
Mkuu wa mkoa wa Iringa alielezea mkakati utakaotumika katika
utoaji chanjo hiyo kuwa ni utaratibu wa kawaida katika vituo vya kutolea huduma
za chanjo, baadhi ya shule zitachaguliwa na maeneo katika jamii na chanjo
itatolewa kwa njia za huduma za mkoba.
Chanjo
ya saratani ya mlango wa kizazi itatolewa katika vituo vya kutolea huduma za
afya vya serikali na binafsi bila malipo.
=30=
No comments:
Post a Comment