Taarifa kutoka afisi ya
rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya
Jumatatu usiku.
Prof. John Attah Mills
Kifo cha rais wa taifa la
pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania
tena urais.Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi
huyo.
Rais Prof. John Attah Mills ambaye
husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y
kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais
huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa
kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya
Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za
uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa
kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo Prof. John Attah Mills
alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake,
uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu
na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana "
taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais
ilisema.
Taarifa hiyo ilisema kuwa
Rais Prof. Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa
hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo
zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake
mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais Prof. John Attah Millis alisikika
siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na
hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Prof. Mills , anajulikana kwa
kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
Chanzo: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment